Nani aliye Msafi ndani ya CCM??

Mtu yoyote makini hawezi kuwa chawa!, huyo jamaa sio chawa na hajawahi kuwa chawa!, jamaa ni very objective, kwenye mazuri anapongeza na kwenye mabaya anakosoa!, chawa kamwe hawezi kukosoa!.
P
Ukosoaji wa kutoa hoja kimalienge ni uchawa...

Unataka kusema fulani hafai unaanza kusema ajitathimini...
 
CCM siyo chama cha kijamaa wala siyo chama cha wakulima!!
 
Hivi mnamjua Jerry Slaa au! Mtu kakataa 300M.
 
Mkuu wewe ni mtu mwenye imani ya kipekee. Nimejiuliza kama unaishi Tanzania.

Jiulize, kwa muundo wa mamlaka wa nchi hii, inawezekana wizi unaohusisha kiasi kinachofikia USD 100m kuhusiana na miradi ya maendeleo au uwekezaji ukafanikiwa na wahusika kuwa “scot-free” bila mamlaka ya juu kabisa kuwa na mkono wa moja kwa moja ama kwa kuruhusu au kwa kufumbia macho?

Mara ngapi matukio ya aina hiyo yametokea: yaliyojulikana na yaliyofichwa?

Tunazungumzia hasa ufisadi wa mabilioni unaofilisi taifa. Acha rushwa za polisi, mahakama, ardhi, n.k. ambazo nazo zinavuruga mipango ya nchi. Serikali ya CCM inakuwaje innocent?
 
Msafi ni Philip Mangula pekee. 2015 nilishuhudia kwa macho yangu ameletewa 300m kwenye boksi ili asaidie kupitisha jina la mgombea fulani Kamati ya Maadili alisema Kwa sauti, "hela zote hizo za nini na nitazipeleka wapi? Yani unanua uongozi!?" Aliyetumwa kuzileta alirudi kichwa chini huku mimi nikimwambia "si ungechukua ukanipa mimi?" Akacheka tu na mwisho akanipa nauli sh. 50,000.
 
CCM watu safi, wamo wa kumwaga!. Mimi namfahamu jamaa mmoja aligombea Kawe, hakutoa hata senti moja kwa yeyote na matokeo yake alipata kura 1!.

Hivyo wasafi wa type hiyo CCM wapo wengi tuu.
P
Ndani ya CCM kumejaa chawa kila kona. Wanachotofautiana ni aina tu...kuna chawa wa kwenye nguo na chawa wa kwenye nywele ambao ni weupe na weusi, mtawalia. Na madhara yao kwa binadamu ni mamoja.
 
Ukosoaji wa kutoa hoja kimalienge ni uchawa...

Unataka kusema fulani hafai unaanza kusema ajitathimini...
Hiyo inaitwa playing safe, mfano mzuri ni Maza alipohojiwa na Kikeke kuhusu kugombea 2025, alisema tuzungumzie ya sasa, ya 2025 nani anajua?. Gazeti la Uhuru likaandika hagombei, Mhariri akatimuliwa!, kisha akasema 2025, tutakwenda na mwanamke, by implication ni yeye!, who would dare kumwambia 2025 itoshe?, lazima uende taratibu, kwanza show her support Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! kisha a dare devil unamgonga na kitu kizito utosini kama HII sauti!, message sent.

It's better to play it it safe than sorry!, hivyo mtu mwenye maandiko ya type hii, ukimuona ni chawa, ujue ni mambo ya viwango vya uelewa!.
P
 
Waliobakia ni Wazee wa Mabulungutu.👎Wazee wa kuzikopa kwa jina letu na kuzisunda kwenye Benki za CHINA HONG KONG.

Wakati wa kulipa tunalipishwa sisi Manamba na Watoto wetu na Vijukuu na Vilembwe vyetu kwa Mijeledi ya Kodi Tozo Takrima nk.

Wakati huo hou wamawaanda Watoto wao wawatawale Watoto wetu,Wajukuu wao wawatawale Wajukuu wetu Vilembwe vyao viwatawale Vilembwe vyetu ni kama Masultani wa Zanzibar lakini hawa ni Wanyiramba Watumbatu Wangazija Wamakonde nk. weusi wenzetu.

Tukiwaambia wafanye HAKI kwanye Chaguzi hawataki wanavuruga Chaguzi kwa kutumia mabavu UJECHA tukiwaambia MABAVU yatatuingiza kwenye Vita vya sisi kwa sisi wanaziba masikio.

Ogopa sana Mtu aliyepoteza Matumaini.
 
Pasco wanao-play safe wana msaada gani kwa wale wanaotumia ile kanuni ya "Call spade a spade and not a big Spoon"?

Play safe people always are bard people!! How could you differentiate safe players with Cowards and hypocrites??


Dr. Martin Luther King aliwahi kusema "in the end we will remember not the words of our enemies, but the silence of our friends"

Kristo Yesu naye pia alisema mtu kama anataka kuwa moto awe moto au kama anataka kuwa baridi awe baridi na siyo vuguvugu.

Kristo Yesu alisema siku ya mwisho watu wote vuguvugu atawatapika.

Don't be Lukewarm my broda!!!

Pascal Mayalla aione kwenye jalada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…