Nadhani kisa cha huyu doctor aliyesimamishwa kazi na Waziri Gwajima kwa sakata la ugonjwa ulioibuka huko Chunya, Mbeya kitampa jibu zuri sana kwa nini madaktari na wafanyakazi wengine wengi wanaamua kukimbia ajira za serikalini na kuingia private sector.
Ukweli ni kwamba katika awamu ya uongozi wa Magufuli, kufanya kazi serikalini, na hasa ukiwa na madaraka fulani imekuwa kero sana. Uongozi wa juu umesimamia zaidi kwenye siasa na kujipendekeza kwa Magufuli kuliko taaluma za kazi. Viongozi seikalini wamekuwa waoga wa kufanya maamuzi, na mara nyingine hata kuchukua msimamo kwamba ni bora kutofanya chochote kuliko kufanya kitu halafu Magufuli au waziri wakakutumbua.
Sasa kazi katika mazingira kama hayo inakuwa very stressful - kwanza mtu unakuwa na stress za kazi, na pili unakuwa na stress za kiongozi mwenye nidhamu ya woga anaegopa kufanya maamuzi au anaefanya maamuzi ili kujipendekeza au kujikosha kwa Magufuli asitumbuliwe yeye!
Kwa hiyo Magufuli anapaswa kuelewa kwamba kwa sasa kufanyia kazi serikali ni kujitafutia stress zisizo la lazima zinazoweza kukuaa kabla ya wakati wako, na kadiri unavyokuwa na madaraka ndivyo stress zinavyozidi.
Mfano mzuri ni huyu Waziri Gwajima, alivyokurupuka kumsimamisha kazi huyu daktari. Gwajima hakufanya hivyo kama taratibu za kazi, bali amefanya hivyo kumu-impress Magufuli - na ni wazi amefanya uamuzi mbaya na wa uonevu. Sasa huyu doctr akienda private sector, au madaktari wengine wakifanya hivyo kwa kuepuka hii mihemuko ya kisiasa kwenye taaluma mtawalaumu?