Namsaidiaje mdogo wangu huyu angalau awe msafi?

Kwasababu ushamsema, anatarajia utasema tena na tena, sio kwasababu anapenda kusemwa, hapana, ila ni kwamba hivyo unavyotaka awe ni jambo analotakiwa akue, yani ajifunze, akue kiakili kufikia hatua hiyo.

Yani japo unamuona mkubwa, bado hajakua kujitambua kufanya mazingira ya hapo nyumbani yawe kama unavyotamani

Kwakua ushamwambia, next time ukiona pako hivyo usimuongeleshe sana
Mkumbushe tu, mwambie "naomba mazingira ya hapa yawe kama ninvyoyataka yawe" halafu endelea na mambo yako, mwenyewe ataanza usafi

Halafu utakuwa umemuendolea hofu, ila hiyo itamsaidia kukua

Kukua tunatofautiana, ndio maana kuna watu wanajimudu kiusafi bado wadogo wengine wanachelewa, huyo mpe nafasi ya kukua


Au mkalishe chini mwambie aandike ratiba, ajiorodheshee kazi za kufanya kila siku, mfano kutandika kitanda kusafisha vyoo na vyombo, hizo ziwe kila siku

Halafu awe na kazi za mara mbili au mara moja kwa wiki, mfano kufua,

Awe na kazi za walau mara moja kwa mwezi kama kufua mataulo mashuka etc

Utamsaidia kukua

Nasema hivi kwasababu hiyo ni changamoto ambayo hata mimi najitahidi kukabiliana nayo,

Usafi, usafi jambo ambalo najitahidi kulimudu, ila nimegundua ratiba tu ya kazi zipi nifanye mara ngapi kwa muda gani, ndio inanisaidia
 
Madogo wa huo umri ndio zao
Yupo mmoja alikuwa haogi kabisaaa na joto lote la mwezi wa 2 dar...boxer hazifuliwi basi hyo harufu mkipishana unataman urudishe chenchi
Hata mtaani madogo wa umri huo walio wengi ninapokutana nao huwa wanatema balaa
 
Mkuu unajisikiaje mtu mwenye akili timamu umekaa vyombo vinanuka hapo karibu. ulipokaa ni pachafu au pako rough.
Ishu ni ile tu usafi wa kawaida kama binadamu mwenye utashi na sio mbuzi au kuku.
 
Bado hakajaanza kupiga madem miti.

Na hasa kama katawaleta hapo hapo home.

Sababu yeye atasafisha na hao wapigwaji pia watataka wasafishe.

Afu hapo ndo pakustuka kwamba dogo sasa anashiba vizuri.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…