View attachment 1714923
Hali ya Nandy kwenye muziki sio nzuri kwa kweli anahitaji sana support yetu. Haya mambo ya kushika keyboard na kumpa sifa za uongo hatumsaidii tumwambie ukweli graph yake inazidi kwenda chini siku baada ya siku.
Huyu sio yule nandy wa ninogeshe au kivuruge.
Nandy amefikia kufanya wimbo na Koffi na hasipate walau watazamaji million 1 ndani ya siku tatu sasa na amekaa namba moja trend kwa masaa hayazidi 8 akatolewa na habari.
Imagine uwekezaji wa million 70 unaishia kupata likes na comments za insta na JF inasikitisha sana. Huko kwenye platforms za downloads na streams ndio huruma kabisa.
Kwa mwendo huu mtawalaumu bure WCB kuwa ndio chanzo cha kushuka kwake.
Mtamlaumu Zuchu kwa kubeba attention za watoto wa kike ambazo awali zilikuwa kwa Nandy.
Wale mnaokujaga na magazeti ya kufarijiana msaidieni hata mawazo.
Siku si nyingi nitashusha uzi kama huu kwa yule kijeba anaejaribu kujinasua wakati mtumbwi ushazama.