Napoleone
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 10,087
- 16,036
Mnapenda kuangushia jumba bovu kwa wenzenu..mbona wew hutukukuona hata sku1 ukiandamana kwenda ikulu kudai hO haki...au kukuona hata ukitoa maoni kwenye video ya kulaan uonevu huo?kwan we si ni raia wa Tz...?Kinachofanyika mahakamani kwa miezi mitatu mfululizo Ni ishara kwa muhimili wa mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake na kutekeleza maelekezo ya serikali.
Kwa kuwa mkuu wa muhimili wa mahakama Ni yule yule aliyekuwepo wakati watu wanaonewa na kubambikiwa kesi na kwa kipindi chote hicho alikaa kimya, naomba busara imwelekeze Jaji Mkuu kuachia ngazi na kuruhusu usukaji upya wa muhimili wa mahakama unaoweza kusimamia haki.
Muhimili huu ukiendelea kusikiliza serikali inataka nini na kutekeleza dhana ya separation of power haitakuwa na maana nchini.
Mzee nikuombe utafakari Kama uliyowafanyia wananchi wa Tanzania kwa miaka mitano yanakushuhudia kuendelea kukalia hicho kiti. Najua ulisukumwa kuminya haki na ukatekeleza kinyume na kiapo chako. Kukaa pembeni si dalili ya kushindwa Bali nikuiombea mahakama msamaha kwa wannchi na kupunguza lawama na dhambi ulizochuma ukiwa hapo juu.
Watanzania wanalia na kuumia kwa kupoteza wapendwa wao wakiwa jela au wengine kufariki kwa presha kwa kusikia wapendwa wao wapo ndani. Wengine Ni walemavu na baadhi familia zimesambaratika, jitafakari