Nani aliyewadanganya Watanzania kuwa Mitazamo ya hawa Wafuatao ndiyo Mitazamo ya Watanzania wote na wako sahihi?

Nani aliyewadanganya Watanzania kuwa Mitazamo ya hawa Wafuatao ndiyo Mitazamo ya Watanzania wote na wako sahihi?

1. Profesa Shivji
2. Tundu Lissu
3. Freeman Mbowe
4. Dk. Wilbroad Slaa
5. Harold Sungusia
6. Godbless Lema
7. Dk. Charles Kitima

GENTAMYCINE nimekaa tayari kabisa kusubiria mirejesho yenu huku nikiendelea kuwaonea Huruma Watanzania wengi ( siyo Wote ) wenye Uwezo mdogo sana wa Kufikiri na Akili.
nani alikuroga uamini kuwa mitazamo ya wafuatao ni mtazamo wa watanzania?

1 - Kitila Mkumbo
2-Makame mbarawa
3-Kibajaji
4-Rostam Aziz
5-etc
na wapuuzi wengine kama stivi nyerere, maulid Kitenge, baba levo na wengine wengi wa sampuli yao?
 
Watu Wanafiki huwa na Umuhimu Kimaendeleo? Bado Tanzania kuna Wapumbavu wengi sana.
Hujui mnafiki wewe....
Hujui watu wanashauri nini...
Wasome vizuri, kila mtu anapenda maendeleo, wahahofia yasijetokea kama yaliyotokea nyuma..Mikataba hii
 
1. Profesa Shivji
2. Tundu Lissu
3. Freeman Mbowe
4. Dk. Wilbroad Slaa
5. Harold Sungusia
6. Godbless Lema
7. Dk. Charles Kitima

GENTAMYCINE nimekaa tayari kabisa kusubiria mirejesho yenu huku nikiendelea kuwaonea Huruma Watanzania wengi ( siyo Wote ) wenye Uwezo mdogo sana wa Kufikiri na Akili.
Naunga mkono hoja.

Ukimtoa Lisu,Mbowe,Lema hao ni Wanasiasa wanaotumia Hilo la Bandari kutafuta political advantage so ni WA kupuuuzwa.

The rest ni ujamaa mentality ambao wamekulia kwenye keki ya Taifa hawajui shida za kutafuta na wenye hofu ya mabadiliko sawa na Jiwe aliyetaka matajiri wawe maskini so ni WA kupuuzwa hawana jipya.
 
Naunga mkono.

Ukimtoa Lisu,Mbowe,Lema hao ni Wanasiasa wanaotumia Hilo la Bandari kutafuta political advantage so ni WA kupuuuzwa.

The rest ni ujamaa mentality ambao wamekulia kwenye keki ya Taifa hawajui shida za kutafuta na wenye hofu ya mabadiliko sawa na Jiwe aliyetaka matajiri wawe maskini so ni WA kupuuzwa hawana jipya.
Chifu mangungo alkua na mentality Yako🤣🤣🤣
 
Kuna baadhi ya watu hapo kati ya uliowataja,walifanya vizuri sana katika kuchanganua mambo na kuyaweka wazi kwa wananchi,ndiyo maana wanaaminiwa mpaka sasa.
Mfano mmojawapo ni Profesa Shivji alifanya vizuri sana kwenye uchanganuaji wa vifungu vya katiba wakati ule Kuna ule mchakato wa katiba mpya chini ya jaji Warioba,halafu mtu kama Slaa alifanya vizuri sana alipokuwa mgombea wa uraisi wa URT kwa tiketi ya CHADEMA, kwa hiyo wewe GENTAMYCIN usikurupuke na Uzi wa wivu,hao watu wana nafasi kubwa ya kusikilizwa na kiaminiwa na jamii.(halafu nakufahamu Huwa ukishindwa hoja unarusha matusi)
 
1. Profesa Shivji
2. Tundu Lissu
3. Freeman Mbowe
4. Dk. Wilbroad Slaa
5. Harold Sungusia
6. Godbless Lema
7. Dk. Charles Kitima

GENTAMYCINE nimekaa tayari kabisa kusubiria mirejesho yenu huku nikiendelea kuwaonea Huruma Watanzania wengi ( siyo Wote ) wenye Uwezo mdogo sana wa Kufikiri na Akili.
Fake news
 
Chifu mangungo alkua na mentality Yako🤣🤣🤣
Ndivyo mlidanganywa na Babu yenu Mjamaa Nyerere si ndio?

Bora Mangungo kuliko huyo Babu yenu ambae alikuwa anatumia rasilimali watu na Fedha za Tanzania kuwapa Nchi jirani huku nyie akiwacha na umaskini na vilaka bila Elimu na ndio matokeo yake haya Sasa mumejaa upumbavu.
 
Umepiga kwenye mshono ,huo ni ukondoo kuamini mtu fulani kauli yake na mawazo yake ndio bora kabisa kuliko wengine.
 
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO), je makubaliano yanaweza kusema tunakupa bandari zote alafu mkataba ukasema tunakupa bandari moja tu?

Si spika Tulia, waziri mkuu wala Rais mwenyewe wala wale vikaragosi wengine wanaotumwa kutetea mkataba aliyeweza kujibu swali hili.
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Uwezo na ujasiri walionao katika kutetea wanacho kiamini,hata kuhatarisha maisha yao.
So,why nikuamini wewe uliyejificha nyuma ya fake Id hapa JF ukiogopa kutoa mawazo yako kwa real name yako?
 
Weee siku nyingi nishasema akili zako haziko sawa and sijui kwanini wanakupa attention kwa thread zako za ovyo
1. Profesa Shivji
2. Tundu Lissu
3. Freeman Mbowe
4. Dk. Wilbroad Slaa
5. Harold Sungusia
6. Godbless Lema
7. Dk. Charles Kitima

GENTAMYCINE nimekaa tayari kabisa kusubiria mirejesho yenu huku nikiendelea kuwaonea Huruma Watanzania wengi ( siyo Wote ) wenye Uwezo mdogo sana wa Kufikiri na Ak
 
Ni kweli lazima tupate msaada was wabobevu was Sheria lakini ni muhimu tuangalie background zao tupime umahili wao wa Sheria umesaidia nini katika nchi hii?
Kuna mmoja hapo alikuwa Mkufunzi je, ametuzalishia kizazi gani cha manguli wa Sheria nchini? au ndiyo wale waliokuwa wanajinadi kwa kwa kupata A na kuzuia asitokee MTU wa kupata A nchini? Au ni miongoni ya Walimu na wakufunzi ambao wamerithi kufundisha wanafunzi kwa kutoa maswali ambayo mwanafunzi hawezi kuelewa ili afeli?

Hivi hawa siyo miongoni mwa wabobevu waliopewa kazi ya kufanya utafiti ili migogoro ya Ardhi iishe nchini lakini badala yake wakaishia kupiga pesa na kuacha matatizo ya Ardhi yaendelee mpaka leo?

Pamoja na kwamba hawa jamaa hawaaminiki lakini hoja hii ya mkataba tunahitaji utulivu na utafiti wa kina ili kama kuna mabaya yaondolewe na kama kuna mazuri yaendelezwe kwa manufaa ya nchi.
 
Back
Top Bottom