Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Na wala Mara sio wazubaifu kihivyo ila ni kama alivosema mchangiaji hapo juu,watu wengi wa Mara wakifanikiwa kidogo tu wanakimbilia kuwekeza Mwanza na mkoa wao unabaki bila fursa za mzunguko wa fedha siku hadi siku. Inasikitisha sana
 
Wakurya wana wivu na majungu sana.

Wewe sasa una matatizo yako
Hauwafahamu wakurya
Hizo ni fikra zako tu ndogo ndizo zinazokutuma kufikiri hivyo

Unaposema wakurya ni kama useme wachaga
Humo ndani yake kuna Wamarangu, wakibosho, wamachame n.k
na wakurya nao wapo hivyo hivyo
Humo ndani kuna wanchari, warenchoka, wakira, wanyamongo n.k

Sasa usipende sana ku generalize
Coz tabia za wamachame sio tabia za wachaga wote
Hivyo jifunze
 
Werema nilijua kwao ni Wegero/Kiagata huko msoma vijijini maana kuna mtu mmoja anaewafaham vizuri aliwahi kuniambia hivyo.

Maswi pia nilidhani kwao ni hapa maeneo ya Kinesi upande wa Musoma vijijini kabla hujavuta mto.

Hilo jimbo lilikua moja kabla hawajaligawanya na mimi nimezungumzia hilo.

Ahsante kwa taarifa.
Wewe haujui kitu, unasema kinesi ni musoma vijijini??
 
Wewe unaijua Mara vzuri? Werema na Mkono watokeee Musoma Vijijin? Rudi kaangalie vzur Wilaya za Mkoa wa Mara.
Mleta mada umesahau kuwaambia hao Jamaa zako wa Mara wanabana sana Ulaji wapewapo nafasi kubwa mwisho wa siku wanalipuliwa kirahisi mno. Mbadilike na msome tabia ya mchezo mahala pa kazi.
Mjinga akinyamaza uhesabiwa hekima, jimbo la Musoma vijijini sasa hivi limegawanywa, mkono amebaki jimbo la Butiama wilaya ya Butiama na Mkono yupo jimbo la Musoma vijijini.

Kama kitu hujui kaa kimya au nyamaza kuliko kujicholesha na kuumbuliwa kama hivi.
 
Na wala Mara sio wazubaifu kihivyo ila ni kama alivosema mchangiaji hapo juu,watu wengi wa Mara wakifanikiwa kidogo tu wanakimbilia kuwekeza Mwanza na mkoa wao unabaki bila fursa za mzunguko wa fedha siku hadi siku. Inasikitisha sana
Msizungushe maneno mchawi wa maendeleo ya mkoa wa Mara ni Nyerere.

Mkoa wa Mara watu walimuogopa Nyerere hakuna mtu aliyetayari awekeze kitu halafu wewe uje kutaifisha unamuita muhujumu uchumi.

Kuna makabila mengine mtu hata awe na pesa kiasi gani hajengi kwao na ukijenga tu wanakuroga labda ujenge nyumba tu ya kawaida ya kufikia inayofanana na zao.

Kwa hili Wachaga wameshinda ni kabila namba moja Tanzania mtu anajisikia fahari kwenda mapumziko kijijini kwake.
 
Ushirikina nao umekuwa mwingi Sana, hata nyumba za kuishi no hovyo, unakuta mtu anaishi Dar (mfano) ananyumba nzuri Sana na maisha mazuri sana, lakini anakotokea kijijini kwao ni aibu, nyumba ya maana hakuna, anaogopa kujenga kwa kuogopa kurogwa yeye mwenyewe ama wazazi wake kisa tu eti watajidai akienda kusalimia anakaa mjini, anakwenda kila siku kusalimia kijijini. Wana-Mara tubadilike, tuache wivu wa kijinga ili Mara yetu Ibadilike.
 
1. Wepesi wa kuamini na kutenda mambo ya ushirikina hata kwa mambo madogo madogo.
2. Wivu wa kijinga uliopitiliza. Mfano ukimzidi tu hatua moja mbele ktkt nyanja yoyote, basi vitimbi na visa vitaanza huku wakikusindikiza na uchawi/ushirikina.
3. Majungu mengi haswa kabila la wajita ambapo kwa jambo lolote utakalofanya la kimaendeleo lazima ufitiniwe kwa uwingi wa majungu.
4. Wengi wao bado sana wako kwenye primitive life- kidogo wanaojitahidi kwa uchakalikaji ni "Wakurya".
 
Kabisa mkuu, yaani hadi inatia hasira kweli, watu hadi wanaogopa kwenda kwao, wa wakienda kwao kusalimia wanaingia usiku, na siku ya kuondoka ni hivyo hivyo! Shem on us Mara people.
 
