Baadhi ya watanzania,kazi yao kulalamika,fursa za kupata kipato,zikija anabakia kulalamika.Wageni wanazitumia hizo fursa,mpaka wao wanashangaa wanasema watanzania ni watu wa ajabu,wakati nchi ina fursa nyingi za kufuatilia ofisi zinazohusika,wao ni kulalamika.Leo mgeni,anakuja Tanzania anazifuatilia fursa,na kuzifanyia kazi.Utamkuta mgeni ndio anasafirisha bidhaa kadhaa nje,madini,mazao kama katani,leo katani inakwenda falme za kiarabu,wamegundua katani ya Tanzania ndio nzuri,kutengeneza jipsum,wasafirishaji wa hiyo katani,ni wageni sio watanzania,sisi ni kulalamika tu,kwa jambo hata mtu hana ushahidi nalo.