Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,912
- 12,904
Salaam jamiiforum
Mungu ni mwema kila wakati naweza kusema hivyo.
Tarehe 13 mwezi wa kumi mwaka Jana 2024 nilipata ajali mbaya sana,tena mbaya mno.
Hakika sikujua kama nitapona haswa baada ya daktari mmoja kuniambia nimeumia ndani Kwa ndani na X ray inaonesha upande wa mbavu ya kulia haipo sawa.
Lakini niwapongeze madaktari wetu walifanya kazi kubwa mno,lakini ndugu ,jamaa na marafiki wameonesha upendo mkuu.
Lakini niwapongeze zaidi Dr Fred na Dr Zainab kwakufika nyumbani kwangu mara Kwa mara kuhakikisha nakuwa sawa mlinipa moyo,mkanifariji na kunitibu pia
Hatimaye Leo nimeenda kazini Kwa mara ya kwanza tangu niumie nilikuwa na hofu kiasi kulingana na maswaibu yangu,nikiwaza hatima yangu kwani sina muda mrefu ninge retire lakini kwanini iwe Kwa lazima kuliko umri
Nimekaa muda mrefu hospital,nimekaa muda nyumbani,kitu pekee nilikuwa nazuga nacho ni kuperuzi jamiiforum.
Heko kwa jamiiforum,ni moja ya mtandao bora kabisa na wenye watu makini,japo hata wenye mitazamo tofauti hawakosekani yote Kwa yote niwapongeze sana.
Lakini shukrani ni Kwa watu wa kijiji cha Jaribu mpakani,wilaya ya Kibiti.
Baada ya kunisaidia Kwa moyo wote
Pesa zangu kidogo,simu zangu zote niliziona,hongereni mwenyezi Mungu atawalipeni zaidi,pamoja na mabadiliko ya walimwengu lakini bado kuna binadamu wana mioyo safi.
Ujumbe.
Tuache dharau,
Tuheshimu kila mmoja hata kama ana kipato cha chini.
Atakaye kusaidia hatumjui
Usiku mwema