Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Kwisaro

Member
Joined
Mar 28, 2018
Posts
30
Reaction score
45
Mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa ambayo imebahatika kutoa viongozi wengi katika Serikali zote za kuanzia muasisi wa taifa hili.Lakini ni kati ya mikoa ambayo maendeleo yake yako nyuma sana, ukifatilia kiundani ni kuwa hata viongozi ambao walipewa nyadhifa mbalimbali wao kwa wao hawaelewani bila kujali itikadi zao za vyama.

Kwa mfano Wasira na Jaji Warioba ni watu wasiopikika chungu kimoja japo wote wako ccm. Mwanasheria mkuu aliyestafu Jaji Welema na Mbunge Nimrod Mkono na Pro ,Mhongo ni maadui na uhasama huu unatokana na masilahi,baada ya kuchaguliwa Mhongo kuwa waziri wa nishati kwa kushirikiana na Mwanasheria mkuu Jaji Welema walikata mirija ya ulaji ambayo Nimrod mkono alikuwa analipwa kwenye kampuni yake ya uwanasheria kutokana na lile sakata la Dowas.

Mkono nae nae akaamua kuwalipua kwa kumpa documents Kafulila na kuwakomalia mbugeni na kusababisha Mhongo,Eriakim Maswe na Welema kupoteza nafasi.

Ninachomaanisha hapa ni kuwa viongozi kutoka mkoa wa Mara bila kujali itikadi zao ni watu ambao hawawezi kukakaa meza moja na kuzungumzia matatizo ya Mara kwa sababu wao kwa wao hawapendani.

Ni mji ambao hata miundombinu yake ni shida pamoja na kuwa na ziwa victoria lkn maji bado ni shida hasa kwa wakazi wa nje kidogo ya mji, Ukienda makao mkuu ya wilaya ya Serengeti mji wa Mugumu huwezi amini palivyo choka na wakati wako karibu na hifadhi.

Wakuu wa kaya nao wameususa kuanzia awamu ya Jk na sasa JPM ndio hana hbr kabisa na mkoa wa Mara.

Tupatiwe fursa hata viwanda vilivyokuwepo vifanye kazi pamoja na kuwa na chuo kikuu ,kwani chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere ni jina tu hakuna kinachoendelea.
 
Nyie wenyewe mmefanya nini kabla ya kuanza kulalamika ?
 
Wewe ungesema watu wa Musoma vijijini hawaelewani. Maana hao wote kwao ni Musoma Vijijini.

Muhongo, Maswi, Werema na Mkono wote ni wa Musoma vijijini na mbunge wao alikua Mkono kabla hawajaligawanya jimbo hilo.

Watu wa Serengeti huna haja ya kuwalaum maana serikali mdio haikufanya mgawanyo sahihi wa rasilimali, Mbuga iko Serengeti ila makao makuu yakawa Arusha.

Watu wa Arusha wakaendelea kwa kutumia mgongo wa watu wa Serengeti.

Tatizo la mkoa wa Mara ni unequal distribution of resources. Mkoa wa Mara ni mkoa tajiri, una dhahabu na madini mengine karibu kila kijiji, una ziwa, una mbuga kubwa kuliko zote Afrika.

Cha ajabu, Dhahabu yote haiwasaidii watu aa Mara, migodi ya kihuni kama Meremeta imewaibia wana Mara, North Mara kila mtu anajua, Serikali ikaua viwanda vyote vya samaki, wao watauza wapi samaki? Wajita na wakwaya wamebakia kua na majungu tu maana hawana kazi nyingine ya kufanya.

Serengeti haiwasaidii wana serengeti, mbuga inayoingiza 80% ya mapato ya utalii Tanzania, cha ajabu wanaofaidika nayo ni watu wa Arusha na Kilimanjaro. Hata chuo kimoja cha utalii cha serikali cha ngazi ya cheti serikali haikuwajengea wakazi wa serengeti, vyote viko Arusha na Kilimanjaro.

Watu wa Mara hasa Serengeti na Tarime wana ardhi nzuri ya kulima, wanalima misimu 2 kwa mwaka lakini hawana masoko, wakitaka kuuza Kenya serikali haitaki, wanakua hawana namna zaidi ya wizi wa ng'ombe.

Serikali ndio imechangia kuua mkoa wa Mara. Watu wa Mara inabidi tuwalaum wenzetu waliotangulia kupata fursa kisha hawakuendeleza mkoa wetu.

Watu wengone wakipata uwaziri wa maji tu mikoa yao inakua na maji hadi ya kuogeshea kuku, urais ndio balaa.

Watu wa Mara tujifunze. Ukipata fursa itumie.
 
Wana Mara wanafanya maendeleo makubwa Mwanza.
Wengi wa Wana Mara wamewekeza Mwanza lakini pia kutokuwekeza Mara kunachangiwa na Wana Mara wenyewe kutokuwa na Umoja wa pamoja kuwaunganisha.
Wajiunge pamoja na kukubaliana wapi master plan ya Jiji la Mara la baadae liwe wapi, kwa mfano wanaweza kuichagua wilaya ya Butiama kama Centre zone ya Jiji la Mara la baadae.
 
Wewe ungesema watu wa Musoma vijijini hawaelewani. Maana hao wote kwao ni Musoma Vijijini.

Muhongo, Maswi, Werema na Mkono wote ni wa Musoma vijijini na mbunge wao alikua Mkono kabla hawajaligawanya jimbo hilo.

Watu wa Serengeti huna haja ya kuwalaum maana serikali mdio haikufanya mgawanyo sahihi wa rasilimali, Mbuga iko Serengeti ila makao makuu yakawa Arusha.

