Namuombea msamaha hayati Magufuli kwa makosa aliyoyatenda

Namuombea msamaha hayati Magufuli kwa makosa aliyoyatenda

Watanzania wote tunajua wanaompondea ni waovu aliowabana kwenye utawala wake, hakuna haja ya kuwaomba msamaha kwa makosa ambayo Magufuli hakuyatenda.
Magufuri hakuwa Mungu, alipatia na kukosea mengi tu. Angekuwa kiongozi mzuri ila alitaka tumuone yeye ndio pekee anaweza kazi kuliko mwingine. Kama wewe ulimuona Malaika sawa
 
Magufuri hakuwa Mungu, alipatia na kukosea mengi tu. Angekuwa kiongozi mzuri ila alitaka tumuone yeye ndio pekee anaweza kazi kuliko mwingine. Kama wewe ulimuona Malaika sawa
ingekuwa hivyo asingekuwa na wasaidizi.ujue shida yenu mnafanya propaganda kwa kuropoka.
 
Naunga mkono hoja, JPM was a human being just like human being mwingine yeyote, anaweza kuwa na mapungufu, no one is perfect, aachwe apumzike kwa amani
P

Kwani kuna aliyeenda kumfukua kaburini, hapa watu wanaweka rekodi sawa ili asitokee kiongozi mwingine akafanya kama yeye. Hayo mapungufu yake hakutaka yasemwe akiwa hai, acha watu wayaseme sasa na siku yoyote watakayo.
 
Kheee c tulikua tunaambiwa ni nabii mara Yesu, MUNGU, Musa . That's why haya yote yanakuja. Kwanza ku entertain hayo majina bila kukemea ni pigo kubwa san kwake. Refer kifo cha Herode!!!
Naunga mkono hoja, JPM was a human being just like human being mwingine yeyote, anaweza kuwa na mapungufu, no one is perfect, aachwe apumzike kwa amani
P
 
Habari ndugu zangu Watanzania.

Nimekuwa nikifatilia mijadala ya kumsema hayati Magufuli ikiwa inataradadi hapa jukwaani. Nipende tu kusema hakuna mwanadamu aliyemkamilifu. Kila mwanadamu ana mazuri na mabaya yake. Wote sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu...
Tatizo ni moja tuu hapa... Ukiangalia sifa alizokua anapewa na majina ya ukuu wa mbinguni halaf hakua anakemea. Means alifurahia, so hilo lilikua kosa kubwa san kutaka kusifiwa na kuipenda nafas ya MUNGU na mitume wake!

Soma kisa cha Herode kweny maandiko utaelewa hii mambo. Pia sasa kila kitu kinawekwa waz ndipo yanajulikana manyang'unyang'u yote, ndo point za kusema zinapoanzia!!
 
ingekuwa hivyo asingekuwa na wasaidizi.ujue shida yenu mnafanya propaganda kwa kuropoka.
Tuliza hasira na mihemko ili ujenge hoja nzuri na watu wakuelewe. Hoja ya kutetea wanyonge was totally " propaganda '' ilikuwa njia ya kupata public sympathy kwa mambo mepesi tu.

Suala la kujengwa miundombinu lilianza tangu enzi za wakoloni ambao walituachia reli na bandari ya dar es salaam. Ila mzee jpm alikuwa amatimiza wajibu wake na filimbi nyingi sana as if alikuwa anatumia pesa kutoka mfukoni kwake.

Kwa sasa anavuna alichopanda mwenyewe maana ilikuwa tabia yake kukandia watangulizi wake as if hawakufanya chochote.

Chuki za waziwazi na upendeleo kwa baadhi ya viongozi ambao walifanya makosa na kulindwa bila kutumbuliwa. Rejea issue ya makontena ya makonda bandarini. Kuna mambo mengine ni confidential mzee wetu alikosea.
 
Tuliza hasira na mihemko ili ujenge hoja nzuri na watu wakuelewe. Hoja ya kutetea wanyonge was totally " propaganda '' ilikuwa njia ya kupata public sympathy kwa mambo mepesi tu..
hamna mwenye hasira hapa ni kichwa chako kigumu kinafanya nitumie lugha yenye amri ili kukuongezea umakini.
unasema hakuwa mtetezi wa wanyonge,unajua bei ya mafuta na vifaa vya ujenzi imefika wapi saa hii ??achana na ya kupikia hii imekuwa anasa kuwa nayo.

kutumia pesa za serikali ni jambo moja,na kuzisimamia zionekane zikifanya jambo ndio sifa ya jpm pekee,labda hukuwa umezaliwa nenda kafatilie akiwa waziri wa ujenzi alifanya nini wajinga wajinga,nenda kafatilie akiwa waziri wa uchukuzi hali ilikiwaje!

Msikae mbele za watu na makelele tupu,tafitini mambo.makonda alitumbuliwa wakati ambao labda weww hukupenda.ila kapoteza kazi bado jpm akiwa rais.

jpm havuni alichopanda,ameshakufa tayari kazi mnayo nyinyi kupigia kelee mtu asiyekuwepo,watanzania wanawachora jinsi mlivyo hamnazo.
 
