Nampongeza Askofu Rugambwa wa Nyaishozi kwa Kuteuliwa kuwa Kardinali Mpya

Nampongeza Askofu Rugambwa wa Nyaishozi kwa Kuteuliwa kuwa Kardinali Mpya

Mpk sasa Tanzania tumekua na makadinali wangapi?

1688929731973.png


Watatu!
 
Hivi huyu anauhusiano gani na yule Kardinali wa kwanza Tanzania?
Nilimuuliza yeye mwenyewe swali hilo miaka mitano iliyopita. Akajibu kwamba hana undugu na Kardinali Laureano Rugambwa. Isipokuwa baba yake walikuwa marafiki wa karibu sana na marehemu Kardinali Laureano Rugambwa. Wakati marehemu anatawazwa kuwa Kardinali mjini Dar es Salaam mwaka 1960, baba wa Protase Rugambwa alisafiri kutoka Kagera kuja Dar kuhudhuria sherehe hiyo, akimwacha mama yake Protase hospitali akingojea kujifungua. Akaahidi kwamba kama mtoto atakuwa mwanaume atamwita Rugambwa na atafanya juu chini mpaka naye awe Kardinali kama Laureano. Hayo ndiyo yametimia.
 
Nje ya mada:
Mimi huvutiwa sana na hoja zako, uko sober na una upeo mkubwa sana. Mimi huamini, moja ya jambo huwajenga watu ni vitabu.

Aidha hapa au kwa uzi mwingine (kwa faida ya bibliophiles wengine pia), naomba uniorodheshee vitabu unavyovipenda, walau kumi.
 
View attachment 2683335
Kardinali Rugambwa akiwa na Rais Kikwete, lakini kabla hajawa Kardinali

Kwa dhati, nampongeza Askofu Rugambwa wa Nyaishozi Karagwe, mkoani Kagera, kwa Kuteuliwa kuwa Kardinali Mpya.

Nawapongeza waumini wa Nyaishozi Karagwe, mkoani Kagera, kwa kumzaa na kulea Kardinali Rugabwa.

Pia nawapongeza wanafunzi wake wote wa Seminari Ndogo ya Katoke, Biharamulo kwa mwalimu wao kuwa Kardinali.

Pia namkaribisha sana Kardinali Rugambwa huku kwetu "Sumbawanga Town".

Wote tumwekeni katika maombi.
Hilo lina manufaa gani kwa taifa?
 
Leta ushahidi wa kuwa Rugambwa kazaliwa Karagwe kwanza ndo mengine yafuate.

Matatu:

1. Umeninukuu vibaya. Sijasea alizaliwa Karagwe.

2. Sio kila mtu anayezaliwa eneo linalokaliwa na kabila X ni kabila X, kama ambavyo sio kila mtu anayezaliwa Tanzania ni Mtanzania.

3. Wasifu wa Kardinali Protase Rugabwa huu hapa:

Wasifu wa Askofu mkuu Protas Rugambwa​


Askofu mkuu Protas Rugambwa alizaliwa kunako tarehe 31 Mei 1960, Bunena, Jimbo Katoliki la Bukoba.

Alipata majiundo yake ya Kipadre kutoka katika Seminari ndogo za Katoke iliyoko Rulenge-Ngara na Itaga, Jimbo kuu la Tabora.

Kwa masomo ya Falsafa alipelekwa Seminari kuu ya Kibosho iliyoko Jimbo Katoliki la Moshi na Masomo ya Taalimungu aliyapatia Seminari kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga, maarufu kama Segerea.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, alipadrishwa kunako tarehe 2 Septemba 1990, Jimbo kuu la Dar es Salaam wakati wa Hija ya Kichungaji ya Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili nchini Tanzania.

Yeye alikuwa ni kwa ajili ya Jimbo Katoliki Rulenge kwa wakati huo. Baada ya Upadrisho alifanya utume Parokiani, Seminari Ndogo ya Katoke, Mwenyekiti wa Idara la Liturjia Jimbo Katoliki Rulenge na Mhudumu wa shughuli za kiroho Hospitali ya Biharamulo.

Kuanzia mwaka 1994 hadi 1999 alipelekwa mjini Roma kwa masomo kwa masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano na kujipatia Shahada ya Uzalimivu katika shughuli za kichungaji.

Baada ya kurudi Jimboni mwake Rulenge, alipangiwa kuwa Mwalimu na Mkurugenzi wa miito na Mkurugenzi wa shughuli za Kichungaji; Makamu Askofu.

Kunako mwaka 2002 hadi 2008 aliombwa kwenda kusaidia kutoa huduma za kichungaji kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, utume ambao aliufanya kwa ufanisi mkubwa.