Msizungushe maneno mchawi wa maendeleo ya mkoa wa Mara ni Nyerere.

Mkoa wa Mara watu walimuogopa Nyerere hakuna mtu aliyetayari awekeze kitu halafu wewe uje kutaifisha unamuita muhujumu uchumi.

Kuna makabila mengine mtu hata awe na pesa kiasi gani hajengi kwao na ukijenga tu wanakuroga labda ujenge nyumba tu ya kawaida ya kufikia inayofanana na zao.

Kwa hili Wachaga wameshinda ni kabila namba moja Tanzania mtu anajisikia fahari kwenda mapumziko kijijini kwake.

Kwa sasa Nyerere haishi na wala si kiongozi tena hivyo hiyo point yako ya kwanza bado haina mashiko.
Mchawi akikutaka atakufuata hata ukiwa dar ndugu Matola,tuondokane na dhana za kichawi linapokuja suala la maendeleo ya mkoa wa Mara. Kilimanjaro na wachagga ni exceptional case linapokuja suala la kuuendeleza mkoa wao na vijiji wanavyotoka,mbali na hao mikoa mingi tu dhana ya kuendeleza makwetu tunafanana kwa asilimia kubwa tu
 
Swala la majungu na ukabila ni tabia ya kibinadamu, hata watu wa kanda zengine ni hivyo hivyo mbona wahaya pia wanabaguana, kaskazini je
 
Kabisa mkuu, yaani hadi inatia hasira kweli, watu hadi wanaogopa kwenda kwao, wa wakienda kwao kusalimia wanaingia usiku, na siku ya kuondoka ni hivyo hivyo! Shem on us Mara people.
Wale watu ni development haters. Wao kwa wao kurogana ni nje nje. Wageni wanaofanya kazi kule wanapata shida sana ktk uwekezaji sababu ya ushirikina na majungu/fitna.
 
Mimi pia nawakubali Sana watu wa mara. Sio double standard, nikikumbuka watu kama Mwalimu Nyerere, Profesa Sarungi, jenerali David Musuguri , Mzee Joseph Butiku, Mzee warioba. hakuna mfano kama viongozi hawa. Hembu jiulize Tangu uhuru mpaka miaka ya mid 90's utawala wa nchi ulikua mikononi mwa watu hawa, Lakini hawakupendelea kwao, kwao kwa kawaida tuu.......
 
Nawashukuru kwa michango yenu ,ila kuna mambo nataka niyaweke sawa.Welema anatokea Kijiji kinaitwa kongoto wilaya ya Butiama,Mhongo anatokea Majita ,Mkono anatotokea Butiama na Eriakimu Maswi kwao ni tarime,Uliyeongelewa wakurya utakuwa hujafanya utafiti vzr,Hakuna kabila lenye husuda kwa mkoa wa Mara kama Wajita yego jaji, Suala la watu kujenga kwao inatengemeana ila siyo mambo ya kurongwa .Nenda kwao Jaji Warioba huwezi amini kuwa ndipo anatokea,Lkn kwao mke wake moshi mambo yako vzr,Hivyo hivyo kwao welema alijenga msonge tena baada ya wazee kukomalia kuwa huwezi kufikia kwenye nyumba mama yake mzazi,Kwahiyo suala la kujenga hata wanawake tunaoa wanaweza kuchangia mwanaume kushindwa kuwekeza nyumbani.
 
Hapo Mnaongelea Musoma na vitongoji vyake, Tarime pako poa sana, ni mji ambao mgeni hata akifika hatamani kuondoka, fursa zipo kibao, na Yule aliyesema Wakurya wana husuda na fitina hawajui vizuri, labda anahisi Mkoa wote wa Mara wenyeji ni Wakurya, Musoma nature ya eneo ndio inapafanya pawe nyuma, ni peninsula, barabara ya kutoka na kuingia ni hiyo hiyo moja, hakuna shughuli yoyote ya maendeleo mbali na uvuvi ambao ni wa kusuasua ukilinganisha na maeneo mengine kama Bunda na Mwanza, hali ya hawa na ardhi sio nzuri kwa kilimo, wenyeji wake sio wafugaji, pale kupata maendeleo ni ngumu sana, ni bora hata Makao Makuu ya Mkoa wangepeleka Tarime
 
Ni watu wa ajabu !! Sana sitaman kuja kukaa tena hukoo nilikooma
 
Nimefanya kazi na watu wanaotokea Mara wengi wao kwa asili wana wivu sana na ni wafitini mno.
Unachokisema kama kina ukweli ndani yakeeee hawa watu kuna kitu sio bure......binafsi sijawahi kufika katika huo mkoa lakini nadhani huo mkoa utakuwa ni miongoni mwa mikoa maskini
 
Kwa kifupi mkoa wa mara wamekopa/wanakopa tabia za wakenya
 
Back
Top Bottom