Nani aliamuru jengo la bunge Dodoma kujengwa uswahilini

Watunga Sheria ni kina kibajaj, Taletale na msukuma halafu anayepitisha Ni ndugai.
 
Kwa wanayo yaongea mle bungeni hata Hilo eneo bado Ni zuri invebidi Bunge lijengwe Tandale au Manzese
 
Bunge linaspace ya kutosha ya parking mpaka hivi sasa kama uliwahi kupita njia ya nyuma upande iliopo veta utaona space iliopo,au upande wa nyuma wa CBE zilizopo ofisi za TANTRADE eneo ni kubwa mno nadhani hawaruhusu gari zote kupark ndani maybe kuepusha usumbufu
 
Hapo ndo panafaa
Tuwe tunawaona wanaoingia na wanaotega

Pia tuwe tunaona yanayojiri

Ukipeleka porini ndo ile minada ya Ndugai hufanyika kwa utulivu
 
Kwanza kabisa baada ya Uhuru shughuli za bunge zilikua zinafanyika kwenye ukumbi wa karimjee jijini Dar, then zikahamishiwa Dodoma lkn jengo lilikua Ile white house pale katikati ya mji barabara ya nane, kipindi hicho hapo lilipo jengo la bunge la Sasa ilikua nje kabisa ya mji wa Dodoma. Cbe ndio usiseme. Imagine uwanja wa ndege ulikua hapo area C walipokua wanakaa vigogo ukiondoa wale vingunge waliokua wanakaa uzunguni.
Kipindi kile tunasoma Mazengo, shule ilikua porini kabisa. Msalato ndio usiseme. Enzi zile mnadani ilikua Ni hapo mjini kabisa.
Ni Kama chuo kikuu Dar, miaka ya 70 kilikua nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
 
Kwa hiyo mji umesinyaa maana udsm bado ni mbali kutoka posta city center,ila kutoka city center ya dodoma mpaka bungeni unaenda kwa mguu,city center ya dodoma nyerere square ukikaa uwanja wa ndege unaona mita 300
 
Bunge lenyewe ni la kiswahili halizingatii sheria wala katiba wacha liwe huko huko uswahilini
 
Kwa hiyo mji umesinyaa maana udsm bado ni mbali kutoka posta city center,ila kutoka city center ya dodoma mpaka bungeni unaenda kwa mguu,city center ya dodoma nyerere square ukikaa uwanja wa ndege unaona mita 300
Hivi Dom uwanja wa ndege bado Ni ule ule wa area C tuliouacha wakati wa Nyerere tukiwa tunasoma Mazengo chini ya Mkoba RIP
Msasa na Ddungu?
Long time sijatia mguu hapo.
Sasa mlikimbilia Nini kujenga uwanja chatu kumbe makao makuu yenu hayana uwanja wa ndege?
 
Bado ni huo huo unaotumika ila kuna mpya unajengwa mkuu bonge la uwanja
 
Daaah! Mkuu umenikumbusha Walimu wangu wa Mazengo Sekondari, enzi hizo: Mkoba RIP - Headmaster, Msasa - Second Master & Ddungu - Discipline Master!
 
Jengo la bunge aliamuru lijengwe pale JPM.

Kama kawaida Nyumbu wamefurahi kusikia hivyo
 
Jengo la bunge aliamuru lijengwe pale JPM.

Kama kawaida Nyumbu wamefurahi kusikia hivyo
Wakati linajengwa lilikuwepo lile la zamani Ile sehemu iko vizuri sema tu utengenezaji wa mazingira bongo bado sana
 
Hao naweza kuwatetea Nairobi kupata ardhi tupu inaweza kuwa changamoto ila sio Dodoma, jengo zuri nafasi finyu, location pia sio sahihi

Kamfufueni Sitta , spika wa viwango awape majibu ya maswali yenu!
 
Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifanyika wakati utawala ulikuwa wa chama kimoja. Kwa sababu umuhimu ulipewa kwa jengo la Mkutano Mkuu wa Chama cha CCM ambalo pia lingetumika kama Bunge. Jengo hilo ndio la Chimwaga. Ulazima wa kuwa na jengo la Bunge ulitokea baada ya mfumo wetu kugeuka kuwa wa chama kimoja maana Bunge lisingeweza kutumia jengo la Chama kimoja cha siasa. Kwa vile jengo la Chimwaga lilikuwa linasua sua uamuzi ulifanyika kupangisha ukumbi uliojengwa na LAPF kwa ajili ya shughuli za Bunge kwa muda mpaka jengo la Chimwaga litakapokamilika. Baadae serikali lilinunua ukumbi huo na kuufanya kuwa jengo rasmi la Bunge. Huu ukumbi wa sasa ulijengwa sehemu hiyo hiyo ili ukidhi mahitaji ya Bunge la sasa. Mpango wa kutumia jengo la Chimwaga nao umekufa. Mambo yoye haya yalifanyika kabla ya JPM kuwa waziri.

Amandla...
 
Kuhusu uswahilini no comment, lakini kuhusu barabara ile ufinyu wake ni changamoto hasa kama siku hiyo kuna namba 1 au 2 mmoja anaenda bungeni. Usumbufu wake kwa watumiaji wa barabara ni mkubwa sana.
Sio lazima upite CBE,unaweza kuzungukia Shoppers,Njia panda ya Area D ukasepa sio hadi mpishane na misafara

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…