MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Heri ya mwaka mpya wana JF
Kwanza naomba nikiri mimi siyo chawa na siamini kwenye uchawa. Pili mapenzi yangu kwa huyu mama si ya kimahaba au kingono, bali navutiwa na jinsi alivyo nyanyuliwa na utendaji wake.
Sababu zangu:
Kwanza, huyu mama ni chaguo la Mungu. Hakuwahi utaka uraisi, bali uraisi umemtaka yeye.
Kuna wale maviongozi waliopata uongozi kiudhalimu, kuiba kura, kutesa na kukandamiza wenzao alafu wanakuja bila haya kutuambia wao ni chaguo la Mungu.
Huyu mama, haikua hivyo, yaani ameupata uraisi kwa mapenzi ya Mungu ki ukweli
Wapo wale wapiga mapambio wa tawala zilizopita na zitakazokuja wajifunze kutoka kwenye maandiko: Bwana asipoijenga nyumba, waijengao wanafanya kazi bure. Tazama: Zaburi ya 127
Pili, huyu mama ni mtenda haki, na kwa kitendo hicho atashibishwa.
Huyu mama katika kipindi kifupi cha utawala wake amefanya matendo makuu ya haki, amewagusa walioonewa, amewatoa magerezani wafungwa wa mchongo, amesambaratisha wadhalimu na magenge yao (Sukuma Gang), amerudisha matumaini yaliyopotea (mikutano ya hadhara) na sasa anajenga umoja wa kitaifa uliobomolewa kupitia Katiba Mpya.
Bwana wetu Yesu Kristu anasema heri wapatanishi, maana wao wataitwa wana wa Mungu, heri wenye njaa na kiu ya haki, maana wao watashibishwa. Tazama: Injili ya Mtakatifu Mathayo 5:6-10
Tatu, Mungu hujiinua kupitia udhaifu wetu, hivyo ukuu wa Mungu na upako wake unadhihirika
Tangu kale Mungu amefanya kazi na watu dhaifu au waliodharaulika, angalia background za manabii kama Musa na Daudi, pia na bwana wetu Yesu Kristu. Ni katika udhaifu, ukuu wa Mungu hujidhihirisha. Mungu ametaka tuwe na Rais mwanamke, katika mfumo dume wa leo, isigekua rahisi, kama si kwa mapenzi ya Mungu huyu mama kuupata urais.
Kama Mungu amempenda mama Samia Suluhu Hassani mimi ni nani wa kubisha?
Mungu anawapenda maraisi wote wa Tanzania, ila amewapenda zaidi J.K. Nyerere, Benjamin Mkapa na John Magufuli, tuendelee kuwaombea waendelee kupumzika kwa amani
Nawatakia Jumapili njema.