Nani anaiongoza CCM?

Nani anaiongoza CCM?

Katika utaratibu wa kumsaidia mtu mlevi (kama aliyelewa madaraka) ujulikanao kama "Hatua 12). Hatua ya kwanza kabisa inamtaka mhusika kukubali kuwa ana tatizo na ya kuwa hakuweza kulikabili. NI hatua ya "kuown" your problem.

Hadi CCM itakapoanza hapa ndipo itaanza kweli kurudi kwenye misingi yake. NI vigumu sana kutoka denial kwenda acceptance. But slowly, watafika tu hata kwa kulazimishwa au kuanzishwa kauli.

"Hi, mimi ni mwana CCM, na Chama chetu kina matatizo!".

Wana CCM wote rudieni kauli hiyo hadi izame kwenye mitima yenu!
 
- "Mimi ni M-Tanzania na taifa letu lina matatizo",

- "Mimi ni M-Tanzania vyama vyetu vya siasa vina matatizo",

- "Mimi ni M-Tanzania sisi wananchi wa taifa hili tuna matatizo"

FMES!
 
Susuviri;410947]FMES: umeandika na kuainisha vyema hoja zako.
As a student of history nakataa kwani ukiangalia historia ya USA, walizaliwa katika mfumo wa multiparty demokrasia unaoheshimu property rights. Ni kweli walikuwa na utumwa na kadhalika lakini the environment that was created, the constitution that was written including its flexibility of the the Bills of Rights foresaw possbile changes in the future and came up with a way to address it, including an independent judiciary.
Sasa what I say is that we do not need to reinvent the wheel and to go through the same mistakes eti kwa sababu sisi ni taifa changa. We have many relevant examples that we can emulate
.

- Mkuu Susuviri, ninaheshimu sana hoja zako, lakini hapa kuna walakini kidogo kwa sababu katiba ya US imeundwa na matajiri na haikuwa ina heshimu masikini, wanawake walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura, na wasiokuwa na ardhi walikuwa hawaruhusiwi pia, sasa huwezi kusema kwamba hiii ilikuwa walizaliwa katika mfumo safi, hapana ila with time wameurkebsisha lakini bado una wafavor matajiri.

I seriously respect your view, lakini naomba nikuulize kwa nini umeng'ang'ania kubaki ndani ya chama wakati uongozi wa juu mzima wa CCM hivi sasa ni wanamtandao? They are ineffective na walikuwa part and parcel of one of the most corrupt and sleazy campaign in the history of Tanzania. Tatizo si kuwa wametenda kosa, tatizo ni kuwa hawataki kukiri na kutubu makosa yao. They think it is just fine. Na watu waadilifu kama nyie FMES, ndo mnawapa nguvu ya kusema kwamba eti bado wanaendelea kupigiwa kura. This has to stop. Mtu ukivuruga basi ni lazima utimuliwe, uende ukajirudi. That is the healthy way. So kama mzalendo, naomba uweke pembeni ushabiki wa chama na upigie kura upinzani kwani kama unaipenda CCM basi kitu pekee kitakachonusuru chama chako ni kama ikishindwa katika uchaguzi halali (isiyochafuliwa na vyombo vya usalama, rushwa n.k.). Otherwise itakuwa kama vyama vya kikomunisti huko Eastern Europe which were dissolved and faded into irrelevance.

- Labda ungeniuliza kwamba kwa nini ninaendelea kuwa M-Tanzania kwa sababu matatizo tuliyonayo Tanzania ni ya wa-Tanzania wote, sio ya CCM tu hata Upinzani kuna matatizo yale yale ya CCM, ndio maana rais wangu Dr. Slaa anakataa kutoa comment on Zitto na Dowans, kama Malecela alivyokataa kutoa comments za ufisadi ndani ya CCM, au?

Sasa mbona mkuki unauma upande mmoja tu?

Respect!

Asante mkuu kwa mjadala mzuri.

FMES!

Mimi ni mwana CCM, na sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa. Pamoja na kuwa mwanaCCM, siwezi kujivunia mambo yanavyokwenda ndani ya chama hiki hasa katika kipindi hiki. Mambo hayaendi sawasawa kama inavyotakiwa. Chama hiki kina sinyaa (kimawazo, kiutawala, kuishirikishi n.k.). Chama changu hiki, kinakwenda kinyume kabisa na kanuni zake, kinakwenda kinyume na ahadi zake na kinyume na matarajio, imani na matumaini ambayo wananchi wa Tanzania wamekuwa nayo kwake kwa kipindi kirefu. Matatizo ya chama changu hiki sio matatizo ya wananchi. Ni matatizo ya kimfumo na kiutendaji ndani ya chama chenyewe. Matatizo yake mengi yanasababishwa na matendo machafu ya viongozi wachache wenye nia/tamaa na malengo ya kibinafsi kuliko ya kitaifa. Chama hiki ni chama kinachofifisha matumaini yote yaliyokuwepo kwa wananchi kuhusiana na mustakbal wa Taifa letu. Ni chama ambacho miaka yote nimekipigia kura, na sasa naamini hakistahili tena kura yangu.

Ndugu zangu, Taifa hili lazima liwe la wote. Wale wanaodhani kuwa Taifa hili ni la wote sasa, wanajidanganya, kwa kuwa huo sio ukweli. Wote ni akina nani? Ni wale wanaojiuliza wataishije? Ni wale wanaonyimwa haki ya kupona magonjwa yanayotibika? Je, ni ya wale wanaohitajika kwa viongozi wakati wa uchaguzi tu? Ni wale wanaotakiwa kukaa kimya, wasiulize lolote linalotendwana viongozi wao kwa kuwa kufanya hivyo kutaharibu usalama wa chama (uongo mtupu). Au ni ya wale wanaoweza kuiba na kulindwa na wanaotakiwa kuwachukulia hatua? Ni nchi ya nani hii?

CCM yetu si hii ya sasa. Si hii kwakuwa ile CCM yetu haikuwa ikibagua wanachama wake (CCM wanamtandao na CCM halisi). CCM yetu tuliyoizoea haikuwa ikiandamana na waovu, wahujumu uchumi, wabadhirifu, na wasiojali uTaifa.

CCM inahitaji kukaa chini (hata kama si kwenye vikao vyake kama baadhi wasivyotaka vifanyike), Ijiulize, ina malengo yale yale ama ina malengo mapya? Ijuilize, inasimamia imani zile zile ama ina imani mpya? Ijuilize, inatenda kama inayosema ama inasema isiyotenda? Ijuilize, inatetea maslahi ya umma ama maslahi ya mtu/watu binafsi?
 
- CCM we are fine, kwa sababu hakuna upinzani, mpaka siku utakpopatikana upinzani wa kweli then CCM tutajirekebisha, not now kwa sababu ni clear kwamba sisi wananchi tumeshindwa kujenga upinzani, tunasubiri somebody aje atujengee huku tukilaumu tu bila kufanya anything serious, angalau hata Mrema asiyekuwa na elimu kubwa alijitahidi, sisi wenye elimu kubwa ndio haya!

- Wakuu tukazane tuingie wenyewe huko ndani, hakuna tena wa kutufanyia tukabadilishe wenyewe!

FMES!

I completely agree but you being one amongst many (wananchi) why dont you quit and show us the way into building the true opposition which I realy admire?
 
Katika utaratibu wa kumsaidia mtu mlevi (kama aliyelewa madaraka) ujulikanao kama "Hatua 12). Hatua ya kwanza kabisa inamtaka mhusika kukubali kuwa ana tatizo na ya kuwa hakuweza kulikabili. NI hatua ya "kuown" your problem.

Hadi CCM itakapoanza hapa ndipo itaanza kweli kurudi kwenye misingi yake. NI vigumu sana kutoka denial kwenda acceptance. But slowly, watafika tu hata kwa kulazimishwa au kuanzishwa kauli.

"Hi, mimi ni mwana CCM, na Chama chetu kina matatizo!".

Wana CCM wote rudieni kauli hiyo hadi izame kwenye mitima yenu!

Gombea uongozi ili ufanye unacho kiamini inawezekana wenzako hawana maono kama yako why condeming them in what they dont believe in?
 
SSM inaongozwa na mafisadi na makundi the so called mitandao.
 
....Ndiyo, CCM haina uongozi tena unaoongoza, bali kinaongozwa na viiongozi wanaoongozwa na matukio!

Mzee, Hiyo ni kweli ni kweli kabisa. Hapo umegusa penyewe. Ni matukio tu yanayoongoza viongozi wa CCM. Very true.
 