Watu wa Arusha wakaendelea kwa kutumia mgongo wa watu wa Serengeti.
Maswi na Werema kwao ni Tarime na Mkono ni Butiama na sio Musoma vijijini.
 
Wewe ungesema watu wa Musoma vijijini hawaelewani. Maana hao wote kwao ni Musoma Vijijini.

Muhongo, Maswi, Werema na Mkono wote ni wa Musoma vijijini na mbunge wao alikua Mkono kabla hawajaligawanya jimbo hilo.

Watu wa Serengeti huna haja ya kuwalaum maana serikali mdio haikufanya mgawanyo sahihi wa rasilimali, Mbuga iko Serengeti ila makao makuu yakawa Arusha.

Watu wa Arusha wakaendelea kwa kutumia mgongo wa watu wa Serengeti.
Wewe unaijua Mara vzuri? Werema na Mkono watokeee Musoma Vijijin? Rudi kaangalie vzur Wilaya za Mkoa wa Mara.
Mleta mada umesahau kuwaambia hao Jamaa zako wa Mara wanabana sana Ulaji wapewapo nafasi kubwa mwisho wa siku wanalipuliwa kirahisi mno. Mbadilike na msome tabia ya mchezo mahala pa kazi.
 
Tatizo kubwa la watu wa Musoma ni ubaguzi ulioegemea kwenye koo, na kabila, mfano Wakurya wamewagawanyika zaidi ya koo 10 na wanabaguana hasa yaani akitokea kiongozi kwenye koo fulani hapewi ushirikiano na koo nyingine, hata makabila ni hivyo hivyo. Ukweli ni kwamba watu wa Mara hawapendani kwa misingi hiyo hasa kutokana uhasama wa koo na koo au kabila na kabila.
 
Mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa ambayo imebahatika kutoa viongozi wengi katika serikali zote za kuanzia muasisi wa taifa hili.Lakini ni kati ya mikoa ambayo maendeleo yake yako nyuma sana, ukifatilia kiundani ni kuwa hata viongozi ambao walipewa nyadhifa mbalimbali wao kwa wao hawaelewani bila kujali itikadi zao za vyama.Kwa mfano Wasira na Jaji Warioba ni watu wasiopikika chungu kimoja japo wote wako ccm. Mwanasheria mkuu aliyestafu Jaji Welema na Mbunge Nimrod Mkono na Pro ,Mhongo ni maadui na uhasama huu unatokana na masilahi,baada ya kuchaguliwa Mhongo kuwa waziri wa nishati kwa kushirikiana na Mwanasheria mkuu Jaji Welema walikata mirija ya ulaji ambayo Nimrod mkono alikuwa analipwa kwenye kampuni yake ya uwanasheria kutokana na lile sakata la Dowas.Mkono nae nae akaamua kuwalipua kwa kumpa documents Kafulila na kuwakomalia mbugeni na kusababisha Mhongo,Eriakim Maswe na Welema kupoteza nafasi.Ninachomaanisha hapa ni kuwa viongozi kutoka mkoa wa Mara bila kujali itikadi zao ni watu ambao hawawezi kukakaa meza moja na kuzungumzia matatizo ya Mara kwa sababu wao kwa wao hawapendani.Ni mji ambao hata miundombinu yake ni shida pamoja na kuwa na ziwa victoria lkn maji bado ni shida hasa kwa wakazi wa nje kidogo ya mji, Ukienda makao mkuu ya wilaya ya Serengeti mji wa Mugumu huwezi amini palivyo choka na wakati wako karibu na hifadhi. Wakuu wa kaya nao wameususa kuanzia awamu ya Jk na sasa JPM ndio hana hbr kabisa na mkoa wa Mara.Tupatiwe fursa hata viwanda vilivyokuwepo vifanye kazi pamoja na kuwa na chuo kikuu ,kwani chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere ni jina tu hakuna kinachoendelea.

Na ubabe pia umezidi!
 
Nimefanya kazi na watu wanaotokea Mara wengi wao kwa asili wana wivu sana na ni wafitini mno.
Usemacho nakuunga mkono kuna tasisi moja ya mkopo watumishi wake ni watu wa uko mara ukikaa nao wanavyopigana madogo wanafitiana mpaka kulogana, unabaki unashangaa hawa si wanatoka mkoa mmoja tatizo nini sasa unabaki unawashangaa tu.
 
Usemacho nakuunga mkono kuna tasisi moja ya mkopo watumishi wake ni watu wa uko mara ukikaa nao wanavyopigana madogo wanafitiana mpaka kulogana, unabaki unashangaa hawa si wanatoka mkoa mmoja tatizo nini sasa unabaki unawashangaa tu.
Hao watu kwa majungu hutawaweza ndo wanaoongoza kuuana kwa wivu
 
Maswi na Werema kwao ni Tarime na Mkono ni Butiama na sio Musoma vijijini.
Werema nilijua kwao ni Wegero/Kiagata huko msoma vijijini maana kuna mtu mmoja anaewafaham vizuri aliwahi kuniambia hivyo.

Maswi pia nilidhani kwao ni hapa maeneo ya Kinesi upande wa Musoma vijijini kabla hujavuta mto.

Hilo jimbo lilikua moja kabla hawajaligawanya na mimi nimezungumzia hilo.

Ahsante kwa taarifa.
 
Jiografia ya mkoa wa Mara kama ilivyo kwa mikoa ya Kagera,Kigoma,Mtwara,Lindi,Ruvuma na mingineyo ndio sababu ya kuwa nyuma kimaendeleo katika nyanja nyingi sana. Tabia hata huku jijini zinatofautiana mtu hadi mtu.
 
Back
Top Bottom