Namsaidiaje mdogo wangu huyu angalau awe msafi?

Namsaidiaje mdogo wangu huyu angalau awe msafi?

Hello members!!!

Ni mdogo wangu wa mwisho wa kiume miaka 17+ Nashindwa kuelewa ni malezi au nini. Ila mbona sie wengine ndugu zake hatuko hivyo.
Naanza kuhofia asije kuona namnyanyasa.

Yaani unaweza kurudi home unakuta kakaa na mavyombo machafu hana habari. Vitu viko hovyo, kupangilia kila kitu kiwe pahala pake, mfano amekula mavyombo kaacha hapo. Kupika anajua ila usafi wa pale anakopikia ni hadi umkumbushe wee naniii embu safisha safisha kidogo hapo sehemu ya kupikia.

Hapo nje anaingia na kutoka ndani, unarudi unakuta mamchanga yamejaa, kabla sijaingia ndani nafanya kuyafagia kidogo mazingira ya nje. Unaweza kuta kitanda hakijatandikwa na yupo tu kashinda nyumbani sijui ni uvivu au ndio uchafu wenyewe. Siku narudi naingia chumbani nakuta kitanda kiko vururuvururu alivyoamka ndivyo hvyo hivyo,(kidogo nimzabe makofi) hapa alijirekebisha. Mbaya zaidi kila siku namsema. Sio kwamba me ni msafi saaana ila kiukweli me angalau.

Kuhusu usafi wake binafsi hana shida sana.

Nashindwa kuelewa kimalezi mzee alifariki akiwa bado mdogo kama 2-3yrs hivi. Alilelewa zaidi na mama pekee. Nawaza labda malezi ya mzazi mmoja ndio sababu.

Sasa naanza kuona huyu dogo labda anaona tu broo wake nina nongwa.[emoji1]
Mfundishe kwa maongezi na vitendo pia,na kwskuwa ni mdogo bado atakuelewa
 
Weee, wacha kumsimanga chalii,. By necha wanaume wengi tuko hivo. Cha kumsaidia sio makelele yako, mweke kwenye target apate pisi kaliii. Af hiyo pisi iwe inakuja kumsalimia hapo ghetto mara kwa mara. Utaona patakavokua panang'aa. As long as hakuna external factor, mwanaume yuko tayari kufikiria jinsi ya kupata hela rather than trivial matters kama vile ndala yenye mchanga. Muhimu hanuki mdomo na kikwapa. Hizo vingine zinavumilika tu. Lakini tukiskia mtoto mzuri anakuja na kuna uhakika wa kupiga mbususu, usafi utakaokuwepo ni wa 5 star hotel
 
Kawaida hiyo
Mwanaume anatakiwa kuwa hivyo

Waoaji ndio wanavyokuwa,dogo atakuja kuoa mapema sana

Usiogope
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hilo limenirithi mimi babu yake. Mimi hata neti naonaga uvivu kupandisha... nachomoka na kuingia kama panya dadeki
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna jamaa yangu mpaka alishindwana na manzi wake.

Imagine mrembo anampigia nguo pasi, jamaa linaona haitoshi linapasi upya tena mbele yake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbona kwa ulivyoelezea sio too much

Manake mie pia nina mdogo wa kiume umri 17+ yeye ni mvivu hadi akitafuna big G anaona uvivu kuitupa nje anabandika ukutani
Mzabue na wewe uhame home uolewe
 
Mkuu madogo wako hivyo, nilikua na dogo langu huyo wa kiume akitoka shule hanawi ni direct jikoni, kama ngedere, akimaliza kula utakuta maganda ya ndizi mezani, sukari imetapakaa, hapo kamaliza.

Inakubidi wewe ndio uanze usafi huku huna la kuongea, unahisi kila muda ukimwambia atahisi una personal issues na kwa jinsi tunavyopenda madogo zetu unakaa kimya.

Nilipohamia kwangu, nilimwambia kabisa ni marufuku kuingia jikoni kwangu hujanawa mikono tena na sabuni.

Ukiamka asubuhi jambo la kwanza tandika kitanda, habari ya kukaa siku 2 huogi kama mbuzi ifeee!!

Inshort dogo kanyooka nilimwambia hapa si kwenu hapa ni kwangu, my house my rules, dogo kanielewa na anajua nampenda, mambo madogo madogo haya huwa namsaidia sana.
 
Kumbe dume.
Nadhani ungeona magheto ya wahuni mtaani wenye umri kama huo mbona dogo lako tuzo ya usafi.!
 
Kawaida hiyo
Mwanaume anatakiwa kuwa hivyo

Waoaji ndio wanavyokuwa,dogo atakuja kuoa mapema sana

Usiogope
Kutokuwa smart si kawaida na siyo sifa na si kigezo au kisababishi cha kuoa mapema, kuna sababu mbalimbali zinazomsukuma mtu kuoa mapema mbali na hiyo uliyoianisha, maisha hayana kanuni maalum.
 
Mkuu acha kukufuru Mungu, dogo hana shida wee ndio mwenye shida unataka dogo awe kama wewe wakati wewe hujawa kama waliokulea,kila mtu ana mapungufu yake kaka na kuna ambavyo amejaaliwa wewe haujajaaliwa,kama hvyo kupika huenda ewe hupendi n,k.


Angekua msafi sana ungekuja na lawama huku oooh dogo simuelew mbona msafi sana usikute sio ridhiki,,,haya ameamua jentoman bdo unakua mkali.

Embu relax.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom