Nani anaifahamu vema gari hii DISCOVERY 4. Naomba mnipe details

Nani anaifahamu vema gari hii DISCOVERY 4. Naomba mnipe details

Gari zuri kwa maana ya comfortability na drive feel, ni practical pia na ina utumiaji mzuri wa mafuta kwa large and heavy SUV kama ile.
Kitu ambacho si kizuri hapo ni maintenance costs, hasa discovery 4 kuliko hata 3. Ziko juu na asitokee mtu kukudanganya ni kawaida.
Okay. Gharama zipo eneo gani sasa ufundi au eneo la manunuzi ya spare?!

Hapo South Africa si kuna kiwanda so i guess spare si zinapatikana kwa urahisi hapo South Africa?
 
Kuna Uzi huku kuhusu hayo Magari mkuu . Gari nzuri sana sio haya Maprado yamejazana huku mjini kama lst mpaka unafungua gari ya mwenzako .
Ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hebu share hiyo link ya uzi nijionee mkuu.
 
Habari zenu wajumbe wa balaza hili tukufu la wapenda magari.

Mimi raia mwenzenu mnyenyekevu na Mzalendo nipo hapa mbele yenu kupata maoni, ufafanuzi, ujuzi, taarifa na maelezo ya kina juu ya gari hii aina ya Discovery 4.

Najua haya magari yanakuja na options tofauti kwa maana ya kuwa manual transmission na automatic transmission. Pia engine za ukubwa tofauti na fuel tofauti kwa maana ya diesel au petroleum. Lakini pia najua yanakuja kwa kutokea location tofauti kwa maana ya kutokea Ulaya yaani UK na kuna yanayotokea hapa bondeni kwa madiba yaani South Africa.

Hebu nifahamisheni zaidi enyi watukufu watalaamu na wapenda magari wenzangu. Napenda nifahamu zaidi kuhusu hii gari.

Naomba wazee wa suggestions msianze kujadili Discovery 3 maana ile siipendi ndio maana nimekuwa specific kuwa nataka Discovery 4 so please naomba wazee wa suggestions msianze kunichanganyia madawa taarifa za model tofauti na hii ya discovery 4.

Karibuni sana nawasubiria. View attachment 2608252View attachment 2608254View attachment 2608255View attachment 2608253
Mchukue mnyama huyo hutajuta
20230505_203813.jpg
 
Kama unapenda mbio chukua V8 petrol. Kama unapenda fuel efficient chukua ya diesel. Epuka kuchukua yenye air suspension kwani ni nzuri sana kama unatembea mawinguni ila ikizingua utaita maji mma unless uwe na milioni 3-6 ya matengenezo
 
Sjafanya price comparison- ningekuwa na hio pesa estimate ninge i substitue kwa toyota fortuner- mara nyingi huwasimshauri mtu achukue europian car kama gari yake ya kwanza / au kuichukua wakati kavunja kibubu chake chote.. au akaenda kununua ya bei rahisi/ ya mkononi. IMG_1504.jpeg
 
Hizi ni akili za kitoyota

Na akili zangu za kitoyota nisisitize ushauri wangu kwa mtoa mada maana hakutaja kujua watu wana akili gani ila facts kuhusu Disco 4.

Disocvery ni comfortable, practical na nzuri kuendesha na ina power ila ni sophisticated, complicated kama zilivyo gari nyingi za Ulaya. Atapambana na umeme, mziki wa air suspension, Electronic Parking brake yake inahitaji maintenance ya mara kwa mara n.k
Kama ana hela ya maintenance anunue. MAINTENANCE COSTS ni ghali, ziko juu (hii ni facts siyo maoni)
 
Okay. Gharama zipo eneo gani sasa ufundi au eneo la manunuzi ya spare?!

Hapo South Africa si kuna kiwanda so i guess spare si zinapatikana kwa urahisi hapo South Africa?

Spare utapata ila si rahisi. Baadhi ya issue ni
1. Electronic parking brake (lazima ufanye service mara kwa mara, la sivyo kuna siku ita jam)
2. Air suspension system (compressor, bags)
3. EGR Valves (diesel)
4. Umeme
 
Back
Top Bottom