Namfahamu, ni mzaliwa wa Singida. Ana postgraduate diploma ya mambo ya finance. Alikuwa miongoni mwa wanafunzi bora uahasibu Arusha akiwa anafanya advance diploma.
Siyo muongeaji kiasili ila ni mtu mwenye akili nyingi sana. Yeye ndiyo amekuwa mpangaji mkubwa na kiongozi muendesha wa Chadema kuanzia Arusha na hata kaskazini nzima. Amefanya kazi kubwa. LEMA mwenyewe amejiunga na CHADEMA akitokea NCCR akipokelewa na Golugwa. Golugwa siyo mtu mwenye kuweza kununuliwa wala kuwa na msimamo ya kuyumbiwa yumbiwa. Hivyo siyo rahisi kuachana na Chadema.
Kabla ya kuachana na ajira alikuwa anafanya na shirika moja liitwalo EANASO pale Arusha kama Chief Accountant wakati huo huo alifanya kama katibu wa Chadema Mkoa Arusha pia, kama katibu wa kanisa moja la TAG lililopo Mshono kule Arusha. Kazi zote hizo alizifaya kiufasaha. Asubhuhi kibaruani, muda wa Lunchi ofisini kwa chadema na jioni kanisani. Very smart and busy guy.
Ni mzuri sana kwenye mipango ya kiharakati. Siyo mtu mwenye kupenda sana madaraka wala kujionyesha. Hivyo basi Golugwa hajawahi kugombea ubunge, hajawahi kuweka ndani katika harakati zote za Chadema na wala kushitakiwa kisiasa. Hii ndiyo driving engineer ya chadema kwa sasa. Naweza kusema huyu ni mtu mwenye mshahsuri mkuu wa wakina LEMA.
Taifa lilipaswa kuwa na mikakati ya kuwafahamu watu kama hawa na kuwatumia kwa maendeleo ya taifa bila kujali itikadi zao.