Mtaji wako ni uthubutu wako unaeza anza na kidogo ulichonacho sema sisi huwa tunataka hadi tufikishe kiwango fulani ndipo tuanze rasmi kujiajiri jambo ambalo ni mtihani kulitekeleza,. Sema kikwazo pia ni mazingira si rafiki kwa biashara rasmi tozo zinazidi uhalisia, pia mfumo wa elimu haumjengi mtu kujiajiri bali kuwa mtumishi jambo linalopekea mhitimu kuona aibu na kuwa selective kuchagua kazi badala ya kujiajiri.MTAJI
Mengine ngonjera tu.
Huna tofauti na Mimi aisee nilipo maliza chuo nili wambia nyumbani sihitaji kuajiriwa hawa kuni elewa kabisa ila nili wambia msimamo wangu ndo huo na utabaki kuwa hivyo nashukuru Mungu toka nimalize chuo mpaka sasa sijawahi omba ajira na sijawahi ajiriwa maisha yana kwenda Mungu ni mwema sana sana kwangu nafanya biashara zangu ndogo ndogo Mungu ni mkubwa tatizo co mtaji tatizo kubwa ni uoga na uthubutuMkuu
Mimi nimejiajiri tangu 2014
Ni mjasiriamali mdogo
Nilikataa kuajiriwa na Polisi
Sijawahi kujutia maamuzi yangu
Bado sijafikia malengo kwa 100% lakini naona milango ikifunguka siku hadi siku
Nimejifunza uthubutu, kupambana, uvumilivu na kusimamia ninachokiamini bila kuyumba ( Consistence) na vimenisaidia Sana.
Mwanzo ndugu zangu hawakunielewa, walitaka niajiriwe lakini niliweka msimamo sihitaji kuajiriwa lakini sasa wameelewa nilichokuwa namaanisha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mimi si mhanga wa ajira. Nimeajiriwa na Serikali lakini pia nimejiajiri mwenyewe hvyo nina uzoefu mkubwa wa kuweza kushahuri vijana maana mimi ni Business Coach
Sorry nilisoma vbaya
Huna tofauti na Mimi aisee nilipo maliza chuo nili wambia nyumbani sihitaji kuajiriwa hawa kuni elewa kabisa ila nili wambia msimamo wangu ndo huo na utabaki kuwa hivyo nashukuru Mungu toka nimalize chuo mpaka sasa sijawahi omba ajira na sijawahi ajiriwa maisha yana kwenda Mungu ni mwema sana sana kwangu nafanya biashara zangu ndogo ndogo Mungu ni mkubwa tatizo co mtaji tatizo kubwa ni uoga na uthubutu
Another motivation speakerSio kweli
Kikwazo kikubwa ni umaskini wa mawazo. Hakuna ubunifu.
Hela zipo nyingi sana
Mkuu Umeandika Points.SABABU KUBWA NI MINDSET
Asilimia kubwa ya vijana mfano hapa Tanzania tunaishi chini ya utamaduni na mfumo wa maisha unaofanana kwa wengi. Kutokana na hali hii, wazazi/walezi wanaandaa vijana kusoma ili wapate kazi nzuri kwa kuajiriwa. Hvyo kijana anaanza kusoma akilenga kuajiriwa sehemu fulani na sio kujiajiri sehemu fulani. Kutokana na % kubwa kuwa na Mindset inayofanana, ndiyo maana tatizo la ukosefu wa ajira linazidi kuwa kubwa kwa vijana wengi.
SABABU BAADHI NDOGO NDOGO ZINAZOUNDA SABABU KUBWA TAJWA HAPO JUU NI-:
1. Kijana Kutotambua wapi aanzie ili kujiajili.
2. Vijana wengi wanahisi hawana uwezo wa kufanya kazi fulani wakisema kazi hzo ni za watu fulani au ni za mataifa fulani na mwisho wa siku hukaa bila kuwa na kitu cha kufanya maana kila wanachofikiri wanaona kwao hakiwezekani.
3. Uzembe wa kuchukua hatua, yaani kijana anasema kesho nitafanya na kesho huzaa kesho bila kuanza anachokifikiri.
4. Kukosa plan B na hvyo Kupoteza muda mwingi kulaumu Serikali, ndugu na marafiki badala ya kuangalia nini cha kufanya.
5. Vijana wengi wanahisi kujiajiri ni kuuza bidhaa tu na kama hana fedha za kuanzisha biashara fulani basi anakaa wakati anaweza kuanzisha biashara inayouza huduma na akaingiza fedha nyingi bila hata mtaji wa fedha.
