Nampongeza Rais Samia na Serikali yake Kudhibiti uvujaji wa siri na Nyaraka za Serikali

Mapinduzi Zanzibar picha za watawala waliopo madarakani zimetamalaki kuliko picha za John Gideon Okello na wenzake. Abeid Karume aliyekuwa DSM siku ya mapinduzi anaitwa shujaa.

Umeweza kukubali kuwa kuna Tanzania bara na Zanzibar wakati ukweli ni Tanganyika na Zanzibar hii mtawala wanataka kuficha.

Wameshindwa kueleza Rasilimali zetu zina faida gani. Unawekwa ujinga kwenye siri za watu kutaka kuongoza kwa ufisadi.
Embu Tuliza akili kwanza, kwani wewe hujaona hatua za kimaendeleo tulizopiga Kama Taifa
 
Ina uhusiano Gani na utopolo ulioandika? Hata maskini ana maendleo inategemea maendeleo unaya define vipi! Nilikuomba CV yako ukakimbia kuficha ujinga WAKO!
Alokudanganya hii ni Njia ya uteuzi amekupoteza ndio maana sasa unataka kushika nyeti za serikali Ili ishtuke!
Ndio mana gt kama kina Pasco au gentamicin au johnthepatist huwakuti wakichagia kwenye hizi takataka zako!

Uwe unasoma kabla ya kuandika,angalia niliyekuwa namjibu na alivyokuwa ameuliza,
 
Ucwe mzalendo.mjinga
Ndugu zangu watanzania,

Kuna kipindi kulikuwa Kuna washangaza wazalendo wengi Sana juu ya Uvujaji na usambaaji wa Siri na Nyaraka za Siri za serikali, watu walikuwa wanaona fahari kuvujisha Siri za serikali na Nyaraka za serikali, ilikuwa Ni kawaida kukuta na kuona mitandaoni habari nyeti za serikali. Nilikuwa najiuliza ujasiri huo ulikuwa unatoka wapi wa kufanya hayo mambo pasipo kuhukumiwa na dhamira zao juu ya viapo vyao.vikali kimaneno.

Ndugu zangu Ili ushinde Vita ya aina yoyote Ile Ni lazima uwe msiri wa mambo yako,mipango yako,mikakati yako na mbinu zako za kimedani. Huwezi ukaishinda Vita kwa kuandika Siri za jeshi lako hadharani utafikiri pumba za mashineni, mataifa yaliyoendelea na yenye nguvu za kijeshi, kiuchumi, kisayansi, kiteknolojia, kijasusi na kiinterejensia yamefanikiwa katika suala la utunzaji wa Siri na kuzilinda Siri za mafanikio Yao kwa jasho na Damu, hawana mchezo katika suala la Siri za Taifa na Nyaraka za serikali au vyombo vya ulinzi na usalama na mipango yake.

Ifahamike kuwa kuvujisha Siri na Nyaraka za serikali ni hatari kiusalama. Ni kulivua Nguo Taifa kwa kuwa inatoa mwanya kwa maadui zetu na wapinzani wetu wa kiuchumi na hata maadui zetu kiusalama kuweza kupata mahali pa kuanzia na kujuwa udhaifu wetu ulipo, wanapata kujuwa udhaifu wetu wa kutunza mambo yenye maslahi kwa Taifa letu na hivyo kuwa Rahisi kutuhujumu kiuchumi na hata kiusalama.

Kwa bahati nzuri Tangia ameingia madarakani mama yetu mpendwa kipenzi Cha watanzania, mama imara na shupavu. Jasiri na mzalendo wa kweli Mama Samia Suluhu Hassan kumeonekana kupatiwa dawa kwa Tabia hii mbaya iliyokuwa inataka kumea hapa nchini kwa baadhi ya watumishi, kwa Sasa watu wanashindwa hata kubashiri ni nani anaweza kuteuliwa katika nafasi fulani hata Kama mh Rais akisema kuwa anataka kufanya mabadiliko mahali fulani kwa wasaidizi wake, iwe Ni kwenye chama aliko Kama Mwenyekiti au serikalini ambako Ni Rais na Amiri Jeshi mkuu amedhibiti Sana Uvujaji Wa Siri za serikali Hali iliyoleta utulivu serikalini na kuondoa Taharuki kwa wananchi, imeondoa presha na hata sintofahamu iliyokuwa ikitokea na maneno maneno.

