Namuombea msamaha hayati Magufuli kwa makosa aliyoyatenda

Namuombea msamaha hayati Magufuli kwa makosa aliyoyatenda

BrownRange

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2020
Posts
927
Reaction score
1,191
Habari ndugu zangu Watanzania.

Nimekuwa nikifatilia mijadala ya kumsema hayati Magufuli ikiwa inataradadi hapa jukwaani. Nipende tu kusema hakuna mwanadamu aliyemkamilifu. Kila mwanadamu ana mazuri na mabaya yake. Wote sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu, na hatujakamilika.

Ukitaka kuangalia kwa undani utaona mazuri ni mengi kuliko mabaya kwa hayati Magufuli.

Namuombea msamaha kwa hayo mabaya machache aliyoyatenda maana yeye ni mwanadamu hajakamilika, na tufurahie kwa mazuri mengi aliyoyatenda. Tumuache hayati apumzike

Namuombea msamaha kwa haya machache
  • Kupunguza mishahara kwa baadhi ya taasisi.
  • Kutokuwa na kauli nzuri kwa watendaji wa hovyo
  • Kushirikisha wasaidizi wako kabla ya kutenda kwa kila jambo

Ushauri kwa Mh. Rais wa Sasa
  • Sahihisha makosa ya mtangulizi wako kwa kuwarejeshea mishahara taasisi zote watumishi wake waliopunguziwa mishahara
  • Jitahidi kutoa kauli nzuri, za staha
  • Shirikisha wasaidizi wako hatua kwa hatua

Naomba kuwasilisha
 
... kama msamaha anatakiwa aombewe na his equivalent na sio vinginevyo.
 
Ni jambo zuri sana.

lakini inabidi uyataje hayo makosa, na waliokosewa.

Tanzania inahitaji TUME YA UCHUNGUZI itakayowezesha wote walioumizwa, kujulikana, kusuluhishwa, na kuombwa msamaha.
 
Unarahisisha mambo ili yaonekane kuwa ni makosa madogo ya kiutawala.

Waliouliwa je?

Waliotekwa je?

Waliobomolewa nyumba bila fidia(wale wa Mwanza hawamo)?

Waliobaguliwa kwa rangi, ukabila na eneo je?

Yapo mengi, huwa hayaishi hivi hivi.

Hata South Africa , wazungu ingalau walikubali kuwa kwa vizazi vingi vya kwao walikosa kuendesha siasa ya Apartheid.
Tuishauri CCM ikubali makosa ili itengeneze imani mpya ya wanachama na nchi kwa ujumla.
 
..Ni jambo zuri sana.

..lakini inabidi uyataje hayo makosa, na waliokosewa.

..Tanzania inahitaji TUME YA UCHUNGUZI itakayowezesha wote walioumizwa kujulikana kusuluhishwa na kuombwa msamaha.
Taasisi watumishi wake waliopunguziwa mishahara inajulikana
Waliotolewa kauli mbaya inajulikana

Tumsamehe hayati kwa makosa machache madogo, na tufurahie mazuri yake mengi. Mh. Rais arekebishe kasoro hizo ndogo. Mi naona mengi mazuri kwake
 
Habari ndugu zangu Watanzania.

Nimekuwa nikifatilia mijadala ya kumsema hayati Magufuli ikiwa inataradadi hapa jukwaani. Nipende tu kusema hakuna mwanadamu aliyemkamilifu. Kila mwanadamu ana mazuri na mabaya yake. Wote sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu, na hatujakamilika.

Ukitaka kuangalia kwa undani utaona mazuri ni mengi kuliko mabaya kwa hayati Magufuli.

