Nani anaestahili kuchukua nafasi ya IGP kumrithi Sirro endapo mabadiliko yakitokea?

Kamanda Heche angefaa sana hiyo nafasi akishirkiana kwa karibu na kamanda Lema.
 
Watu mnasahau haraka Sana
Kipindi Cha said mwema si ndio akina zombe walikuwa wanauwa wafanyabiashara, mwangosi alipigwa bomu na Askari, maandamano ya chadema kule Arusha n.k
Kifupi polisi wote wanafanana
Kipindi salama nafikiri ni kipindi cha Ernest Mangu ila na yeye ndipo lilipoibuka kundi la Al shabab kula Tanga na Kibiti.
 
Bashite makonda alikuwa akimtesa sana, sasa Dua la kuwabambikia kesi wapinzani na Dua la kuitesa familia ya Hamza kuwakamata hovyo watu wasiohusika ndilo linamtafuna IGP
Acha tu limtafune maana sasa hivi hekima na busara zimempita kushoto
 
Kipindi salama nafikiri ni kipindi cha Ernest Mangu ila na yeye ndipo lilipoibuka kundi la Al shabab kula Tanga na Kibiti.
Yes, hata kipindi Cha Mangu yalikuwa yaleyale tu
Tena katika IGP waliokuwa wakionekana dhaifu basi Ni Mangu, maana kipindi chake ndio ulianza uvamizi wa vituo vya polisi.
Polisi wwlivamiwa vituoni, waliuliwa na kuporwa bunduki.
Moja ya tukio lisilosahaulika ni lile la kituo kikubwa cha Ukonga Stakishari
 
John John Mnyika naona atafaa sana. Ile kauli yake ya ushujaa aliyo mwambia Mkwere kuwa dhaifu ina onyesha utimamu na Ushujaa wake. Mnyika na Jamhuri ya JF OYEEEEEE.
 
Ni muda muafaka wa kuwa na IGP mwana mama.
Kumradhi kinababa makamanda wametamalaki sana katika majeshi yetu na tunawashukuru kwa mchango wao, ila kwa sasa ni muda muafaka wa kuwapisha kina mama kwenye sekta hizi nyeti za taifa.
Mama tuanze na IGP mwanamke.
Then utuletee mkuu wa TISS mwanamke, kisha Chief of diffence mwanamke, na ikikupendeza magereza, JKT,nk....
Wanawake wanauwezo zaidi wa kuongoza hizi taasisi nyeti kama ulivyoonyesha njia.
Mamwavi Nkabasia (@Joeselasini) Tweeted:
Huyu kamanda awe IGP mnasemaje. Tena tutaandika historia ya kuwa na IGP wa kwanza mwanamke nchini. https://t.co/isHUUGYjIW
 
Camillus Wambura
 
Kuna Jamaa anaitwa Njeera Nadhani ni RPC Mtwara Jamaa ana utulivu sana anaweza..
 
 
Wewe ndiyo unastahiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…