Binadamu bwana! Tenda wema nenda zako hivi kweli hawa jamaa wana ujasili wa kumuona SIRO ni mbaya eti kwasababu vijana wake wamefanya maovu! Basi kama ndivyo tusiishie kwake.
Tume kama hizi ziundwe kuchunguza mauaji yote pamoja na mashambulio kadhaa bila kuliacha la Yule mbunge aliyekimbilia ughaibuni.,tume iundwe kupitia hali ya uchaguzi iliyowaweka madarakani.
Hakuna ubishi kwamba vitendo vya hao Askari wa Mtwara havikubaliki na wanastahili hatua Kali za kisheria lakini huwezi kuwalaumi maelfu ya Askari Kwa kosa ya Askari kumi.
Hivi jeshi lote linaweza Kuwa Baya? Leo wamezunguka kila Kona ili kuwalinda HAO viongozi wasafiri salama walale salama wanasema hali ni shwari kwasababu Kuna watu wamekesha kuandaa hali hiyo.
Mangapi hayafahamiki ambayo yamezuiwa na jeshi Hilo Baya na kama yangeachiwa nchi ingekuwa kama DRC CONGO au Msumbiji.?