Namuombea msamaha kwa hayo mabaya machache aliyoyatenda maana yeye ni mwanadamu hajakamilika, na tufurahie kwa mazuri mengi aliyoyatenda. Tumuache hayati apumzike

Namuombea msamaha kwa haya machache
-Kupunguza mishahara kwa baadhi ya taasisi.
-Kutokuwa na kauli nzuri kwa watendaji wa hovyo
-Kushirikisha wasaidizi wako kabla ya kutenda kwa kila jambo

Ushauri kwa Mh. Rais wa Sasa
  • Sahihisha makosa ya mtangulizi wako kwa kuwarejeshea mishahara taasisi zote watumishi wake waliopunguziwa mishahara
  • Jitahidi kutoa kauli nzuri, za staha
  • Shirikisha wasaidizi wako hatua kwa hatua

Naomba kuwasilisha
Ngumu sana kusamehewa,sawa sisi tunaweza kumsamehe ila Mungu awezi kumsamehe,apambane na hali yake

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Vipi na tuliopoteza wapendwa wetu ambao mpaka leo hatujui walipo? Lissu tunamwachia mwenyewe maana bado yupo hai akiamua kumsamehe au akidai fidia atajua mwenyewe
 
Taasisi watumishi wake waliopunguziwa mishahara inajulikana
Waliotolewa kauli mbaya inajulikana

Tumsamehe hayati kwa makosa machache madogo, na tufurahie mazuri yake mengi. Mh. Rais arekebishe kasoro hizo ndogo. Mi naona mengi mazuri kwake

..Kila kitu kiwekwe WAZI.

..Kuna wengi walioumizwa zaidi ya watumishi wa umma.

..Ilifika mahali wafuasi wake walikuwa wanashangilia na kusifia ukatili wa serikali ya awamu ya 5.

..Ni lazima kama Taifa tulaani utamaduni huo mpya aliotuletea Magufuli.
 
Watanzania wote tunajua wanaompondea ni waovu aliowabana kwenye utawala wake, hakuna haja ya kuwaomba msamaha kwa makosa ambayo Magufuli hakuyatenda.
 
Wengi naona mnadhani mtu anapokosolewa kwenye uongozi basi anachukiwa au ni kukosa adabu. Hakuna kiongozi asiyekosolewa duniani. Ni Afrika tu ndiyo na hasa Tanzania ndiyo mnadhani kusema mabaya ya kiongozi ni vibaya na haitakiwi.

Hakuna mtu mwenye chuki na Magufuli, na tena wengi wa watu wanamkosoa walikuwa wanampenda kwa dhati. Ukishkuwa kiongozi ni lazima utasifiwa na kukosolewa ukiwa hai au ukishafariki.

Hii inasaidia sana ili nchi iweze kurekebisha makosa ya viongozi waliopita. Sasa nyie timu sifia sifia mnadhani Samia akielezea hali halisi ilivyokuwa wakati akiwa makamu wa rais hampendi Magufuli?
 
Habari ndugu zangu Watanzania.

Nimekuwa nikifatilia mijadala ya kumsema hayati Magufuli ikiwa inataradadi hapa jukwaani. Nipende tu kusema hakuna mwanadamu aliyemkamilifu. Kila mwanadamu ana mazuri na mabaya yake. Wote sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu...
Mi hata sijui alinikosea nini. Basi tu sikumpenda yule mwendazake. Apumzike alipojiandalia makazi
 
Taasisi watumishi wake waliopunguziwa mishahara inajulikana
Waliotolewa kauli mbaya inajulikana

Tumsamehe hayati kwa makosa machache madogo, na tufurahie mazuri yake mengi. Mh. Rais arekebishe kasoro hizo ndogo. Mi naona mengi mazuri kwake
Hivi mtu ambaye mwanae aliuawa kwa amri ya Magufuli ataona hiyo ni kasoro ndogo? Infact mtu yeyote mwenye akili na utu lazima alaani watu waliouawa bila makosa na wengine wakagezwa vilema. Yuko wapi Ben Saanane? Kwa nini walimuua? Kuhoji elimu ya mtu ndiyo kosa la kuuawa?
 
Habari ndugu zangu Watanzania.

Nimekuwa nikifatilia mijadala ya kumsema hayati Magufuli ikiwa inataradadi hapa jukwaani. Nipende tu kusema hakuna mwanadamu aliyemkamilifu...
Nani atalipia uhai wa Ben Saanane, Godfrey Luena, Mawazo, Azori, Daniel John n.k

Nani atamwomba msamaha Tundu Lisu?

Nani atamrudisha Samson Kanguye?

Magufuli alitakiwa atengeneze mambo ya nyumba yake. Hakufanya hivyo. Wacha wampopoe hata akiwa mfu
 
Back
Top Bottom