Nani Alikuwa Bora kati ya Zidane na Ronaldinho?

Nani Alikuwa Bora Kati ya Zidane na Ronaldinho?


  • Total voters
    27
  • Poll closed .
Dinho alikuwa entertainer uwanjani... Na ni mchezaji wa kawaida Kwa maana hana chochote cha kukumbukwa lakini alikuwa mjanja sana kuweza ku fool watu wengi wakamuona Kama mchezaji bora kuwahi kutokea.. Zidane ni legend katika soka, ni mtu mwenye heshima na historia kubwa kisoka na kuna mambo mengi sana ya kukumbuka kuhusu zidane. Zidane aliweza kuamua mechi, dinho hakuwa na uwezo huo , ni Kwa mda mfupi tu alikuwa tegemezi Kwa barcelona lakini alivokuja messi ghafla watu , makocha na wataalam wa mpira wakahamisha macho yao yoye Kwa messi.. Ikumbukwe hata mourinho alijizajititi kumdhibiti messi zaidi kuliko dinho (alipanga mkakati chelsea wakamtoa uwanjani) Kwa macho ya kawaida huwezi liona hili, ni huyu huyu messi aliyekuja kudumu na kuwa tegemezi, kuandika historia na kuvunja record zilizokaa Kwa zaidi ya miaka 40 ..

Katika wachezaji bora kuwahi kutokea dinho hayumo, wengi tusingependa kusikia hili lakini dinho hayumo na wala mijadala ya soka huwezi msikia dinho.. Sana sana utasikia wakimlinganisha messi na maradona au pelle na hii inaonesha ni Kwa kiasi gani dinho hana chake katika mpira....

Zizzo was far better !
 

 
Acheni Gaucho aende zake jamaa uwezo wake ulikuwa si wa kawaida kwenye kutandaza kandanda.

 
Nimeandika humu na naomba utenganishe mtu anaechezea mpira na mtu anaeujua mchezo wa mpira wa miguu
 
Mkuu Gaucho ni mtu mwingine
 
Gaucho was the best ever!....angalia hata mechi walizocheza barca na real wote wakiwa uwanjani!
 
Madrid wenyewe baada ya kupigwa 3 bila pale Bernabeu, 2 katupia Dinho moja etoo mashabiki wote walinyanyuka, wakampigia makofi Dinho. Dinho alikuwa anakuafanya uone kama umewadhulumu hela ya kiingilio kwenye vibanda umiza, sababu anakupa burudani kubwa kwa gharama ndogo.
 
Kuwa mchezaji mzuri sio sababu ya kuwa kocha. Pele na ubora wake hajawahi kuwa Kocha. Kwa hiyo kuuliza Dinho yuko kwa kuwa unamuona Zidane ni kocha hilo ni kosa kubwa sana.
anamaanisha amefulia mkuu muelewe.
 
Na mimi nilitaka kusema hivyo.


MAGUFULI4LIFE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…