CCM inaongozwa na nani?
Mwenyekiti ni Jakaya Mrisho Kikwete..kijana wa Pwani asiye na maono ya wapi anataka kuipeleka Tanzania.

makamu Mkiti ni Pius msekwa ambaye nafasi aliyo nayo ni sawa na KK security, hawezi kusema kinyume na mkiti wake..

Mshauri wake ni Kingune Ngombale Mwiru ambaye kwa sababu ya uzee anasubiria fadhila za Rais na ni mshauri ambaye wakati umemtupa na elimu yake na propanganda zilishaganda; Chiligati naye mawazo yake ni mgando kama ya Ngombale.

Viongozi wengine ni Rostam Aziz ambaye na mapedeshee wengi ambao wanafadhili kampeni na walijipatia utajiri kupitia EPA
 
Katika utaratibu wa kumsaidia mtu mlevi (kama aliyelewa madaraka) ujulikanao kama "Hatua 12). Hatua ya kwanza kabisa inamtaka mhusika kukubali kuwa ana tatizo na ya kuwa hakuweza kulikabili. NI hatua ya "kuown" your problem.
NI vigumu sana kutoka denial kwenda acceptance.

Hmmmm....Miafrika Ndivyo Tulivyo kinda falls right along those lines...lol
 
- "Mimi ni M-Tanzania na taifa letu lina matatizo",

- "Mimi ni M-Tanzania vyama vyetu vya siasa vina matatizo",

- "Mimi ni M-Tanzania sisi wananchi wa taifa hili tuna matatizo"

FMES!

Safi sana... tuanzie hapa kwenye utanzania na kuanza kuangalia matatizo yetu,a mbayo ni pamoja na uongozi ndani ya vyama na serikalini. Tuwaangalie kwanza wenye dhamana ya kutuongoza na kisha tuwageukie na wale wanaotafuta dhamana ya kutuongoza.
 
- "Mimi ni M-Tanzania na taifa letu lina matatizo",

- "Mimi ni M-Tanzania vyama vyetu vya siasa vina matatizo",

- "Mimi ni M-Tanzania sisi wananchi wa taifa hili tuna matatizo"

FMES!

This is the classic definition of denial of the first order!
 
wanafalsafa hawawi wafalme!

Ni zaidi ya wafalme!

Wewe unaji consider kuwa mwanafalsafa?

Unataka nani awe mwanafalsafa? wazungu?? au kwako mwanafalsafa ni nani?? anafanya nini??, kwani wewe kitu gani kinatuaminisha kuwa jina lako ni Ng'waninyami?? au unakubali Mwanakijiji jina lake ni Mwanakijiji?? kwa nini usipinge hilo kwanza, ukiweza kuamini Identity yake kwa nini usikubali na hili lingine?? sorry napoteza muda
kifupi ni kuwa, you have inferiority complex and self esteem yako ni kuwa hujitambui!!! hilo ni tatizo, RISE UP MAN!
 
- "Mimi ni M-Tanzania na taifa letu lina matatizo",

Tunakubaliana 100% - sasa swali, matatizo yamekujaje ? Je kuna uwezekano yalipandwa, yakamwagiliwa, yakawekewa mbolea, yakalindwa yasiliwe na ndege, yakakua, yakavunwa kwa wingi na sasa yamehifadhiwa kwenye maghala yanayolindwa usiku na mchana ?

- "Mimi ni M-Tanzania vyama vyetu vya siasa vina matatizo",

Tunakubaliana 100% - sasa swali, matatizo yamekujaje ? soma hapo juu. Tulipanda tukavuna.

- "Mimi ni M-Tanzania sisi wananchi wa taifa hili tuna matatizo"

Tunakubaliana 50% - sasa swali, mtoto anayezaliwa je, tayari ana matatizo? Kama anayo bila shaka kayarithi.

Tusidanganyane, kama wote tunakubaliana kuwa tuna tatizo (ugonjwa) dawa ni kuutibu ugonjwa. Kwa kuwa kuna wanaofaidika na hali hii sasa ni wakati muafaka wa kuwakataa na haya maghala ni lazima yachomwe moto. Kwa kuwa maghala yanalindwa usiku na mchana, hawa walinzi wa maghala haya ya kifisadi lazima tuanze nao kwa kuwachoma moto.
 