6. Baadhi walijaribu kujiajiri lakini walichagua mawazo ya biashara yasiyosahihi (WRONG BUSINESS MODELS) ambapo biashara zao zilikufa mapema na wakakata tamaa.
NINI KIFANYIKE KAMA SULUHU
Suluhu kubwa ya tatizo la ajira ni jamii kwa ujumla kubadili MINDSET zao ili mtu awe na mawazo ya kujiajiri tokea akiwa mdogo.
MAMBO MENGINE YA KUZINGATIA KAMA SULUHU NI KAMA
1. Jambo la kwanza ni kuepuka vikwazo kama hivyo nilivyovitaja hapo juu.
2. Vijana watambue mtaji mkubwa ni akili na uwezo waliopewa na mwenyezi Mungu wala sio pesa.
3. Vijana wasiwe wabinafsi. Mfano, mtu anawazo zuri la biashara na hana pesa na anashindwa kumshirikisha mwenzake mwenye pesa ili waanzishe biashara na hivyo anakaa na wazo lake hadi linakufa bila mafanikio.
4. Vijana wasikimbilie kuuliza biashara gani inalipa wataangukia shimoni maana mahesabu ya kwenye karatasi ni tofauti na mahesabau halisia. Hivyo vijana wajikite katika kutatua matatizo ya watu hapo ndipo kuna biashara inayolipa maana mtu akitatuliwa tatizo lake yuko tayari kulipa kiasi chochote.
5. Kila kijana aamini kuwa anauwezo wa kufanya jambo fulani hata kama anahisi hana uwezo wa kufanya. Imani inaweza kufanya mambo makubwa.
Another motivation speaker
Kwamba we unaona hela zipo nyingi sana ila vijana ndio hatuna uwezo was kufikiria?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna kitu kinaitwa root cause failure analysis (RCA)
bila ufaham mzuri kila mtu atazuka na visababu vyake kimtazamo ambavyo sio root cause.
lakini jibu sahihi lisilenge mtu mmoja ametokaje Bali asilimia mfano 50% au 70%
tunapotoa majibu tunatakiwa kutazama Wastani wa wahusika sio mafanikio ya mtu mmoja watatu au wanne sababu hawa hawawakilishi sample spaces or representative sample
vijana kwanini asilimia kubwa hawawezi kutoka/kufanikiwa/kupiga hatua/kujiajiri/kujitegemea/kujijenga ...... tatizo ni nini?
1. Aibu...... nikweli nchi nzima vijana wanakwama sababu wanaaibu? Sio kweli
2. Uzembe .... nikweli vijana mikoa yote wazembe? Sio kweli
3. Elimu.... nikweli vijana wakitanzania asilimia kubwa Elimu haiwasaidii .... may be but not certainly
4. Malezi.... nikweli malezi yanawakwamisha maelfu ya vijana! Kwamba wazazi wanamalezi yakufanana nchi nzima? Kigoma, tanga, mtwara .... singida......shinyanga? Sio kweli
5. Mazingira... je mazingira yanaweza kuwa sababu? May be but not certainly kwa taifa zima
6. Uthubutu.... nikweli vijana wengi hawana uthubutu? Kivipi kama taifa tunaongelea asilimia kubwa ya vijana zaidi ya 50%
7. Uoga... kwamba zaidi ya 50% ya vijana wetu waoga? Sio kweli
Mkuu naomba nikufuate PmHapana mimi si mhanga wa ajira. Nimeajiriwa na Serikali lakini pia nimejiajiri mwenyewe hvyo nina uzoefu mkubwa wa kuweza kushahuri vijana maana mimi ni Business Coach
Nifuate mzee usihofu.
Asante boss. Wachache Sana watakuelewaKwenye kujiajiri ni kutokufikiria zaidi na kufanya uchunguzi wa nini ambacho anaweza kukipeleka sokoni kikakubalika kirahisi.
Ila Mkuu tuache siasa nyingi pia
UVIVU TUU! na TAMAA za kijinga..
tukirudi kwenye kuajiriwa utakubaliana na mimi kuwa kila taasisi inahitaji watu wakugrow value ya shirika/kampuni sasa miongoni mwa vijana wengi wamejawa na uvivu+tamaa za haraka haraka anataka akipata hela tayari break yake ya kwanza kwenye gari na mademu! + MALEZI MABOVU.
Siku zote ukitaka kupima Inteligence test ya kijana mpe kazi bila pesa,hata ya kujitolea.
Sent using Jamii Forums mobile app