Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane)uwanja wa John Mwakangale Mkoani Mbeya leo tarehe 08 Agosti, 2022
Aliyoyasema waziri wa kilimo Hussein Bashe
Waziri Bashe asema Serikali itaanza kutoa zawadi kwa wakulima bora kila wilaya kuanzia mwaka kesho - Waziri wa kilimo, Hussein Bashe.
Katika kuazimisha siku ya wakulima Tanzania. Rais atasaini miradi yenye jumla ya thamani ya Tsh bil 182. Itakuwa ni miradi 21 ikiwa kwenye mikoa 7, wilaya 12. Itahusisha hekta 26700 na itazalisha ajira 120159
Aidha, itahusisha mabwawa makubwa matatu yenye ujazo wa cubic mita milioni 9. Yatakuwa na mfumo wa water tap kwa ajili ya mifugo
Miradi hii inachukua asilimia 51 ya bajeti nzima ya wizara iliyopitishwa na bunge. Bei ya mbolea imepungua, sasa kununuliwa kwa tsh 70000. Na baadhi yake zitakuwa ths 60000, zingine kufikia hadi tsh 50000.
Mfumo mpya wa utoaji wa ruzuku ndiyo umesaidia unafuu huu. Kila mfuko wa mbolea kupewa namba yake tofauti, pia mawakala kupewa namba tofauti kama mawakala wa makampuni ya simu ya vodacom na airtel.
Wakulima kusajiliwa kwa vidole kwa code maalumu kupitia mfumo wa ku scan. Wizara itajua nani kanunua mfuko wa mbolea, na sehemu alipo.
Sekta hii inachangia 25% ya pato la taifa. Imeajiri 60% ya Watanzania. Wakandarasi hawa waliosaini mikataba wanapaswa kuanza kazi kabla msimu wa mvua haujaanza
Mfumo wa rusuku utatoa pesa baada ya kupokelewa kwa mbolea. Hii inalenga kudhibiti pesa ya serikali isipotee. Sera za kukopesha bado siyo rafiki kwa wakulima
Gavana na waziri wa fedha pamoja na wewe Rais, imefika wakato sera za fedha ziendane na mifumo ya uchumi
Mwenye mashine anapewa fedha, ananunua mbolea. Hawapewi wananchi moja kwa moja. Wizara imeanza kuweka mioundombinu rafiki kwa wakulima na sekta ya kilimo ili iendane na matakwa ya sasa.
Nawaomba wadau wa maendeleo wabadilike. Fedha nyingi zinaenda kwenye capacity building na mambo mengine. Kwa sasa hadi watuambie pesa zinaenda wapi, capacity building na semina zimetosha. Sasa pesa lazima ziwe approved na Wizara
Aliyozungumza Rais Samia
Niungane na wengine kumshukuru Mungu kwa kukutana hapa viwanja vya John Mwakangale hapa Mbeya. Nilikuwa ziara hapa kwa siku 3, leo ya 4 kufunga maadhimisho haya. Nipo Mbeya kwa siku 4, haijapata kutokea
Nimshukuru Mh. Waziri Mkuu kwa kusimamia vizuri wizara za kisekta kulikopelekea kufanisha ufanisi huu. Wito wangu kwa wakulima na wafugaji ni kutumia mafunzo ya maonesho haya kuleta mapinduzi kwenye kilimo na uvuvi
Kauli mbiu ya mwaka huu inatoa hamasa ya kuhesabiwa. Nitoe wito kwa watanzania wote kujitokeza kuhesabiwa. Takwimu zinaonesha kuwa kufikia mwaka 2050 idadi ya watu itafikia bil 9, Afrika bil 2 na Tanzania itakuwa zaidi ya milioni 100
Mahitaji ya chakula yataongezeka sana. Hii ni fursa kuwa ambayo kama nchi tunapaswa kujiandaaa. Sekta za kilimo na uvuvi zimeendelea kuwa kiini cha maendeleo. Tumeongeza bajeti kufikia bil 954.
