Rajabmbisha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2024
- 316
- 530
Amani iwe nanyi Wana JF, ipo hivi: nipo kwenye mahusiano na binti mmoja hapa mtaani kwetu. Tumekuwa tukidate kwa wiki mbili sasa. Mwanzoni alionekana mgumu sana kunielewa, lakini baada ya kukaza juhudi, hatimaye alinikubali.
Katika jitihada za kumshawishi, nilimuahidi kumuoa, na hapo ndipo nilipojichanganya, maana aliamini nitamuoa kweli. Lengo langu halikuwa hilo; nilikusudia kupita tu, na tayari nimeshafanikisha hilo. Hata usiku wa leo amelala kwangu.
Tatizo ni kwamba binti huyu amenipenda kupita kiasi, lakini mimi sina mpango naye. Ni binti mdogo mwenye umri wa miaka 19 tu. Sasa sijui nianzie wapi kumweleza kwamba sina malengo naye, bila kumuumiza.
Naomba mawazo yenu Wana JF, ushauri wenu ni muhimu.