Namwambiaje huyu binti wa miaka 19 kuwa sina malengo nae?

Namwambiaje huyu binti wa miaka 19 kuwa sina malengo nae?

Sasa kwa nini hukufikiria hivyo kabla ya kumwambia utamuoa?

Anaweza kukuganda kama luba mpaka umchukie huyo.

Na ukimuacha anaweza kutengeneza uadui.
Ni kweli anaweza kutengeza uadui,ila sikutegemea Kama angeonesha upendo hivi,
 
Mpotezee tu, ikikulazimu muambie ukweli.

Unamkuza huyo, kwenye haya maisha ili ukomae vizuri unahitaji kuumia mara kadhaa.

Usijilize lize, mambo ya karma sijui dada yako atafanyiwa hivyo ni fikra za kipuuzi.

Simaanishi hujafanya kosa, umefanya. Usilirudie tena, na ukilirudia basi isiwe kwa mtindo huu....
 
Maana yake huyo ni mwanafunzi wa either form two au form three
 
Amani iwe nanyi Wana JF, ipo hivi: nipo kwenye mahusiano na binti mmoja hapa mtaani kwetu. Tumekuwa tukidate kwa wiki mbili sasa. Mwanzoni alionekana mgumu sana kunielewa, lakini baada ya kukaza juhudi, hatimaye alinikubali.

Katika jitihada za kumshawishi, nilimuahidi kumuoa, na hapo ndipo nilipojichanganya, maana aliamini nitamuoa kweli. Lengo langu halikuwa hilo; nilikusudia kupita tu, na tayari nimeshafanikisha hilo. Hata usiku wa leo amelala kwangu.

Tatizo ni kwamba binti huyu amenipenda kupita kiasi, lakini mimi sina mpango naye. Ni binti mdogo mwenye umri wa miaka 19 tu. Sasa sijui nianzie wapi kumweleza kwamba sina malengo naye, bila kumuumiza.

Naomba mawazo yenu Wana JF, ushauri wenu ni muhimu.
Sawa ila ndio amefika kilingeni hapa anataka unga wa ndele ili anachosema umsikilize yeye tu hata ndugu zako husiwasikilize..
Dawa yako inachemka..
 
Amani iwe nanyi Wana JF, ipo hivi: nipo kwenye mahusiano na binti mmoja hapa mtaani kwetu. Tumekuwa tukidate kwa wiki mbili sasa. Mwanzoni alionekana mgumu sana kunielewa, lakini baada ya kukaza juhudi, hatimaye alinikubali.

Katika jitihada za kumshawishi, nilimuahidi kumuoa, na hapo ndipo nilipojichanganya, maana aliamini nitamuoa kweli. Lengo langu halikuwa hilo; nilikusudia kupita tu, na tayari nimeshafanikisha hilo. Hata usiku wa leo amelala kwangu.

Tatizo ni kwamba binti huyu amenipenda kupita kiasi, lakini mimi sina mpango naye. Ni binti mdogo mwenye umri wa miaka 19 tu. Sasa sijui nianzie wapi kumweleza kwamba sina malengo naye, bila kumuumiza.

Naomba mawazo yenu Wana JF, ushauri wenu ni muhimu.
unasema ulifanya juhudi kubwa sana kumpata na ukampata right?

na sasa pia unafanya juhudi kubwa zaidi kumuacha right?

ulifanikiwa nadhani ni muhimu kuonana na daktari wa afya ya fikra kabla tatizo halijawa kubwa zaidi tuendako, haswa kwa wasiopenda kuchezewa kizembe namna hiyo..

Otherwise huna haja kulaumu kutekwa ila ni matokeo ya hizi juhudi zako za kitapeli 🐒
 
Back
Top Bottom