Kunako tarehe 18 Januari 2008, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, akamteuwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Tanzania na kuwekwa wakfu hapo tarehe 13 Aprili 2008.

Baada ya Askofu Protas Rugambwa kuwafundisha, kuwaongoza na kuwatakatifuza Watu wa Mungu Jimbo Katoliki Kigoma, tarehe 16 Juni 2012, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, akamteua kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu na Rais wa Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa.

Chanzo: Wasifu wa Askofu mkuu Protas Rugambwa
 
Hilo lina manufaa gani kwa taifa?

Swali lako ni sawa na kuuliza: Viongozi wa dini wana manufaa gani kwa Taifa?

Na jawabu lake ni hili hapa:

1. Ni wadau muhimu katika ujenzi wa imani ya jamii

2. Ni wadau muhimu katika ujenzi wa jamii ya amani

3. Ni wadau muhimu katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kardinali Protase Rugambwa anahusika katika yote matatu

Vyanzo:

Mosi: https://www.jw.org/sw/maktaba/magazeti/w20060901/Dini-Ina-Faida-Gani/

Pili: Nguvu ya dini katika siasa za Tanzania - BBC News Swahili

Tatu: Dignitatis Humanae
 
View attachment 2683335
Kardinali Rugambwa akiwa na Rais Kikwete, lakini kabla hajawa Kardinali

Kwa dhati, nampongeza Askofu Rugambwa wa Nyaishozi Karagwe, mkoani Kagera, kwa Kuteuliwa kuwa Kardinali Mpya.

Nawapongeza waumini wa Nyaishozi Karagwe, mkoani Kagera, kwa kumzaa na kulea Kardinali Rugabwa.

Pia nawapongeza wanafunzi wake wote wa Seminari Ndogo ya Katoke, Biharamulo kwa mwalimu wao kuwa Kardinali.

Pia namkaribisha sana Kardinali Rugambwa huku kwetu "Sumbawanga Town".

Wote tumwekeni katika maombi.
Mkuu mm pia Ni mkkkt mtihifu sna I'll kwa Hili siko nyuma kumpongeza kwa dhati kadinali huyu kuteuliwa kuwa kadinali na Papa wa sasa ndgu fransico .nampongeza Kweli Kweli kwa hatua na nafsi hyo kubwa kwake na taifa hili changa la mwenyenzi mungu ,mungu ametupa .nampongeza mno pia kwa kutokea kwake ktk Jimbo kuu katoliki tabora akiwa awali akiwa askofu mwandamizi wa Jimbo kuu Hilo la tabora



Je swalli langu kuu jee itammlazimu kuamia jimbo kuu la DSM Kama makaz yake na shughuli zake za kitume au atabakia tabora???


Bila Shaka unatokeaa ktk parokia ya kristo mfalme hapo mjini sumbawanga ambapo mm niliwahi pia kutumika katk Jimbo Hilo
 
Magufuli angekuwepo angefurahi sana. Mungu amuweke mahali pema peponi alikuwa na macho ya rohoni
Angemfanyia dhifa ya kitaifa ktk ikulu ya chamwino ,dodoma na ingependeza pia
Ningefurahi hudhuria
Ingawaa mm Ni mkkkt mtihifu ila Roma Catholic Ni baba lao kwanza kutoa Marais kwa wakati wote pia kuwa kanisa lisilo yumbishwa na watumisha wake Kama padri au paroko Kama tunavyo sumbuliqa ssi kkkt na kina mwaikali wa mbeya
 
... wachaga wamekosea wapi? Ndio wanaongoza kwa idadi ya maaskofu, mapadre, masista, mashemasi, n.k. Anyway, uamuzi wa Papa ni alfa na omega; wanavyosema wao signature yake ni mwisho.
Wacha ukabila, sisi sote ni Watanzania hakuna cha mchaga wala mhaya. Kubwa ni elimu ya dini, maadili na uwezo wa kiuongozi ndizo nguzo za kufika hapo alipofika Protace Cardinal Rugambwa
 
Je inawezekana Mzungu, Mwarabu, na Mhindi kwao ikawa Tanzania?
Think again!
Sijawahi sikia mnyambo anaitwa Rugambwa kwanza.
Ndio kwa kuzaliwa ila ethnicity itabaki yeye ni mzungu na hawezi kufanana na Waafrika wanavowaza kula kimasihara.
 
Magufuli angekuwepo angefurahi sana. Mungu amuweke mahali pema peponi alikuwa na macho ya rohoni
Ni vizuri amepata u cardinal wake wakati huyo mwendazake amekufa. Mungu alijuwa hilo kwa kuwa kupata nafasi hiyo na Magufuli akiwa hai ingekuwa ni najisi. Yule shetani alilitumia kamisa vibaya
 
Back
Top Bottom