Namshukuru mungu sikusoma UDSM

Namshukuru mungu sikusoma UDSM

Ni post yake ya kwanza jamani...Msameheni bure, nadhani alikuwa anajaribisha kama anaweza kurusha ishu na ikajadiliwa na watu!
 
NN at least acknowlege that there are some great minds coming out of the Hill!

Pia kubali kuwa kuna ujenzi wa majengo mapya ya kisasa kule UDBS:

University of Dar es salaam Business School

Who are those great minds that are coming out of there? Name names sir!!

Unataka nikubali kuwa kuna vijengo vipya. Sawa nakubali. Lakini hivyo vijengo vipya ni asilimia ngapi ya campus? Vipi yale ya zamani? Mbona yametelekezwa? Hata ulinzi ni hafifu hadi ofisi za walimu zinawekewa magrill ya kuzuia wezi. Hii ni aibu!!! Au wewe unataka kuniambia hali ya chuo hicho ni nzuri tu na unaridhika nayo?
 
Poleni. Nadhani Nancy yuko sahihi kwani hajasema ni kwa nini amesema hivyo.kupoteza nguvu kujadili hilo ni kupiga risasi gizani.labda uwezo wake mdogo angedisco sasa kwa nini asishukuru mungu kusoma ambako hakuna disko
 
Halafu hii disco siielewi. Watu wana flunk kwa sababu masomo ni magumu au kwa sababu ni wazembe? Naisikia sikia sana hii disco na watu wanaiogopa kaa ukoma as if uki disco ndio mwisho wa dunia. WTF!!!!!
 
Who are those great minds that are coming out of there? Name names sir!!

Unataka nikubali kuwa kuna vijengo vipya. Sawa nakubali. Lakini hivyo vijengo vipya ni asilimia ngapi ya campus? Vipi yale ya zamani? Mbona yametelekezwa? Hata ulinzi ni hafifu hadi ofisi za walimu zinawekewa magrill ya kuzuia wezi. Hii ni aibu!!! Au wewe unataka kuniambia hali ya chuo hicho ni nzuri tu na unaridhika nayo?

Ni kweli hali ni mbaya. Ila kuna 'glimpses' za hali nzuri. Umepita kule nyuma ya Yombo? School of Law inakarabatiwa n.k.

Kuhusu baadhi ya great minds zinazoibukia angalia majina ya vijana katika tovuti ya Bunge - pia pita kwenye CSOs kadhaa.
 
Nimefurahi umekubali kuwa hali ni mbaya. Na ni kweli kuwa kuna ukarabati wa baadhi ya majengo unaoendelea lakini wamekiachia hicho chuo hadi kimechakaa kupita kiasi. Majengo karibu yote yale ya zamani yako katika hali mbaya. Si Nkrumah hall si lile jengo la Sociology (nakumbuka hili wakati niko dogo tulikuwaga tunaenda tunapanda lift (elevator) hadi kule juu mwishoni halafu tunauangalia mji). Mabweni yale wa wanafunzi ndiyo usiseme kabisa. Ni machafu, ni machakavu, na ingekuwa kwenye nchi za watu yangekuwa yameshakuwa condemned siku nyingi sana.

Kuhusu hao great minds....mpaka sasa sijaona yeyote aliyeni impress.....
 
Zitto Kabwe

Mnyika

Kitila Mkumbo (but maybe not, he is an old-timer)

😀

Zitto Kabwe? You can't be serious....:teeth:

Au mara hii ushasahau ile youtube clip ya mahojiano aliyofanya na Daily News? Lol....
 
Zitto Kabwe? You can't be serious....:teeth:

Au mara hii ushasahau ile youtube clip ya mahojiano aliyofanya na Daily News? Lol....

hahha .....ulilala kati kati vile eee? Duh hatari.

Labda Compareno atakuja kututajia wengine manake katika wanasiasa wanaosifika kwa kiasi ndo hao :s
 
Ndugu, UDSM pamechoka kiujumla! Yaani kuanzia mazingira, majengo, vifaa na nyenzo za kufundishia hadi ubora wa elimu itolewayo hapo. Majengo hawayafanyii ukarabati. Vyumba vya madarasa, ofisi za walimu, mabweni ya wanafunzi, na majengo mengine ya chuo hicho yamechakaa vibaya sana. Kwa hadhi yake chuo hicho kilitakiwa kiwe na mazingira mazuri kwa ujumla. Sasa kama mazingira ni mabovu hivyo kweli unategemea hata elimu itolewayo hapo itakuwa bora kweli?
Inaelekea ulipita zamani, tena kwa lengo la kumsalimia ndugu yako pale.
 
kwa kuangalia haraka haraka tuu, kama watu wengi wa humu ndiyo wamesoma udsm, kweli kazi ipo huko nyumbani.
tatizo lako unaangalia haraka haraka
unaandika haraka haraka
na kufikiria kivivu.
Endelea kusoma vyuo vyako vyenye digrii mchakachuo na kamwe husithubutu kujilinganisha na wana Mlimani
 
Nancy tetea hoja yako ni kwa nini unashukuru kutokusoma UDSM. Umesoma chuo gani?? suku hizi kuna misururu ya vyuo vya kata mambo lainiiii hakuna ku disco huko, ni hela yako tu and this is business bana.
 
si lile jengo la Sociology (nakumbuka hili wakati niko dogo tulikuwaga tunaenda tunapanda lift (elevator) hadi kule juu mwishoni halafu tunauangalia mji)

du, dogo ulikuwa masalo - lazima ulikuwa unatoroka sana kule vidudu!
 
du, dogo ulikuwa masalo - lazima ulikuwa unatoroka sana kule vidudu!

Wewe huwezi kuniita mimi dogo wakati nimekuzidi madarasa mawili. Wewe si umemaliza Mlimani primary sijui 91 au 92.....kakako mimi wewe....ooohooooo
 
Back
Top Bottom