Ndugu zangu Watanzania,
Natambua wazi Namna Rais wetu alivyo na Upendo Mkubwa kwa Vijana wa Taifa hili . Natambua Juhudi kubwa sana zinazofanywa na Rais wetu Mpendwa katika Kuhakikisha kuwa analiweka Taifa hili Mikononi Kwa Vijana ambao ni wengi sana Nchini kitakwimu.
Najua Rais wetu anatambua wazi kabisa kuwa Taifa hili ili liendelee kudumu katika Umri Mrefu katika hali ya Mafanikio na Ustawi ni lazma Vijana waandaliwe kushika nafasi za uongozi kwa kuwapa nafasi za kiutendaji na kuendelea kuwalea kwa ukaribu zaidi .
Ni katika upendo huo Alionao Rais wetu kwa Vijana ndio sababu tumeshuhudia akitupatia Makamu wa Rais kijana kabisa na anayejua Mahitaji ya vijana ,Tumeona akitupatia Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye bado Damu inachemka na anaelewa pia kiu ya Vijana . Tumeshuhudia pia Rais Wetu akiteua vijana wengi sanaaa ndani ya Baraza la Mawaziri ,Wakuu wa mikoa ,Wilaya ,Wakurugenzi ,Ma DAS na hata Ma RAS.
Tumeshuhudia hadi ndani ya chama katika ngazi za kiutendaji Rais wetu ambaye ni mwenyekiti wake akiwa amini vijana Kushika nafasi za kiuongozi na uongozi . Tunajua kama vijana kwamba tumekuwa Wakati Mwingine Tunamkosea na kumkatisha Tamaa Rais wetu na pengine Kumvunja Moyo lakini Bado Rais wetu Mpendwa na Mama yetu Kipenzi hajatukatia Tamaa wala kututupa.
Bali ameendelea kutupatia nafasi na kuendelea kutulea na kuwalea vijana mbalimbali. Amekuwa ni zaidi ya Rais kwa vijana , amekuwa ni kama Mama Mlezi ama Mama Mzazi kwa Mwanaye ambaye husamehe muda wote .
Vijana wote Nchini tumeona namna Rais wetu alivyowapandisha na kuwaheshimisha vijana kwa kuwapa nafasi ya kulitumikia Taifa letu katika nafasi mbalimbali. Sote tumeona akiwafungulia Dunia Vijana na kuwapa nafasi ya kuonyesha na kutumia vipawa vyao . Lakini najua ni katika hali ya kibinadamu wengine wamekuwa wakiteleza na kwenda kinyume na maelekezo ama kuharibu ama kukosea ama kuyumba kibinadamu kunakotokana wakati mwingine na ujana ama ugeni wa kazi ama kuwa na dhamira njema katika njia isiyo sahihi kiitifaki na kiutendaji ama kiutaratibu.
Ni katika minajili hiyo ama muktadha huo ama mazingira hayo ya kibinadamu na kukosea Mheshimiwa Beno Malisa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na Baadaye Tabora amejikuta akifanya kosa na kumkosea Rais wetu Mpendwa na hata chama chetu .
Kwa kuwa Mtu huyu na kijana huyu amekiri kwa uchungu na hisia kali na kuomba msamaha hadharani kwa Mheshimiwa Rais na chama chetu cha Mapinduzi. Nilikuwa namuomba Mama yetu Mpendwa na Rais wetu kipenzi Amsamehe Kaka yetu , amsamehe kijana mwenzetu , Amsamehe Mwanaye Benno Malisa na kumfikiria tena.
Mama Msamehe,Mfungulie njia , Mpe nafasi ya pili , Mpe nafasi ya kujifunza na kujirekebisha tena . Amekosea , Amekosa na amekiri Hadharani kukukosea wewe binafsi na chama chetu . Huyu ni Muungwana na amefanya jambo la kiungwana kwa kujutia Makosa na kosa lake na kukuomba msamaha Mama na Rais wetu.
Ameomba Nafasi ya pili ya kulitumikia Taifa letu , Ameomba kwa unyenyekevu kusamehewa . Mama yetu mfikirie Mwanao huyu ambaye kwa Majuto Makali amekiri kwa ulimi wake na kukuomba Radhi . Amefanya kitendo cha kiungwana na kibinadamu.
Msamehe Mama yangu .Mpe nafasi ya Kumlea Tena . Watanzania tunajua Moyo wake Mama yangu kuwa wewe ni Mwenye Upendo ,huruma na Mwenye Kusamehe wakati na siku zote . Ndio Maana Mama yangu hata waliokuwa pengine wakikudharau wakati ukiwa Makamu wa Rais bado uliwasamehe na kufungua ukurasa mpya wa Amani na upendo.
Kuna watu hata kabla hujawa Rais walitamani usiwe Rais na usiapishwe kuwa Rais na uliwajua kabisa lakini bado uliwasamehe Mama yangu na kusema tujenge Nchi na Taifa letu . Kuna watu wamekutukana sana Matusi kwa mihemko tu lakini Mama yetu na Rais wetu Mpendwa bado umeendelea kuwasamehe.
Huu Ni Ushauri tu Mama yangu na Samahani sana kama nitakuwa nimekukosea Adabu ama Kukukwaza kwa namna yoyote ile. Ni Andiko lenye nia njema na lenye kutamani kuona vijana wenzetu wakiendelea kupata nafasi ya kutuwakilisha vijana wenzao . Hata kama mimi siyo Kiongozi lakini nafurahi sana napoona kijana mwenzangu kapata nafsi ya kulitumikia Taifa letu kwa kuamini kuwa atainua Morali ya vijana wengine na kuwatumikia vyema vijana wenzake na wa makundi mengine kwa kuelewa Mahitaji yao lakini pia kwenda na kasi ya vijana .
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania Wanyonge wasio na Sauti.
Soma Pia: Beno Malisa amuomba Rais Samia msamaha
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.