Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Shida watu wa Mkoa wa Mara ni wabinafsi hata wao kwa wao hawapendi kuona mwenzao kapata. Kingine kinachotuumiza ni UCHADEMA mwiiiiingi. Unakuta mtu yuko CCM lakini akiona anayegombea CCM sio kabila lake anakisaliti chama na kukisaidia chama cha upinzani. Naomba tusiwalaumu JK wala JPM, toka enzi za Nyerere marais wetu wamejitahidi sana kutupa nafasi lakini hatukujua kuzitumia. Matokeo yake baadhi ya wateuliwa wakishapata nafasi wanahamia Dodoma na kula maisha na Toto's. Sidhani kama Rais atakuteua then akuelekeze nini cha kufanya. Mwisho naomba tusaidiane kutaja viongozi waliotoka mkoa wa Mara ili tujue ujinga ni wetu na sio wa wale wanaotuteua. Nitakao wasahau mtanikumbusha. 1. Dr Wanyancha. N.waziri wa ujenzi/Mjumbe wa Bodi ya Tanapa. 2. Dr Mwita N.waziri Tamisemi. 3. PR Muhongo. 4. Dr. Sarungi yeye alichofanya ni kuoa Mzungu 5. Wasira. 6.Jaji Warioba 7. Dr Kebwe.8. Mama Kabaka 9. Kamanda Siro. 10. Jaji Werema. 11. Jerenerali Kyaro12. Kichele TRA na wengine wengi. . Tena hao wa mkoa wa Mara ni wasomi tupu.
 
Usimsahau NGULI WA RASILIMALI WATU Dr.Fred Mwita alikuwa ZANTEL,VODACOM,SBL sasa AGAKHAN,Mkurugenzi wa TBC Dr.Ayub Rioba na Mfanyabiashara Gachuma,La Kairo Lameck Airo bila kumsahau mwenye mabasi ya Zakaria
 
Mada yako ilikuwa nzuri umeharibu ulipoanza kuwajadili watu ,badala ya maendeleo ulivyotanabaisha..

Kwa kifupi tu Mchawi wa Nchi hii sio Mara peke yake yaani Tanzania nzima Mchawi ni CCM..
Mara kilichoirudisha nyuma ni mapigano na wizi wa kijinga wa mifugo wala sio CCM. Mbona Serengeti na Tarime kuna CHADEMA lakini mambo ni yaleyale. Mara tunashida ya kifikra. Nenda hata kwenye Halmashauri zetu kukiwa na mtumishi mzawa akianza kujenga tu wanaanza kumpambanisha. Akijenga mgeni sawa. Na Mara wanaojenga majengo ya kifahali ni watu toka nje. In short hatupendani. Ukabila na milangi vina nafasi kubwa sana. Tofauti na wahaya. Nenda mtu tofauti uone kama hujaitwa Mnyamahanga.
 
Usemacho nakuunga mkono kuna tasisi moja ya mkopo watumishi wake ni watu wa uko mara ukikaa nao wanavyopigana madogo wanafitiana mpaka kulogana, unabaki unashangaa hawa si wanatoka mkoa mmoja tatizo nini sasa unabaki unawashangaa tu.
Taasisi moja ndo nini. Sema FinCer. Mbona inajulikana vizuriiiiiiiiiiii
 
Bila kusahau watu wengi wa Mara wapo jeshini na wanalipwa vzr kdg ila maendeleo yao yanaishia kwenye kuonesha eti wana hasira kaliii...

Pia ile kukosa mchanganyiko na watu wa makabira mengine ni tatizo pia. Utakuta full kuongea milugha yao tuuu na kunywa pombe za kienyeji. Mziki wenyewe unaokesha ni local songs!!

Siogopi kufanya kazi huko ila sitasahau jamaa yetu mmoja alidungwa kisu na kufa kisa alikuwa anamdai mkulya pesa yake!! Sasa nani atawekeza kwenye mazingira haya ya uhasama na ujima? Poor Mara n kudos Tarime wanajitahidi!
 
umeandika vzr ila Maswi sio wa musoma vijijini
 


Popoma kama wewe huwezi kuelewa hii ni nini maana yake

Tatizo la mkoa wa Mara ni Nyerere fullstop. Hata wakati wa vita watu wanajiandikisha wakapigane vita ya Uganda aliwapunguza idadi ili kuwe na mgawanyo nchi nzima.

Mkumbuke hata Nimrod Mkono na utajili wake wote pale Busegwe alikuwa anakaa kwa baba yake mpaka alipokufa Nyerere ndio amehama kwao amejenga kasri lake na amejenga mashule na kuikabidhi serikali, Mkono angekuwa anatoka mkoa mwingine yale mashule angeyafanya mradi wake private au angejenga mahotel Musoma mjini.

No research no right to speak
 
Unaposema poor Mara, kudos Tarime unakuwa huna tofauti yoyote , kwani Tarime ipo Tabora?
 
Unaposema poor Mara, kudos Tarime unakuwa huna tofauti yoyote na taahira, kwani Tarime ipo Tabora?
Matola jifunze kupokea changamoto in positive way, hii mihasira isiyo na faida ndiyo inawaangusha wana Mara n u are proving it here!!
 
Maendeleo ya eneo lolote yana msingi wake kwa wananchi wa kawaida na wala siyo viongozi wakubwa wa kitaifa.
Utamaduni wa jamii husika (fikra na vitendo) vinahusika sana katika maendeleo, elimu za darasani na nafasi za uongozi ni catalysts tu. Kama hakuna reaction hata uweke calalyst bado hutaona badiliko haraka.
Jamii zinatakiwa kuwa na watu wanye upeo mpana , hekima, wasio na mihemko au sifa za kilimbukeni za kibinafsi, ubabe ili kupata maendeleo endelevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…