Nani amewapa TFS idhini ya Kujenga Makao Makuu yao Mwanza wakati Makao Makuu ya Nchi ni Dodoma?

Nani amewapa TFS idhini ya Kujenga Makao Makuu yao Mwanza wakati Makao Makuu ya Nchi ni Dodoma?

Moja kwa moja kwenye mada,

Site tunatambua kwamba Makao Makuu ya Nchi na Serikali ni Dodoma ambapo ndipo kunapaswa kujengwa Makao Makuu ya taasisi zote za Kiserikali ikiwemo Ikulu.

Kwamba toka Jobo Ndugai ametolewa kwenye kiti Dodoma imekosa msemaji wake au?

Swali nani katoa ruhusa kwa TFS na Wizara ya Maliasili kujenga Makao Makuu yao Mkoa wa Mwanza Kwa kisingizio cha deforestation Kanda ya Ziwa?

Huo ni upuuzi na utoto kuleta hoja ya kijinga na kukiuka sheria ya Nchi.Hivi Kati ya Dodoma na Kanda ya Kati kiujumla ukilinganisha na Kanda ya Ziwa wapi kunahitaji nguvu kubwa ya kupanda miti Ili kuboresha mazingira?

Waziri husika achana kabisa na huu mpango vinginevyo inakuwa haina maana ya kuwa na Makao Makuu ya Nchi na hivyo tuanze kusambaza taasisi za Kiserikali kikanda na kimkoa..

Mh.Waziri Mkuu zuia huu ujinga. Ingewezekana na TPA wangehamia Dodoma ila hakuna Bahari.👇

View attachment 2302979
Wakati makao makuu ya TANAPA yanajengwa Arusha mbona hakuandika huu utumbo wako??Acha double standard hii nchi ya watu wote hata wanakanda ya ziwa.Sasa inajengwa mwanza jinyonge.
 
1659000488109.png


Makao Makuu ya TACAIDS yako Mkoa gani
 
Mhuu hili nalo wazo na ni uamuzi ili wawafunze wasukuma kutokukata miti kufukuza mbung'o. Wasigeuze nchi nzima kuwa kama shinyanga.
 
Makao Makuu ya Mabenki yote yatakuwa DAR..mtalia sana wagogo
 
Ingetakiwa iwe Mpanda Katavi na chuo kiwehuko ...Mwanza ni Masamaki
 
Nataka nitofautiane na mawazo ya wengi,

Ni kweli utasikia kuwa makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania nayo wanachagizwa wahamie Dodoma.

Makao makuu ya TRC Shirika la Reli yawe Tabora maana ni njia panda kuu ya reli n.k hii itafanya hata keki ya taifa iwe inagawanywa vizuri katika maeneo mbalimbali ya nchi na kupunguza msongamano kati jiji la Dar es Salaam au mji wa Dodoma hivyo miji hiyo kupangika vizuri kwa kutokuwa mikubwa mno hivuo mipango ya miji kuweza kutekelezwa vizuri.

 
Taasisi ni tofauti na wizara, Sasa issue ya Dodoma ni kupiga Hela tu
 
Back
Top Bottom