Nampenda sana mke wa rafiki yangu

Nampenda sana mke wa rafiki yangu

Tumezoeana kiasi cha kunifanya sasa hivi niwe serious na mpango wa kumwomba thawabu aliyojaliwa. Wandugu naombeni ushauri wa kisaikolojia juu ya suala hili kwa kuwa na yeye yupo tayari kunipatia kwa sababu nilimjaribu kumwomba siku moja aliniambia niandae mazingira.

Mkuu kwanza hongera kwa kupendwa na shemeji yako ni jambo zuri.

Pili hongera kwa angalau kulileta hili hapa kupata ushauri.

Tatu nakupa pole sana kwa kuwa unachokiendea ni kitu cha hatari sana kuliko unavyowaza. Yaani unatakiwa ukimbia kutoka hili jambo haraka haraka haraka sana. Madhara ya hili ni kubwa kwako na huyo mwanamke. Pia humu upo uzi unatoa tahadhari kwa wale wanaotaka kutembea na marafiki wa wenzi wao, umeelezea vzr sana hili jambo.

Ipo hivi;

Hivi karibuni nimeshudia kijana mmoja na rafiki yake mahusiano yao yamekufa kabisa kwa sababu ya hili. Ilikuwaje;

Jamaa walikuwa marafiki wa kutembeleana vzr kabisa na jamaa akisafiri kumbe huku nyuma jamaa yake anatoka na mke wake. Jamaa akahisi kitu. Akaweka mtego mkali katika communication link zooote za mke wake. Akampata jamaa bila shida. Na jamaa akamueleza rafiki yake juu ya tabia yake plus ushahidi.

Matokeo yake: Yule mwanamke anaishi maisha magumu kupita maelezo, ndani panawaka moto mkali hadi sasa. Urafiki wa mwanaume na mwenzake umekufa kabisa, jamaa aliyekuwa anakula mke wa mwenzake anajuta mno na anaishi kama ngedere. Mwisho wa siku unakuwa umewakosa wote wawili. Pia jamaa anakisasi cha hali ya juu ameapa kulipiza kwa namna yoyote ile.

Pia jamaa akimuacha mwanamke au ukijua kuwa hawana amani, jambo hilo litakutesa mno mno siku zote. Na pia unajiweka ktk agano ambapo siku moja na wako ataliwa.

Mwisho nakushauri hiyo biashara hailipi, hasara ni nyingi kuliko faida. Kwa kifupi unachofanya ni mauaji, jamaa yako atabaki na maswali mengi mno kiasi kwamba anaweza kuchanganyikiwa endapo atajua. Na mwanamke akiachika ni heri kwake ila asipoachika hata aminika teeena na atakuwa kama raia daraja la pili ktk nyumba yake mwenyewe. Na kwako pia itakufanya usiaminike na hata marafiki zako wanaweza kukukwepa endapo watajua.
 
Tumezoeana kiasi cha kunifanya sasa hivi niwe serious na mpango wa kumwomba thawabu aliyojaliwa. Wandugu naombeni ushauri wa kisaikolojia juu ya suala hili kwa kuwa na yeye yupo tayari kunipatia kwa sababu nilimjaribu kumwomba siku moja aliniambia niandae mazingira.
Kama kweli ni your best friend nakushauri umwombe akupatie huyo shemeji yako. Kwanini unatuuliza sisi wakati nyie ndo marafiki? Omba akupatie na ikiwezekana badilishaneni - mpe wa kwako naye akupe huyo unayetaka. Naamini kama marafiki mnafanana hadi vichwani (wewe na rafikiyo)
 
Kwa hiyo, kwa roho saafi kabisa unataka tukuunge mkono mpango wako wa kutaka kujaza ujazwe?? Haya; kama yupo atakayeona ni vyema unafanya, sawa. Ila; angalia sana ndg usije lia kilio cha mbwa kidomo juu. Utakapo shikishwa ukuta mbele za huyo huyo mke wa mtu, usijali kwani ulijua kuwa ndiko unakoelekezwa na mke wa mtu.
Waweza kujiona kuwa na miguvu na kivua kipana. Hayo kajiangalie chumbani mwako sio mbele ya mke wa mtu. Utakapofumaniwa, utajikuta mdogo ka piriton.
Hahahaha
 
Hivi unaomba ushauri au, toa ufirauni wako hapa tena mwezi huu wa Ramadhani, usitutie majaribuni kaa na ibilisi wako.
 
JF Founders wana akili sana!
WALICHEZA KAMA PELE KUWEKA OPTION YA KUTUMIA MAJINA FEKI!
Nawaza hapa unamshauri mtu kumbe ni best yako!
na mke anayemzungumizia ni mkeo!
AF UMEKAZANA KUMSISITIZA MLEEE TUUU! SI KAJILETA!
AHAHHHAHAHHAHAHHAHAHHA
Hahahaha...aisee, nmecheka sana.
 
Unapoandaa mazingira usisahau kuandaa na babycare.

Tumezoeana kiasi cha kunifanya sasa hivi niwe serious na mpango wa kumwomba thawabu aliyojaliwa. Wandugu naombeni ushauri wa kisaikolojia juu ya suala hili kwa kuwa na yeye yupo tayari kunipatia kwa sababu nilimjaribu kumwomba siku moja aliniambia niandae mazingira.
 
JF Founders wana akili sana!
WALICHEZA KAMA PELE KUWEKA OPTION YA KUTUMIA MAJINA FEKI!
Nawaza hapa unamshauri mtu kumbe ni best yako!
na mke anayemzungumizia ni mkeo!
AF UMEKAZANA KUMSISITIZA MLEEE TUUU! SI KAJILETA!
AHAHHHAHAHHAHAHHAHAHHA
Hahahaaaa!!
 
Back
Top Bottom