Ongezeko hili linalenga kutatua changamoto za upatikanaji wa mbegu bora, umwagiliaji na huduma za ugani
Nikuombe waziri wa fedha tutafute 15% ili wakandarasi waanze kazi haraka. Ruzuku hizi alizoomba Waziri zianze trh 15 mwezi huu. Takwimu zinaonesha kwamba mwaka 2020/21 sekta za kilimo zilichangia 26% za pato la taifa, ba 65.6% za ajira.
Kiwango cha chakula kilikuwa zaidi ya 100% hadi kutosha kuuza soko la nje. Zao la mchele pekee limeingiza bil 476. Safari ya kuzalisha mazao ya biashara imeanza sasa, tuitekeleze vyema. Serikali itaendelea kuvuta uwekezaji na kuboresha mazingira
Ndugu zetu kutoka nje waje tushirikiane, ili tuweze kuilisha Afrika. Miradi hii ikamilike kwa wakati ili wakulima waingie shambani mapema, wote twende na sura hii tunayoionesha kwenye sekta ya kilimo. Tunaagiza bidhaa kutok nje kwa gharama kubwa ambayo ni mafuta, ngano na sukari
Tunaingiza vijana kwenye sekta hii ili kupunguza utegemezi kutoka nje. Kila mkoa utenge maeneo ya kilimo. Tunahitaji hekta zaidi ya laki moja na hamsini kwa ajili ya mazao ya kimkakati. Tumeanza Dodoma, tunakuja Mbeya.
Kila mkoa utenge eneo kubwa kwa ajili ya zao linalomea vizuri mkoani humo. Fedha zipo kwa ajili ya maeneo haya. Vijana njooni kwenye sekta za kilimo. Tutawapatia mashamba yenye hati zenu
Tutaanza kuwaunga na mabenki mpate mikopo kwa riba nafuu. Timejipanga vyema na masoko. Ziara za nje ya nchi ninazokwenda ni kutafuta masoko, tunasubiriwa sisi tu kuzalisha ili tupeleke
Vijana ingieni sasa kwenye sekta ya kilimo. Kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa mbolea nchini. Sasa tunaanza kutoa ruzuku. Si miaka yote tutatoa ruzuku.
Upandaji wa mafuta ni kubwa sana nchini, tumetoa ruzuku. Mbolea pia tumetoa ruzuku, wakulima waweze kuzalisha. Wito kwa wakulima, limeni kibiashara. Tupate chakula cha kutosha kwa chakula, lakini pia tuuze nje
Tubadili utaratibu wa ruzuku, tuanzishe mifuko ya maendeleo ya kilimo. Itasaidi kupunguza ukali wa gharama. Kazalisheni kwa wingi, tuuze kwa wingi. Kalipeni tozo zilizobaki, naomba mlipe ili tuunde mfuko wa maendeleo ya kilimo. Tumechukua hatua za kuzalisha mbolea hapa nchini, tumetengeneza mazingira rafiki ya utengenezaji wa mbolea hii
Tunakwenda kumaliza kabisa tatizo la kutegemea mbolea kutoka nje. Wizara ya kilimo ihakikishe mifuko yote a mbolea ina alama za utambuzi. Kila kampuni ya uuzaji itangaze mawakala wake. Wizara ya kilimo na wizara ya fedha ihakikishe fedha zinatolewa kwa wakati.
