Namuokoaje rafiki yangu ambaye ni Mwalimu Kijijini, michezo ya wabaya usiku inamnyima raha

Namuokoaje rafiki yangu ambaye ni Mwalimu Kijijini, michezo ya wabaya usiku inamnyima raha

Hii nilishawahi kusikia kule Ukerewe na maeneo jirani yake.
 
Rafiki yangu ni mwalimu katika kijiji fulani huko ndani ndani sana mkoa X.

Sasa hicho kijiji kumekuwa na uchawi sana mpaka kero.

Rafiki yangu pamoja na walimu wenzake baadhi hupatwa ma vituko usiku kitu ambacho huleta msongo wa mawazo.

Vibweka hivi ni kama.

1. Sufuria zenye vyakula kukutwa tupu asubuhi ilhali jana zilikuwa na chakula.

2. Kuhisi mtu ama watu kutembea ndani ya nyumba

3. Vishindo mithiri ya watu kukimbizana kwenye dari

4. Mchanga kumwaga kwenye bati

5. Mawe kurushwa kwenye bati.

6. Baadhi ya walimu kuamka miguu ikiwa na vumbi na kadhalika

Sasa anaomba ushauri anawezaje kupata uhamisho
Amkabidhi Mungu maisha yake awe anasali kweli kwa kumaanisha, ukiona wanakuchezea ujue uko empty yaani hauna ulinzi wa Mungu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hio number moja awaulize wenzake vizuri,kuna mtu anaamka usiku na kupitia ubwabwa..ndio huyo huyo wanamsikia akitembea ndani ya nyumba...waweke mtego watamkamata tuu...[emoji1787][emoji1787]
Kwenye ishu ya msosi, aweke sumu tu ili aone je, kesho yake kuna mtu ataenda kwa sir God? Hapo ndo ataheshimika.

Kuhusu hayo ya uchawi, nadhani asali tu. Au kama vp achukue mafuta ya upako aone hao vibwenga kama watakuja tena kwake.

Hivi kila mwlm akitaka kuhama, nani atafundisha shule, za vijijini?
 
Back
Top Bottom