Mimi Mwashambwa nikiwa Kama mzalendo na mpenda nchi yangu nawapongeza Sana wale wote waliokula viapo vya kutunza Siri mahali pa kazi kwa kuwa waadilifu na wenye kuzingatia viapo vyao, Nawasihi Kuendelea na moyo huo kwa maslahi mapana ya Taifa letu, kila mmoja wetu aliyepewa dhamana ahakikishe anatunza Siri za serikali kwa Kiwango Cha juu, kusiwepo kuishiwa uvumilivu katika suala la kiapo, Taifa letu Ni muhimu kuliko kitu kingine chochote, Na kila mtu ajione mwenye hatia inayostahili adhabu Kali ya majuto na majonzi avujishapo Siri za serikali.

Rai yangu kwa wahusika Ni kuhakikisha kuwa maafisa wote serikalini wanazingatia viapo vyao, isitokee hata kwa bahati mbaya mambo ya serikali yanatoka nje na kuleta Taharuki na kutetemesha usalama wetu, kila mmoja aliyepewa dhamani Ahakikishe anakuwa msiri ikiwezekana hata kufa kwa ajili ya kulinda maslahi ya Taifa letu kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo.

Hongera Sana Rais wangu, Umethibitisha uimara na ushupavu wako, umetoa dira na muelekeo wa serikali yako, mausia na maonyo uliyoyatoa hadharani yamezingatiwa na sisi watanzania Tumeona matokeo yake. Tunakuamini sana Rais wetu, tunakuunga mkono, tupo bega kwa bega na wewe, tunakupigania mitaani na kukusemea kila mahali.

Tunaendelea kukuombea afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia wananchi wako, Songa mbele kwa nguvu maana tulio upande wako Ni wengi zaidi ya wale walio kinyume na wewe kwa maslahi yao binafsi, umefanikiwa Kuiteka na kuitawala mioyo ya watanzania kwa uchapa kazi wako, ndio maana unaona utulivu na Amani ukiwa umetamalaki hapa nchini.

Kazi Iendeleee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Wana chadema siwabagui Ila siku zote naamini asilimia kubwa ya wanachadema wanahitaji kuongozwa kwa kuonyesha mstari wa kupita maana bila hivyo wanaweza wakakupanda kichwani,No watu wasioeleweka na vigeu geu, wamekosa staha na adabu katika midomo Yao hasa vijana wao, wamejaa matusi wanayoweza wakam poromoshea hata anayelibgana na baba yao,hapa Rejea kimaneno michafu ya mdude chadema,katika hili nabaki na msimamo wangu kuwa Ni wanachadema wachache Sana wenye kujitambua Ila wengi wao akili zao wanazijuwa wenyewe ,hawana adabu wala staha, hawana heshima Wala busara, wamejaa mihemuko tu na majazba utafikiri wamekosa malezi na mtu wa kuwalea kimaadili
Hahaaa nikufananishe na ule mmea tena?
Kwenye mabandiko yako mengi unaandika hivi machadema kama unabisha kapitie mabandiko yako ewe usiye na kumbu kumbu.
Sasa mada yangu sio hiyo na sitaki unitoe kwenye reli! Naomba utuambia Siri za serikali ziliwahi kuvuja hapo nyuma Nani alikua anavujisha na utupe tu mifano angalau mitatu na zikahatarisha usalama WA NCHI na kukwamisha maendeleo ya taifa hili na
Mama Samia akalifanyia Kazi kwa weledi mkubwa hata Leo ukaamua kukaa chini usiku huu na kutupandishia huu uzi!

Hapa tuende hoja kwa Hoja tafadhali maana gazeti lako limesheheni mambo mengi ambayo hata yeye akisoma atashtuka.

Ninachokumbuka mwezi Nov Mwishoni alikumbusha umuhimu wa kutunza nyaraka na Siri za serikali!

Utuambie classified au secret, top secret information na confidential information zilizokua zinavuja kipindi Cha Jiwe na hata jk zikahatarisha usalama WA NCHI na kukwamisha maendeleo ya NCHI na Samia amelufanyia kazi na utuambie namna amelufanyia Kazi na wahusika kadhaa wametiwa nguvuni na hatua Gani zimechukuliwa na sasa NCHI ipo salama na ukaamua kuleta huu Uzi!

