Nani anaestahili kuchukua nafasi ya IGP kumrithi Sirro endapo mabadiliko yakitokea?

IGP anatoka pemba na unguja mama anataka Zanzibar ikalie hicho cheo maana wamekimis mda mrefu
 
Sirro tangia samia awe Raisi amekosa sana busara hata u Igp umemshinda nikikumbuka jinsi alivokuwa ana mtetemekea bashite nashangaa kweli kweli
Bashite makonda alikuwa akimtesa sana, sasa Dua la kuwabambikia kesi wapinzani na Dua la kuitesa familia ya Hamza kuwakamata hovyo watu wasiohusika ndilo linamtafuna IGP
 
Kuwabambikia kesi wapinzani kuwakamata familia ya Hamza ndilo kosa litamvua cheo IGP
 
Apelekwe Jenerali wa JWTZ akaongoze hao raia si unaona Magereza hamna manung'uniko tena
 
Ataridhia kutoka kwa nani? Kwamba IGP kaomba kujiudhuru? Acha roho ya kishetani ya kuombea mabaya watu muda wote. Sometimes try to think positively. By the way umeshapata salary slip zako?
 
Kwanza IGP, makamishina wote na ma-RPC wote wastaafishwe kwa manufaa ya umma. Pili achukuliwe mjeda mmoja aliyesomea sheria ateuliwe kuwa IGP. Halafu baadhi ya polisi waliosomea sheria na utawala wapandishwe vyeo wawe makamishina na ma-RPC.
Naunga mkono kwa 100%
 
Hicho cheo apewe askari kutoka JWTZ. Hawa policcm hamna kitu wanaweza.
 
Ataridhia kutoka kwa nani? Kwamba IGP kaomba kujiudhuru? Acha roho ya kishetani ya kuombea mabaya watu muda wote. Sometimes try to think positively. By the way umeshapata salary slip zako?
Soma maoni ya watu mitandaoni ndio ujue watu wanataka nini.
 
Ataridhia kutoka kwa nani? Kwamba IGP kaomba kujiudhuru? Acha roho ya kishetani ya kuombea mabaya watu muda wote. Sometimes try to think positively. By the way umeshapata salary slip zako?
Wewe utakuwa mnufaika chawa wake maana umejitoa fahamu zote mpaka huoni kuwa IGP amejaa mapungufu sasa
 
Wewe utakuwa mnufaika chawa wake maana umejitoa fahamu zote mpaka huoni kuwa IGP amejaa mapungufu sasa
Ungelikuwa wewe ni IGP yapi ungefanya. Tatizo la sisi binadamu ni kujiona wakamilifu, tusio na mapungufu hata chembe huku tukiwaona wengine hawafai. Hesabu mapungufu yako kwanza kabla hujaangalia ya mwingine. Ikibidi angalia mapungufu katika familia na ukoo wako, zaidi jitathmini kama umeleta mabadiliko chanya.
 
Askari mmoja kutoka Jeshi la wananchi
 
Adadi Rajabu au wamrejeshe Saidi Mwema
 
Adadi Rajabu au wamrejeshe Saidi Mwema
Watu mnasahau haraka Sana
Kipindi Cha said mwema si ndio akina zombe walikuwa wanauwa wafanyabiashara, mwangosi alipigwa bomu na Askari, maandamano ya chadema kule Arusha n.k
Kifupi polisi wote wanafanana
 
Wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…