Kwani kuna aliyeenda kumfukua kaburini, hapa watu wanaweka rekodi sawa ili asitokee kiongozi mwingine akafanya kama yeye. Hayo mapungufu yake hakutaka yasemwe akiwa hai, acha watu wayaseme sasa na siku yoyote watakayo.
tunathibitishaje kama ni ya kwake wakati wanaotakiwa kujibu wapo,hawajibu na ndio wako kwenye usukani!!!!
watanzania sio wajinga.
yaani na meno 32 unaamini makamu wake na PM hawana cha kujibu hapa!!!
 
Mimini nani nimpinge mheshimiwa rais anayeanika mabaya yake..
 
Naunga mkono hoja, JPM was a human being just like human being mwingine yeyote, anaweza kuwa na mapungufu yake ya kibinaadamu kama binadamu mwingine yeyote, no one is perfect, aachwe apumzike kwa amani
P
Miaka 23 hatujamwacha Mwalimu Nyerere akapumzika. Mwl si alikuwa mwanadamu! kwanini hatudhani kwamba hakuwa perfect. Makapa hatujamwacha akapumzika n.k.

Viongozi ni public figures kuna privileges' lakini pia responsibilities

Kinachoongelewa si mwanadamu bali kiongozi na mtawala.
Rekodi yake inajadiliwa na kupitia rekodi za viongozi tunajifunza kama Taifa

Nyerere aliposema Katiba inamruhusu kuwa Dikteta nani alimwelewa?
Leo nani asiyemwelewa? Na watu wamejifunza wapi na lini?

JokaKuu ni makosa gani asamehewe na aliwakosea akina nani?
 
Naunga mkono hoja, JPM was a human being just like human being mwingine yeyote, anaweza kuwa na mapungufu yake ya kibinaadamu kama binadamu mwingine yeyote, no one is perfect, aachwe apumzike kwa amani
P
Mr. Mayalla I'd rather think otherwise but let me put it clear...
JPM is long dead,he cannot apologise,he cannot respond nor can he defend himself against all these allegations.

My question is,why do politicians and some few people use a lot of resources and time to abuse somebody who is already a spirit...?

Ikiwa JPM alikuwa mbaya kiasi hicho kwanini watu walikuwa wanahangaika kuuzungusha mwili wake huku wakimsifia......?

Hivi hawa wanasiasa wanakumbuka kuna familia ziliangamia kipindi cha kuagwa mwili wa JPM kwa uzembe wao?

Uzuri almost 80% ya watanzania wanajua magufuli alikuwa ni rais mwenye nia njema.

Watamtetea kwenye nafsi zao....magufuli ataandikwa kwenye vitabu na watoto wetu watamsoma.
 
Habari ndugu zangu Watanzania.

Nimekuwa nikifatilia mijadala ya kumsema hayati Magufuli ikiwa inataradadi hapa jukwaani. Nipende tu kusema hakuna mwanadamu aliyemkamilifu...

Kama unamuombea msamaha basi wote walioumizwa nao utawasaidia vp
 
Wote sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu, na hatujakamilika

Usilitaje bure jina la Mungu wako katika kazi za kibinadamu (siasa) hapa duniani.

Siasa ni kushawishi watu na shughuli hii ya siasa ni watu.

Tuendelee na kujadili watu hawa wanasiasa.
 
Mr. Mayalla I'd rather think otherwise but let me put it clear...
JPM is long dead,he cannot apologise,he cannot respond nor can he defend himself against all these allegations.
Huyu alikuwa kiongozi kama walivyo viongozi wote duniani. Mbona watu wanamsoma Hitler, Churchill , Mahtma , Lincoln, mapapa wa Vatican n.k.
Kwanini iwe tofauti na Nyerere ambaye 23 bado anasemwa left-right !
My question is,why do politicians and some few people use a lot of resources and time to abuse somebody who is already a spirit...?
Ipi ni abuse? Kumbuka alikuwa public figure, kuna msemo '' with great power comes great responsibilities ''
Uzuri almost 80% ya watanzania wanajua magufuli alikuwa ni rais mwenye nia njema.

Watamtetea kwenye nafsi zao....magufuli ataandikwa kwenye vitabu na watoto wetu watamsoma.
Nukuu ya kwanza '' unakataza watu wasimseme marehemu kwasababu ameshafiriki , hawez kujitetea au kuomba msamaha. Nukuu yako ya mwisho unajipa uwezo wa kumsifia kwa 80% ya Watanzania kujua nia yake njema na kumtetea katika nafsi zao''

Mosi, unapata wapi mtima wa kukataza wengine wasimjadili lakini ukajipa uhuru wa kumjadili?

Pili, 80% ni kwa mujibu wa takwimu gani?
Mwingine akisema kinyume chake atakuwa amekosea wapi?
 
Back
Top Bottom