Ukishindwa kufanya hivyo nitakujibu jambo
 
Unakumbuka na unafikiri kwa Nini mh Rais aliwakumbusha watumishi juu ya kulinda Nyaraka za serikali? Unafikiri aliongea kwa bahati mbaya? Unafikiri kwanini alikemea suala Hilo na kutoa onyo kwa watu wenye Tabia ya kuwek Nyaraka za serikali mitandaoni? Unakumbuka na kuwakumbuka akina mange kimambi ! Unafahamu kilicho mpa umaarufu Hadi nyie wanachadema mkamuona Kama mkombozi wenu wa kuwasemea? Unakumbuka mlikuwa mnamshangilia na kutega masikio yenu na macho yenu kwake? Au umesahau kwa kuwa nyie huwa wasahaulifu Kama ndege
 
BBrO

Bro jibu Hoja acha kutanga tanga!
Mpaka Leo Rais akifanya uteuzi kurugenzi ya mawasiliano ikulu inaweka taarifa mitandaoni ikiwemo website ya ikulu na hata tweeter ya Rais.
Wizara ikitoa ufafanuzi au taarifa ya jambo inaweka taarifa kwenye website ya wizara na kwenye mitandaonya kijami

Kitengo Cha mawasiliano serikalini kikitoa taarifa yoyote kinaweka taarifa Hiyo kwenye website husika na tunazipata kupitia mitandaoni vile vile! Hizo Sio nyaraka za serikali? Au ni nyaraka za familia ya President!

Sasa Hoja haijajibiwa nutajie angalau Siri tatu tu za serikali zilizohatarisha usalama WA NCHI ambazo alitoa huyo unayemwita Mange kimambi ambaye najua sifa yake Kubwa ilikua ni kuitukana serikali na sidhani kama Kuna information ambayo ni secret au top secret au secret secret ambayo amewahi kuivujisha ikahatarisha usalama wa NCHI na kukwamisha maendeleo! (Kama ipo weka)

Nakukumbusha tofautusha Habari za kiuchunguzi zilizoibua kashfa mbali mbali kama kagoda, Richmond na dowans ambazo zote hizo ziliitia serikali hasara plus escrow!

Kama ndio hizo unazungumzia BASi we ni Sawa na torch isiyo na battery au charge at all!

Mange hajawahi kuwa source of information wa chadema au afisa Habari wa chadema, na kwa taarifa yako Mange ni kada wa Ccm pamoja na familia yake kama hujui Hilo na mwaka Jana kampokea Mama yako huko Marekani na kapiga nae picha! Sijui kama unajua?

Mwashambwa jitahidi kuwa critical analytic mana unaruka ruka tu ukiandika ngonjera, Mama hakukekemea alikumbusha wajibu ambako ni jambo la kawaida wewe umekurupuka huko eti amefanikiwa kudhibiti amwdhibiti maana kulikua na tatizo Sawa dogo.

Uwe unakaa chini unachanganua Nini matokeo ya ninachoandika! Maandishi hayafutiki Ndugu!

Kwa MTU mwenye akili timamu anayejua kuchambua na kufuatilia mambo katika mabandiko yako yote, unaulinganisha utawala wa Samia na utawala wa Jiwe na hali kadhalika unaonesha kuwa utawala wa Jiwe haukuwahi kufanya chochote!
Sasa nikwambie kwa tabia ya CCM wewe unahesabika kama msaliti mchumia tumbo, akija Rais mwingine utamponda Samia indirect na kwa maana Hiyo namba Yako ya cm itabakia dormant Hivyo tu don't expect any call from madam president!

Leo umeanza kuzungumzia Siri za NCHI as if wewe ni mchambuzi wa maswala ya usalama na Sio siasa tena! Kesho utshindwa kuizungumzia TISS na muundo wake na kumpongeza Rais kwa kuiunda vyema as if unamsaidia kufanya vetting?
Pathetic mediocre!
Kuchamba mwingi kushika mavi!
Jibu hayo maswali hapo Nimekaa pale

Mit 26:4-12
Mit 26:4-12 SUV
Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye. Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake. Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu. Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.
 
Aliyekuwa anavujisha siri kipindi kile na kumpa kigogo 2014 ndiye kawa rais unategemea nani avujishe .
 
Aliyekua anavujisha ni kigogo, kigogo kashika mpini zinaanzaje kuvuja. Mchawi mpe mwana alee
 
Zitaje basi ni zipi hizo siri zilizovuja
Waliokuwa wanavujisha siri ni wale wale wa lile genge la kifisadi ambao jiwe alikuwa anapambana nao na kuna wenzao jiwe aliwaamini na kuwaingiza ndani ya serikali.
 
Mchawi mpe mtoto wako akulelee hawezi mroga au kumuua. msidhani huo msemo ulikuja bahati mbaya.

Hivi mtu anawezaje toa siri zake mwenyewe jamani? Tulisha choka mtuwache kha!
 
Ndugu zangu watanzania,

Kuna kipindi kulikuwa Kuna washangaza wazalendo wengi Sana juu ya Uvujaji na usambaaji wa Siri na Nyaraka za Siri za serikali, watu walikuwa wanaona fahari kuvujisha Siri za serikali na Nyaraka za serikali, ilikuwa Ni kawaida kukuta na kuona mitandaoni habari nyeti za serikali. Nilikuwa najiuliza ujasiri huo ulikuwa unatoka wapi wa kufanya hayo mambo pasipo kuhukumiwa na dhamira zao juu ya viapo vyao.vikali kimaneno.

