Namshauri Diamond Platnumz amsajili Aslay, WCB

likandambwasada

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
5,402
Reaction score
6,081
Baada ya kundi la yamoto Band kuvunjika vipande vipande huku kila mmoja akionesha ufundi wa kuimba kivyake, ni wazi kuwa msanii kijana kabisa ASLAY ameonekana kumudu kuimba nyimbo nzuri bila kutegemea nguvu ya kundi.

Ni dhahiri kwamba Aslay anajua kuimba na kipaji kizuri cha Muziki.

Hata hvyo, wahenga walisema, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Kama aslay angekuwa na management nzuri basi angekuwa msanii hatari zaidi licha ya umri wake kuwa mdogo.

Namshauri Diamond platnumz amsajili huyu dogo ili kuendelea kuongeza ladha zaidi ya WCB ambayo itakuwa imekamilika kwa wachezaji wakali zaidi kwa sasa na baadaye.
 
Aslay anauweza wakujitegemea.

wcb wakisajili wanamziki wakali wote kutakuwa na monopoly kwenye mziki.
 
HAYA NI MAONI YANGU WAKUU

KAMA NILIVYOSEMA AWALI, KIKWAZO CHA ASLAY NI MANAGEMENT MBOVU HVYO ATAFANYA KAZ NGUMU MAFANIKIO KIDUCHU.
 
Aslay,Baraka da prince na Mbosso ni suala la mda tu WCB chama kubwa
 
Nyimbo za aslay karibu zote zinafanana!!
 
Aslay ni zaidi ya WCB yote combined abaki peke yake jamaa ana kipaji matata
 
Eti akasaini lebo ya kiba....hahahaa kiba mwenyewe anahitaji msaada wa kusainiwa...
Afu aslay ana nyimbo za kufanana tatizo,daima ukiwa na kazi za aina moja ni rahisi kupotea
 
Eti akasaini lebo ya kiba....hahahaa kiba mwenyewe anahitaji msaada wa kusainiwa...
Afu aslay ana nyimbo za kufanana tatizo,daima ukiwa na kazi za aina moja ni rahisi kupotea
kwenye kufanana kwa nyimbo zake hapo nakubali kwa asilimia 100 lakini nadhani ni tempo za instrumental anazoimbia.

ajaribu kubadiri tempo za instru lakini jamaa anakipaji hakuna wakumfananishanae.
 
Kwani diamond mjinga akaribishe upinzani, kwanza watambana bana sana yani hutosikia tena akitoa ngoma kila siku
Diamond ni mfanyabiashara! Ingekuwa wa kuogopa upinzani asingethubutu kumchukua Mavoko!!!

But all in all, haya mambo is more than kuwa na sauti mzuri au kuimba vizuri! Kwani ni nani mfuatiliaji wa muziki Tanzania asiemfahamu Aslay?! But still, ukimweka na Diamond Aslay anaonekana kama ni kichuguu mbele ya mlima ya Kilimanjaro kwa sababu, isn't all about ni namna gani unavyojua kuimba but your influence and power in the industry bila kusahau nyota kwa sie tunaoamini mambo ya Kiswahili!
 
ni swala la mdaa tu kabla dogo ajampiku daimond, nadhani kilichokuwa kina mchelewesha dogo ni ile yamoto band .... daimond hana cha kumzidi aslay.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…