nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,902
- 2,488
Kwasababu ushamsema, anatarajia utasema tena na tena, sio kwasababu anapenda kusemwa, hapana, ila ni kwamba hivyo unavyotaka awe ni jambo analotakiwa akue, yani ajifunze, akue kiakili kufikia hatua hiyo.Hello members!
Ni mdogo wangu wa mwisho wa kiume miaka 17+ Nashindwa kuelewa ni malezi au nini. Ila mbona sie wengine ndugu zake hatuko hivyo. Naanza kuhofia asije kuona namnyanyasa.
Yaani unaweza kurudi home unakuta kakaa na mavyombo machafu hana habari. Vitu viko hovyo, kupangilia kila kitu kiwe pahala pake, mfano amekula mavyombo kaacha hapo. Kupika anajua ila usafi wa pale anakopikia ni hadi umkumbushe wee naniii embu safisha safisha kidogo hapo sehemu ya kupikia.
Hapo nje anaingia na kutoka ndani, unarudi unakuta mamchanga yamejaa, kabla sijaingia ndani nafanya kuyafagia kidogo mazingira ya nje. Unaweza kuta kitanda hakijatandikwa na yupo tu kashinda nyumbani sijui ni uvivu au ndio uchafu wenyewe.
Siku narudi naingia chumbani nakuta kitanda kiko vururuvururu alivyoamka ndivyo hvyo hivyo,(kidogo nimzabe makofi) hapa alijirekebisha. Mbaya zaidi kila siku namsema. Sio kwamba me ni msafi saaana ila kiukweli me angalau.
Kuhusu usafi wake binafsi hana shida sana.
Nashindwa kuelewa kimalezi mzee alifariki akiwa bado mdogo kama 2-3yrs hivi. Alilelewa zaidi na mama pekee. Nawaza labda malezi ya mzazi mmoja ndio sababu.
Sasa naanza kuona huyu dogo labda anaona tu broo wake nina nongwa.[emoji1]
Yani japo unamuona mkubwa, bado hajakua kujitambua kufanya mazingira ya hapo nyumbani yawe kama unavyotamani
Kwakua ushamwambia, next time ukiona pako hivyo usimuongeleshe sana
Mkumbushe tu, mwambie "naomba mazingira ya hapa yawe kama ninvyoyataka yawe" halafu endelea na mambo yako, mwenyewe ataanza usafi
Halafu utakuwa umemuendolea hofu, ila hiyo itamsaidia kukua
Kukua tunatofautiana, ndio maana kuna watu wanajimudu kiusafi bado wadogo wengine wanachelewa, huyo mpe nafasi ya kukua
Au mkalishe chini mwambie aandike ratiba, ajiorodheshee kazi za kufanya kila siku, mfano kutandika kitanda kusafisha vyoo na vyombo, hizo ziwe kila siku
Halafu awe na kazi za mara mbili au mara moja kwa wiki, mfano kufua,
Awe na kazi za walau mara moja kwa mwezi kama kufua mataulo mashuka etc
Utamsaidia kukua
Nasema hivi kwasababu hiyo ni changamoto ambayo hata mimi najitahidi kukabiliana nayo,
Usafi, usafi jambo ambalo najitahidi kulimudu, ila nimegundua ratiba tu ya kazi zipi nifanye mara ngapi kwa muda gani, ndio inanisaidia