Nani ana gharama zaidi? Fast jet ni shs 334,000-466,000 na Airtanzania ni shs 324,000- 664,000 kwenda Mwanza na kurudi

Attachments

  • fastjet.PNG
    fastjet.PNG
    40.8 KB · Views: 38
  • fastjet2.PNG
    fastjet2.PNG
    13.7 KB · Views: 40
Kasemaje?
Kasema kwamba wanapata training kwanza for only one month katika ruti fupii kuwawekaa Sharp wafanyakazi wake pia kucheck mifumo pia chombo kizooee huwezi kufika moja kwa moja ukaanza route ndefu na hiyo ipo applicable kwa mashirika yote
 
Air Tanzania ina unafuu kubwa kuliko fastjet. (1) Fastjet ukichelewa reporting masaa mawili kabla ndege haijaondoka imekula kwako. AirTanzania hata ibaki dakika tano utapanda ndege. (2) Air Tanzania kama bahati mbaya hukusafiri bado tiketi yako itatumika kwa muda wa mwezi mzima kinyume na fastjet kama hukusafiri kwa tarehe uliyopanga imekula kwako. (3 Fast jet kama kwa bahati mbaya ndege haikufanya safari hakuna huduma yeyote unayopewa kama msafiri tofauti na Air Tanzania. (4) Fasjet hakuna huduma ya viburudisho unayopewa badala kila kitu ni hela. Niliwahi kuuziwa korosho kwa bei mbaya lakini Air Tanzania kila msafiri anapewa huduma ya viburudisho. (5) Jana nimefanya booking ya safari yangu Mwanza - Dar 10/8/2018 na kurudi 15/8/2018. Gharama ya Air Tanzania ni Tshs.344,000 lakini gharama ya Fastjet ni Tshs.384,000. Je wapi kuna unafuu. Nawashauri tutumie chetu yenye bei nafuu.
 
Nauli inategemea factors nyingi sio kama daladala kuna low Na high season , exchange rate variation nk huwezi weka fixed specific

Bei elekezi inayotolewa na AIR TANZANIA wanamuelekeza nani, FASTJET?
 
Mkuu nauli za ndege zinategemea unasafiri lini na hii sio kwa ATCL tu ni utaratibu wa usafiri wa anga. Ukitaka kusafiri leo ukanunua tiketi leo sio sawa na anaesafiri mwezi ujao akakata tiketi leo.

Bei elekezi sio kitu cha ajabu kwasababu huduma inatofautiana. Hivi Fastjet ina classes(first,business,economy)?

Okay nakuelewa huwezi kuweka bei kwa vile bei ya jana ni tofauti na ya kesho na ya juzi na kesho kutwa.

Kwa hiyo, hiyo BEI ELEKEZI ni ya kesho, ya juzi, ya kesho kutwa, ya leo ama ya jana?
 
Bei elekezi ni 'starting from' yaani mfano dar-mwanza KUANZIA tzs 250,000 hii ukifanya booking mapema ndio bei ya chini utapata ila ukienda leo unataka kusafiri leo bei itakuwa juu zaidi.
Mfano mwingine kwenye magari utakuta mfano toyota land cruiser starting from $45,000 hii ni kwa base model sio kwa full loaded model.
 
Sio kweli, BEI ELEKEZI haimaanishi “bei ya kuanzia.”

BEI ELEKEZI inatolewa na mamlaka za uratibu na udhibiti wa biashara ili kuelekeza bei inayotaliwa kutumika kwa kila mfanyabiashara. Ukienda chini yake ni kosa na ukienda juu ni kosa! TPDC haiwezi kutoa bei elekezi ya diesel halafu wewe ukauza kwa double the rate ukasema eti bei yao ni ya kuanzia, hutabaki salama.

Na ndio maana BEI ELEKEZI iliyotolewa juzi na SUMATRA kwa mabasi, kwa mfano, ilitoa bei ya kiti cha kawaida, cha semi-luxury, na pia full premium seats. Which proves that BEI ELEKEZI sio bei ya kuanzia.

Wapanda ndege wengi ni watu wa middle class and higher, watu wasomi, hawataki mambo yasiyoingia akilini.

ATCL watuambie bei inaanzia laki kadhaa, sio kutuambia bei elekezi na kificha ficha gharama zao. BEI ELEKEZI inayotolewa na ATCL wanamuelekeza nani, RWANDAIR?
 
Kwahio wewe na usomi wako ulishindwa kuelewa wanamaanisha nini walipoweka hizo bei? Na umesisitiza abiria wa ndege ni wasomi na middle class ila hawajui taratibu za bei za ndege?
Hio bei elekezi ATCL wameweka wao sio ya Sumatra. Hata mimi kwenye biashara yangu naweza kuweka bei elekezi yangu kwa kuzingatia gharama zangu.
 
Kwenye biashara yako unapobandika BEI ELEKEZI unamuelekeza nani?
 
Back
Top Bottom