LGE2024 Nani analinda kura ya HAPANA kwa mgombea wa chama kimoja pekee?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

White drone

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2023
Posts
201
Reaction score
386
Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa za mwaka huu hakuna mgombea atakaepita bila kupigwa badala yake kutakuwa na kura ya NDIO au HAPANA kama itatokea mgombea ni mmoja katika nafasi husika.

Vyama vya siasa vina haki ya kuweka mawakala katika vituo vya kupigia kula ikiwa vimetoa wagombea lakini ikiwa havina wagombea hawawezi kuweka mawakala wao.

Swali langu: Ni nani atakaehakikisha kula za HAPANA zinalindwa wakati wa kuhesabiwa ukizingatia hakuna mawakala wa vyama vingine?
 
Hii hoja kubwa..!! Maana hapana zikifika zaidi ya nusu mgombea si anakuwa hajashinda..!!??
 
Tume huru ya uchaguzi inalinda maana ndio maana ya u-huru wa tume.
Nazungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unasimamiwa na TAMISEMI na katika ngazi za vituo unasimamiwa na watendaji wa mitaa ambao ni marafiki wakubwa wa wenyeviti wanaopigiwa kura, katika mukhtadha huo unaona ni rahisi mtendaji kukubali kura za HAPANA ziwe nyingi kuliko kura za NDIO?
 
Vyama vyote vitaweka Mawakala kwenye vituo vyote vya kupigia kura, kwa kuwa kura ya "hapana" nayo ni maamuzi ya wananchi!!

Hakuna SHERIA inayosema usipokuwa na mgombea chama Cha siasa hakiruhusiwi kuweka wakala kwenye kituo Cha kupigia kura. Chaguzi za nyuma waliogopa gharama tu na hawakuwa na la kupigania lkn kwa Sasa watu wao wameenguliwa kiulaghai watahitaji uchaguzi mwingine
 
Umemaliza kila kitu mkuu ikiwa kanuni zinasema hivyo basi kura ya HAPANA italindwa
 
Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa za mwaka huu hakuna mgombea atakaepita bila kupigwa badala yake kutakuwa na kura ya NDIO au HAPANA kama itatokea mgombea ni mmoja katika nafasi husika.

Vyama vya siasa vina haki ya kuweka mawakala katika vituo vya kupigia kula ikiwa vimetoa wagombea lakini ikiwa havina wagombea hawawezi kuweka mawakala wao.

Swali langu: Ni nani atakaehakikisha kula za HAPANA zinalindwa wakati wa kuhesabiwa ukizingatia hakuna mawakala wa vyama vingine?
Mapungufu ya kanuni
 
Ukisema vituo vya kupigia kula wengine watafikiri unazungumzia kwa mama ntilie mambo ya kupiga misosi🤔
 
Yuko sawa ni vituo vya kupigia kula kwa wale wanaoamini ndio wamiliki wa taifa hili.
 
hiyo itategemea nani atahesabu hizo kura na nani atatangaza matokeo yake.!
 
Kila chama kinachoshirki, kitaweka wakala wake kwenye kila kituo. Kumbuka pia kila kijiji kuna wagombea wa halmashauri ya kijiji, ambao watapigiwa kura na kijiji kizima . Hivyo kulinda kura zao kwenye kila kituo ni muhimu.
 
Back
Top Bottom