beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Namungo FC imezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Luanda nchini Angola baada ya mamlaka kudai wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana virusi vya Corona.
Mpaka wakati wa kuandika taarifa hii timu ipo uwanja wa ndege huku utata ukitawala kutokana na mamlaka za nchi hiyo kutaka msafara mzima ama urudi Tanzania au uende karantini.
Namungo ipo Angola kuchuana na Clube Desportivo 1º de Agosto katika mechi ya kombe la shirikisho.
Taarifa zaidi zitafuata.
===========
NAMUNGO YAZUILIWA UWANJA WA NDEGE
Kikosi cha wachezaji wa Namungo fc wamezuiliwa uwanja wa ndege wa Luanda nchini Angola baada ya maafisa nchini humo kudai kuwa wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana virus vya Corona.
Maafisa hao wamesema kuwa Namungo watatakiwa kufanya moja kati ya kurudi Tanzania au waende Quarantine.
Klabu hiyo yenye maskani yake huko Lindi iliondoka kuelekea Angola kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Primeiro De Agosto mchezo ambao utachezwa tarehe 14 Februari.
Namungo chini ya kocha wake Hemed Morocco inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 21 na kucheza michezo 16.
De Agosto iliingia kwenye kombe la shirikisho baada ya kushuka kutoka michuano ya klabu bingwa barani Afrika, baada ya kufungwa na Kaiser chiefs ya Afrika kusini.
Ni moja kati ya michezo miwili ya hatua ya mtoano ambapo mshindi wa matokeo ya ujumla kwamaana ya Nyumbani na Ugenini atafuzu hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.