Namshauri Jaji Mkuu ajiuzulu

Namshauri Jaji Mkuu ajiuzulu

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Kinachofanyika mahakamani kwa miezi mitatu mfululizo ni ishara kwa muhimili wa mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake na kutekeleza maelekezo ya serikali.

Kwa kuwa mkuu wa muhimili wa mahakama ni yule yule aliyekuwepo wakati watu wanaonewa na kubambikiwa kesi na kwa kipindi chote hicho alikaa kimya, naomba busara imwelekeze Jaji Mkuu kuachia ngazi na kuruhusu usukaji upya wa muhimili wa mahakama unaoweza kusimamia haki.

Muhimili huu ukiendelea kusikiliza serikali inataka nini na kutekeleza dhana ya separation of power haitakuwa na maana nchini.

Mzee nikuombe utafakari Kama uliyowafanyia wananchi wa Tanzania kwa miaka mitano yanakushuhudia kuendelea kukalia hicho kiti. Najua ulisukumwa kuminya haki na ukatekeleza kinyume na kiapo chako. Kukaa pembeni si dalili ya kushindwa Bali nikuiombea mahakama msamaha kwa wannchi na kupunguza lawama na dhambi ulizochuma ukiwa hapo juu.

Watanzania wanalia na kuumia kwa kupoteza wapendwa wao wakiwa jela au wengine kufariki kwa presha kwa kusikia wapendwa wao wapo ndani. Wengine Ni walemavu na baadhi familia zimesambaratika, jitafakari.
 
Naunga mkono. Jaji Mkuu hawezi kutenganishwa na ubinyaji haki uliofanyika 2015-21. Ni sehemu ya ufedhuli huo. The same can be said about AG, Jaji Kaijage, Jaji Mutungi, Mahera, Ndugu-gay, IGP, na DPP aliyepandishwa cheo na kuwa Jaji. Lakini kama DPP alipandishwa cheo, unafikiri Jaji Mkuu ana sababu ya kujali?
 
Sio solution,mkitulazimisha basi Jaji Biswalo kuwa jaji mkuu,sisi ni chama dume
 
Point nzuri sana umetoa. Lakini hata akikataa kujiuzulu, tumejua wazi kwamba hana lolote kichwani, alikuwa bendera fuata upepo wa kuamrishwa. Ni mwanasheria very weak ambaye ametia aibu tasnia ya sheria. Kama alishinikizwa alipaswa kujiuzulu kulinda hadhi yake na kada ya sheria

Watu wa namna yake ndio wa kwanza kupigwa risasi hadharani mapinduzi yanapotokea kuondoa tawala dhalimu.
 
1624876733945.png
UHURU WA KUJIELEZA HUU
 
Naunga mkono. Jaji Mkuu hawezi kutenganishwa na ubinyaji haki uliofanyika 2015-21. Ni sehemu ya ufedhuli huo. The same can be said about AG, Jaji Kaijage, Jaji Mutungi, Mahera, Ndugu-gay, IGP, na DPP aliyepandishwa cheo na kuwa Jaji. Lakini kama DPP alipandishwa cheo, unafikiri Jaji Mkuu ana sababu ya kujali?
Hawezi kubali, tuna mfumo mbovu ambao siyo wa kuwajibika
 
Mleta uzi umeniwahi, kama jaji Mkuu alikuwa anasimamia haki na haki haikutendeka anasubiri nini ofisini?
 
Naunga mkono. Jaji Mkuu hawezi kutenganishwa na ubinyaji haki uliofanyika 2015-21. Ni sehemu ya ufedhuli huo. The same can be said about AG, Jaji Kaijage, Jaji Mutungi, Mahera, Ndugu-gay, IGP, na DPP aliyepandishwa cheo na kuwa Jaji. Lakini kama DPP alipandishwa cheo, unafikiri Jaji Mkuu ana sababu ya kujali?
Sio yeye peke yake. Hata IGP na Boss wa usalama wa Taifa kwa haya yanayo endelea wana takiwa waachie ngazi tupate watu wapya wasio na mawaa...
 
Kwa kuwa mkuu wa muhimili wa mahakama Ni yule yule aliyekuwepo wakati watu wanaonewa na kubambikiwa kesi
Ulianza vizuri kwamba huyu jaji alikuwepo wakati watu wanaonewa na kubambikiwa kesi. Hivyo nakubaliana na wewe kwamba huyu ajiuzulu.

Lkn nakushangaa, unaposema haya maneno ya hapa chini:-

Muhimili huu ukiendelea kusikiliza serikali inataka nini na kutekeleza dhana ya separation of power haitakuwa na maana nchini.
Kwa hiyo hutaki haki inayo hubiriwa na awamu ya 6 iendelee kutendeka??? Why? Are you one of the Push Gang members?
 
Point nzuri sana umetoa. Lakini hata akikataa kujiuzulu, tumejua wazi kwamba hana lolote kichwani, alikuwa bendera fuata upepo wa kuamrishwa. Ni mwanasheria very weak ambaye ametia aibu tasnia ya sheria. Kama alishinikizwa alipaswa kujiuzulu kulinda hadhi yake na kada ya sheria

Watu wa namna yake ndio wa kwanza kupigwa risasi hadharani mapinduzi yanapotokea kuondoa tawala dhalimu.
Mnapenda kuangushia jumba bovu kwa wenzenu..mbona wew hutukukuona hata sku1 ukiandamana kwenda ikulu kudai hO haki...au kukuona hata ukitoa maoni kwenye video ya kulaan uonevu huo?kwan we si ni raia wa Tz...?
 
Back
Top Bottom