Namtamani nikiwa na hamu naye lakini baada ya hapo namchukia

Sawa mkuu nitampiga chini..!!
 
Mwambie tu yeye unamuelewa kwa ajili ya kukukaza tu sio zaidi ya hapo.

Aendelee na mishe zake,ila muhakikishie hutakzwa na mwingine zaidi yake. So ukiwa na hamu unamcheki kwa kazi maalum. Sema sasa umlishe ili aje akiwa fiti. Maana ake mtupie maokoto maana hiyo inakuwa kama kazi rasmi.
 
Nimpe maokoto tena?? 😹😹
 
Usikute hivyo unavyohisi ndivyo anavyohisi jamaa yako pia...

Na kama sivyo basi inawezekana hamna muda mrefu sana kwenye hilo penzi lenu, na labda hilo penzi lilianza kwa namna ambayo wewe hukuitarajia kwa maana ya kwamba si mtu ambae mlianza kuonana mara kwa mara kabla ya kwenda kwenye hatua hiyo mliyopo.

Na kama hivyo ndivyo ilivyo, basi hiyo ni kawaida ya mapenzi.

Kwa maana kiuzoefu wangu huwa naona mapenzi yako na stage kuu tatu, ya kwanza yule aliyetongoza huwa anakua na upendo wa hali ya juu kuliko aliye tongozwa(hapa aliyetongoza huwa anakua mtumwa wa mapenzi).

Na akiona anatumia nguvu kubwa ila hapati ule mrejesho ambao yeye aliutarajia basi anaanza kukata tamaa na upendo unaanza kushuka taratibu.

Kwakua yule aliyependwa alikua anafurahia namna anavyopendwa hali hii huwa inamshtua na kuanza kuona kama hapendwi tena na ghafla ataanza kua emotional na kujikuta yeye sasa anakua mtumwa wa mapenzi(hapa mzani unabadisha ulalo)

Na hatua ya tatu huwa ni eidha jamaa aamue kurudi tena juu ili mkutane huko kuufanya mzani ubalance au abaki pale pale hadi na wewe utakapoamua kushuka chini ili mzani ubalancie hapo(na hapa sasa ndio mnaanza kuishi kwa mazoea huku mkisongesha life)

Kwahiyo inawezekana wewe na jamaa yako mko kwenye stage hiyo ya kwanza, ila mtaingia ya pili na ya tatu(ya pili inaweza kukutesa wewe kama hautaamua kufanya maamuzi sahihi hivi sasa).

Na kama hivyo sivyo basi inabidi utuambie kama hiyo hali ni kwa huyo jamaa tu au ilikua inakutokea hata kwa waliopita?
 
Nkamu jamani
Uje tufanye maombi hako karoho ka chuki kwa shemeji kakutoke.

Heaven Sent kuna maombi huku yanahitajika Mama.
 
Nkamu jamani
Uje tufanye maombi hako karoho ka chuki kwa shemeji kakutoke.

Heaven Sent kuna maombi huku yanahitajika Mama.
Nimetoka kukuita ss hivi nikupe pole kwa kipigo kingine kutoka kwa Newcastle kumbe umefika hapa..!! 😹

Nkamu maombi yenu yanahitajika mno na mama mchungaji Heaven Sent 🥰
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…