Ndugu zangu Ili ushinde Vita ya aina yoyote Ile Ni lazima uwe msiri wa mambo yako,mipango yako,mikakati yako na mbinu zako za kimedani. Huwezi ukaishinda Vita kwa kuandika Siri za jeshi lako hadharani utafikiri pumba za mashineni, mataifa yaliyoendelea na yenye nguvu za kijeshi, kiuchumi, kisayansi, kiteknolojia, kijasusi na kiinterejensia yamefanikiwa katika suala la utunzaji wa Siri na kuzilinda Siri za mafanikio Yao kwa jasho na Damu, hawana mchezo katika suala la Siri za Taifa na Nyaraka za serikali au vyombo vya ulinzi na usalama na mipango yake.

Ifahamike kuwa kuvujisha Siri na Nyaraka za serikali ni hatari kiusalama. Ni kulivua Nguo Taifa kwa kuwa inatoa mwanya kwa maadui zetu na wapinzani wetu wa kiuchumi na hata maadui zetu kiusalama kuweza kupata mahali pa kuanzia na kujuwa udhaifu wetu ulipo, wanapata kujuwa udhaifu wetu wa kutunza mambo yenye maslahi kwa Taifa letu na hivyo kuwa Rahisi kutuhujumu kiuchumi na hata kiusalama.

Kwa bahati nzuri Tangia ameingia madarakani mama yetu mpendwa kipenzi Cha watanzania, mama imara na shupavu. Jasiri na mzalendo wa kweli Mama Samia Suluhu Hassan kumeonekana kupatiwa dawa kwa Tabia hii mbaya iliyokuwa inataka kumea hapa nchini kwa baadhi ya watumishi, kwa Sasa watu wanashindwa hata kubashiri ni nani anaweza kuteuliwa katika nafasi fulani hata Kama mh Rais akisema kuwa anataka kufanya mabadiliko mahali fulani kwa wasaidizi wake, iwe Ni kwenye chama aliko Kama Mwenyekiti au serikalini ambako Ni Rais na Amiri Jeshi mkuu amedhibiti Sana Uvujaji Wa Siri za serikali Hali iliyoleta utulivu serikalini na kuondoa Taharuki kwa wananchi, imeondoa presha na hata sintofahamu iliyokuwa ikitokea na maneno maneno.

Mimi Mwashambwa nikiwa Kama mzalendo na mpenda nchi yangu nawapongeza Sana wale wote waliokula viapo vya kutunza Siri mahali pa kazi kwa kuwa waadilifu na wenye kuzingatia viapo vyao, Nawasihi Kuendelea na moyo huo kwa maslahi mapana ya Taifa letu, kila mmoja wetu aliyepewa dhamana ahakikishe anatunza Siri za serikali kwa Kiwango Cha juu, kusiwepo kuishiwa uvumilivu katika suala la kiapo, Taifa letu Ni muhimu kuliko kitu kingine chochote, Na kila mtu ajione mwenye hatia inayostahili adhabu Kali ya majuto na majonzi avujishapo Siri za serikali.

Rai yangu kwa wahusika Ni kuhakikisha kuwa maafisa wote serikalini wanazingatia viapo vyao, isitokee hata kwa bahati mbaya mambo ya serikali yanatoka nje na kuleta Taharuki na kutetemesha usalama wetu, kila mmoja aliyepewa dhamani Ahakikishe anakuwa msiri ikiwezekana hata kufa kwa ajili ya kulinda maslahi ya Taifa letu kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo.

Hongera Sana Rais wangu, Umethibitisha uimara na ushupavu wako, umetoa dira na muelekeo wa serikali yako, mausia na maonyo uliyoyatoa hadharani yamezingatiwa na sisi watanzania Tumeona matokeo yake. Tunakuamini sana Rais wetu, tunakuunga mkono, tupo bega kwa bega na wewe, tunakupigania mitaani na kukusemea kila mahali.

Tunaendelea kukuombea afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia wananchi wako, Songa mbele kwa nguvu maana tulio upande wako Ni wengi zaidi ya wale walio kinyume na wewe kwa maslahi yao binafsi, umefanikiwa Kuiteka na kuitawala mioyo ya watanzania kwa uchapa kazi wako, ndio maana unaona utulivu na Amani ukiwa umetamalaki hapa nchini.

Kazi Iendeleee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
umeandika kwa kujipendekeza,hajadhibiti ila anaishi nao vema kwa kiasi.
 
Back
Top Bottom