Tajiri wa kusini
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,079
- 2,947
Namuachaje kwa amani, nilimtoa kwenye ndoa yake ili anizalie sasa mke wangu naye kapata mtoto sitaki tena kuchepuka!
Niko kwenye ndoa huu ni mwaka wa 7. Katika kipindi chote hicho mimi na mke wangu tulikuwa hatujabarikiwa kupata mtoto. Tulikwenda hospitalini kupima, ikagundulika yeye ndiye mwenye matatizo, ana hormonal imbalance.
Kabla kuoa kuna mwanamke mwingine nilikuwa naye lakini tulikuja kuachana tu sababu ya umbali, hivyo yeye akaja kuolewa na mimi nikaoa. Yeye tayari alikuwa na mtoto mmoja na mume wake, kuna siku tulikutana mtaani kwa bahati na tukabadilishana namba.
Tukaanza kuchat na akaniambia changamoto za ndoa yake. Kuna wakati alikuwa anaomba pesa namsaidia, basi tukajikuta tumerudiana. Ndipo hapo nikaanza kumuelezea changamoto za ndoa yangu kuwa nimechelewa kupata mtoto na mke wangu ndiye mwenye tatizo. Alikuwa ananiambia mambo ya mume wake na kikubwa ni kipato, mume anafanya kazi lakini ana majukumu mengi ya ndugu, hivyo hawafikii malengo.
Nilimwambia anizalie ili iwe rahisi kumwacha mke wangu. Kweli nilishafikiria kumuacha mke wangu na kwa kuwa alikuwa na mtoto mmoja tu, nilijua hata akimuacha mume wake basi nitaweza kumlea huyo mtoto wake. Kweli alikubali, akabeba mimba yangu akafanya vituko mpaka mume wake akajua!
Nilimshawishi aachane na mume wake na kweli alidai talaka nilimsaidia mpaka wakili. Mimi nikamchukua na kumpangishia sehemu nyingine! Nilihudumia ujauzito lakini mimba ilipofikisha miezi 6 mke wangu naye alipata ujauzito, kweli ilikuwa kama muujiza hata sikutaka kuamini, ila sikumwambia huyo X wangu kua mke wangu ana mimba.
Mke wangu kajifungua mtoto ana miezi miwili sasa, ni kopi yangu kabisa. Nina furaha sana, hivyo siwezi tena kumwacha mke wangu. Kule kwingine bado naenda lakini sasa hivi siwezi kumuoa tena yule mwanamke. Kwanza ana mtoto na mwanaume mwingine, kitu ambacho siwezi kufurahia, lakini pia kama aliweza kumuacha mume wake kwa ajili yangu, vipi siku na mimi sina kipato?
Ninachotaka kujua ni namna gani nitaongea naye ili asije kuniharibia kwa mke wangu. Kwa ninavyomjua muda wote huo amekaa kimya, hajamtafuta mke wangu kwa kuwa anajua kuwa nitamuoa. Hajui hata kama nimeshapata mtoto na mke wangu kwani yuko mkoa tofauti, nisaidie niongee vipi na huyu mtu akubali tu nitalea mtoto ila siwezi kuendelea kumsaliti tena mke wangu!