Watendaji wote washiriki kikamilifu kusajili wakulima watakao nufaika na ruzuku hii. Naomba wakulima wote mkajisajili. Mbele tutaoa vitambulisho, ndivyo vitafanya upate huduma huko mbele. Baadae bila kitambulisho hutapata hudum, hasara ni kwako
Naomba sana wakulima mjiandikishe. Waziri nakuelekeza kusimamia vizuri bei ua mbolea hii. Maafisa ughani waende kufundisha wakulima, pesa ziende chini kusaidia wakulima. Masemina na mafunzo visubiri kwanza
Tuna hekta 10000 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Tufanye utafiti, tuzalishe mbegu zetu wenyewe. Itasaidia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni, pia tutapata uhakika wa mbegu tunazotumia
Nimeridhishwa na utafiti unaoendelea kuhusu mbegu hapa nchini. Sasa wanapata zaidi ya bilioni 40 kwenye uzalishaji wa mbegu. Waziri wa kilimo simamia hilo. Mwaka 2021/22 sekta ya mifugo ilikuwa na bil 21.6, mwaka huu mifupo peke yake ni bil 46.7
Tunaweza kuwa wa kwanza Afrika, au wa pili kwenye biashara ya mifugo. Tuna rasilimali za kutosha lakini hatuzitumii.
Tuna vijana wa SUA wanahangaika kutafuta kazi. Bado hawana kazi. Njia pekee kutoa ajira ni kutumia vijana hawa kwenye ranchi zetu. Halijafanyika, waziri shughulikia hili. Nimesema mara mbili, leo ya tatu. Waziri, sitarudia tena
Neno la Rais Kuhusu Ranchi za Nchini, ataka vitalu vifutwe
Tuna rachi 14 na jumla ya mifugo 155,554. Rachi nyingi zimekodishwa na hazina manufaa kwa serikali. Naagiza kufanya uchambuzi wa ranchi zote zilizokatwa, vimeingiza kiasi gani kwa serikali. Ikibidi kufuta kabisa usajili wa vitalu hivi
Huoni hata ranchi moja zimewekezwa kwa ubia. Ranchi zote zimekatwa vitalu kwa manufaa ya watu binafsi. Sasa nitaanza kuwashughulikia ili nanyi mshughulikie vitalu. Vijana waingizwe kwenye ufugaji. Tuna masoko ya kutosha ya kupeleka hizo nyama.
Njia pekee za kufanya viwanda vyetu vifanye kazi ni kuingiza vijana kwenye ranchi zetu, wanenepeshe mifupo. Uvuvi nako tumepanisha bajeti hadi kufikia bil 135.7. Tanzania hatujaingia kwenye uvuvi wa bahari kuu
Fedha tumeweka nyingi, ili lengo tulilojiwekea la kuongeza uzalishaji wa samaki hadi tani laki 6 tunapofika mwaka 2025 litimie. Soko lipo kubwa sana kwa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Tanzania tumepata ithibati katika maeneo mbalimbali. Tunaweza sasa kuuza nje ya nchi. Twendeni sasa kuuza mazao hayo
Nawaagiza wakuu wa mikoa kusimamia maeneo yanayotumika kwa sherehe hizi yasitumike kwa mambo mengine. Viwanja vya nanenane vianze kutengeneza fedha. Mapato yaache kuingia mifukono badala ya kuviboresha
Rais asisitiza kuhusu sensa
Niongeze sauti na mimi kwenye sensa. Twendeni tukahesabiwe. Waziri wa kilimo nilikuagiza kutafuta magari kwa ajili umwagiliaji mpaka leo sijasikia chochote. Punguzeni urasimu
Watendaji hawawezi kwenda bila magari. Fedha ipo, shida nini? Magari yanunuliwe, kazi ifanyike. Nihitimishe kwa kusema maonesho haya yamefungwa rasmi.
Nimeona ukarimu wa Mbeya. Nimepokelewa vizuri, nimeulizwa hoja nyingi sana. Nawashukuru mawaziri waliokuwa nami. Changamoto zote tunafanyia kazi
Kila nilipopita nilipewa zawadi. Nashukuru sana kwa zawadi. Baada ya kusema hayo asanteni sana mbeya. Nakwenda kumalizia Mbarali, jioni naingia Njombe. Asanteni sana.