Tunakubaliana 100% - sasa swali, matatizo yamekujaje ? Je kuna uwezekano yalipandwa, yakamwagiliwa, yakawekewa mbolea, yakalindwa yasiliwe na ndege, yakakua, yakavunwa kwa wingi na sasa yamehifadhiwa kwenye maghala yanayolindwa usiku na mchana ?

Tunakubaliana 100% - sasa swali, matatizo yamekujaje ? soma hapo juu. Tulipanda tukavuna.

Tunakubaliana 50% - sasa swali, mtoto anayezaliwa je, tayari ana matatizo? Kama anayo bila shaka kayarithi.

Tusidanganyane, kama wote tunakubaliana kuwa tuna tatizo (ugonjwa) dawa ni kuutibu ugonjwa. Kwa kuwa kuna wanaofaidika na hali hii sasa ni wakati muafaka wa kuwakataa na haya maghala ni lazima yachomwe moto. Kwa kuwa maghala yanalindwa usiku na mchana, hawa walinzi wa maghala haya ya kifisadi lazima tuanze nao kwa kuwachoma moto.

- CCM haina uongozi bora kama wa Mbowe na Chadema.

- CCM haina uongozi bora kama wa Mrema na TLP.

- CCM haina uongozi bora kama wa Mbatia na NCCR.

- CCM haina uongozi bora kama wa Lipumba na CUF.

- CCM haina uongozi bora kama wa Cheyo na UDP.

- Smart politics demands kwamba tuwape wananchi choices, tuwape wananchi alternatives badala ya kuwaondolea the little hope they have in CCM bila ya kuwapa replacement, otherwise tunakua wachonganishi tu na kujaribu kuwagombanisha wananchi na viongozi wao waliowachagua wenyewe bila ya kulazimishwa na bunduki.

- Sasa what are the motives za hawa wanaojaribu kutuchonganisha na serikali yetu? ambao wanatumabia kwamba hatuna uongozi mzuri lakini hawatupi alternatives? Maana yake ni kwamba wao ndio wenye akili sana, na wao ndio wanaofaa kutuongoza, is that so?

- CCM tunao viongozi wabovu na wazuri, tunawajua viongozi wengi wazuri wa zamani na wa sasa, mimi ni mkazi wa kijiji cha Kinyerezi, nimezungukwa na high profiles politicains wa zamani na wa sasa ninawaona waliokuwa wazuri na wabovu kwa sababu you can tell kutokana na life style zao, mmoja wa majirani zangu wa karibu sana ni Mzee Apiyo na Mahita, you can tell kwamba Mzee apiyo alikuwa ni kiongozi safi, masikini ya Mungu hana kitu kabisaa, lakini ninawangalia majirani zangu wengine kama Mahita.

- Tunawajua wananchi wengi waliokataa kuwa wezi au kutumiwa na mafisadi, pamoja na juhudi zote za kujaribu kumshawishi kuiba na wezi wa Richimonduli, Jamaa yangu Mkulu Wangu Chidou pale Sheria alikataa kata kata na kubaki na umasikini wake, sasa hatuwezi kuwatukana viongozi wetu wote kwa sababu ya wezi wachache, na hatuwezi kuwatukana wananchi wote kwa sababu kuna wachache bado wasafi, Chidou na Apiyo wanawawakilisha wananchi na viongozi wetu wengi wasafi, dawa ni kuwaondoa hao wachache wachafu, lakini sio kututukana wananchi wote kua hatufai na viongozi wetu, hapana dawa ni kusaidiana kuliokoa taifa letu.

- CCM tuna matatizo ni kweli, kama vyama vingine vyote Tanzania vilivyo na matatizo, sasa hawa mabingwa wa akili basi angalau wangejiunga na chama kimoja cha siasa watuonyeshe maana ya uongozi bora, ambao wanakubali kwamba vyama vyetu vyote Tanzania hazvina.

Wananchi wa Tanzania tunahitaji kuwa macho sana na hawa wachonganishi, wasiokuwa na majawabu ya matatizo yetu, kwa sababu wangekua nayo basi wangejiunga na chama kimojawapo, au wangeanzsiha chama chao kipya cha kutuokoa taifa na matatizo yetu.

Kwenye Halaiki tuliwahi kuimba wimbo mmoja unaoenda like: "....na mtu asiyejua kufa, mwambieni aone kaburi wananchi tulinde taifa wakoloni wasije kurudi Tanzaniaaaaaa...."

Respect!

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Back
Top Bottom