Nani aliamuru jengo la bunge Dodoma kujengwa uswahilini

Nani aliamuru jengo la bunge Dodoma kujengwa uswahilini

Aliyeshauri Kama Yupo Akamatwe Atupwe Ndani
 
Waliangalia vitu muhimu:
Stesheni ya Reli ipo karibu.
Ipo karibu na Hospitali ya Mkoa
Sio mbali na makao makuu ya polisi ya mkoa
Huduma za mabenki za kumwagwa
Airport ipo karibu
Nyumba za wageni zipo nyingi.
Ipo mjini
 
Kila nikipita mbele ya ofisi za bunge Dodoma najiuliza nani alimuru lile jengo kujengwa pale
Hakuna parking ya kutosha,magari ya wabunge mengi huishia nje ya uzio
Ni uswahilini hakuna utulivu huku wahuni wa makole huku wanafunzi wa cbe na vurugu zao
Mapori yote ya dodoma mkakosa kukamata hata ekari kumi sehemu tulivu
Kongole JK kupeleka UDOM sehemu sahihi
Swali lako ni la wakati huu au wakati uliopita?

Majinga yanaweza hata kuuliza hivi wayahudi kwanini walitumia miaka 40 kutembea kwa miguu kutoka Egypt hadi Caanan si wangetumia magari au ndege siku moja tu...
 
Swali lako ni la wakati huu au wakati uliopita?

Majinga ya JF yanaweza hata kuuliza hivi wayahudi kwanini walitumia miaka 40 kutembea kwa miguu kutoka Egypt hadi Caanan si wangetumia magari au ndege siku moja tu...
Kama itahitajika nafasi kubwa kwa ajili ya shughuli za bunge nje ya ukumbi wa bunge serikali inaweza kulipa fidia wale waliojenga karibu na jengo la bunge na kuongeza eneo.
 
Nasikia parking haitoshi, magari ya waheshimiwa yanapaki zig zag na wakati mwingine wahuni wanafanya yao!! Nasikia Mzee wa S&P ndiye alilazimisha jengo lijengwe pale badala ya kupelekwa Jedengwa!
 
Kama itahitajika nafasi kubwa kwa ajili ya shughuli za bunge nje ya ukumbi wa bunge serikali inaweza kulipa fidia wale waliojenga karibu na jengo la bunge na kuongeza eneo.
Bunge lilikuwa linatakuwa kuwa na eka hata 100! Angalia Ikulu ya Dodoma nadhani ina eka mia tano!!!
 
Bunge lilikuwa linatakuwa kuwa na eka hata 100! Angalia Ikulu ya Dodoma nadhani ina eka mia tano!!!
Kwa hiyo ushauri wako ni upi? Eneo kubwa la bunge litafutwe na jengo jipya la bunge lijengwe huko?
 
Tatizo lako mtazamo wako umeishia urefu wa pua yako

Unahisi hapo palipo jengwa ikulu baada ya miaka 50 ijayo patakuwaje???

Wazee wetu waliona miaka 500 mbele wewe unaona miaka 10 mbele

Bila Shaka utakuwa mkazi wa mkoa wa Pwani au Dar.

Kwa sababu watu wa Dar, Arusha na Pwani hawataki kuona maendeleo yanafanyika nje ya mikoa yao
 
Kwanza naomba uanze na maana ya neno uswahilini. Je jengo la bunge kweli liko Uswahilini?
Kale ka mtaa ka Makole pale ni uswahili sanaa,

Basi ule upande kama unaenda cbe (kushoto) kale ka mtaa ni uswaaaz sanaa mara mbuzi zina zururaaa

Alichosema mdau wa uzi huh yupo sahihi, bunge lilipaswa lijengwe sehemu flan very planned yaani kuwe na huduma hizo za parking za kutoshaaa,

Kwa miaka invyozidi kwenda, Je lile eneo litarubjsi maongezo ya majengo mengine kwa baadae incase kukitokea uhitaj
 
Kila nikipita mbele ya ofisi za bunge Dodoma najiuliza nani alimuru lile jengo kujengwa pale
Hakuna parking ya kutosha,magari ya wabunge mengi huishia nje ya uzio
Ni uswahilini hakuna utulivu huku wahuni wa makole huku wanafunzi wa cbe na vurugu zao
Mapori yote ya dodoma mkakosa kukamata hata ekari kumi sehemu tulivu
Kongole JK kupeleka UDOM sehemu sahihi
Kweli halikutakiwa kuwa hapo. Jengo cha Chimwaga ndio lilikuwa liwe la Bunge na la Kamati Kuu ya Chama (mambo ya chama kimoja). Hapo lilipo ilikuwa liwe kwa muda tu wakati Chimwaga inakamilika. Hata majengo ya mawizara hayakutakiwa kuwa yanapojengwa sasa hivi. Ila kama kawaida yetu neno Masterplan haliko kwenye msamiati wetu.

Amandla...
 
Kuhusu uswahilini no comment, lakini kuhusu barabara ile ufinyu wake ni changamoto hasa kama siku hiyo kuna namba 1 au 2 mmoja anaenda bungeni. Usumbufu wake kwa watumiaji wa barabara ni mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom