Nani anamdanganya Rais Samia kuwa kati ya Watanzania mil 65, ni milioni 2 tu wanaolipa kodi?

Punguza jazba.

Kuna direct taxes na indirect taxes. Indirect taxes mpaka mtoto mdogo analipia maana ni consumer based (mtu anapotumia kitu au bidhaa.)

Direct taxes ni presictable na inalipwa moja kwa moja. Hiyo wapiga kelele wengi hawalipi
Umesikia akisema mambo ya direct na indirect ,unaweza ukanifafanulia kwa weledi kuwa kabla ya technology ya kulipa kwa simu kama mafuta ,kodi ya miamala, LUKU na MAJI hiyo indirect walikuwa wanalipaje .

Kwa uelewa wako kiduchu kwa civics ya form two unadhani LUKU sio direct?

USSR
 
Kama aliweza kukubali kuwa kile kilikua kikao cha CHADEMA na Yale yalikua maongezi Yao unategemea nini?
 
Hivi VAT inamaana gani kuwekwa kwenye bidhaa?

Kama hawatambui malengo na mchango wa Vat katika kukusanya kodi, basi kodi hiyo ya kichwa inayotozwa kwa kila mwananchi iondolewe iwapo haitambuliwi wala kuheshimika!
Hata nikinunua vocha ya kero wanakata VAT leo waseme hatulipi kodi

USSR
 
Sijui kuhusu uthabiti wa namba alizotoa, lakini nafikiri point kubwa ni kwamba Watanzania wengi sana, majority, hawalipi kodi wanavyotakiwa kulipa.

Unaweza kuona unalipa kodi katika kununua umeme kwenye Luku, kumbe hiyo bei ya umeme unayolipia kodi imekuwa subsidized na serikali kwa kutumia kodi za wenye viwanda wachache. Kimsingi hapo serikali inatumia pesa za watu wachache wenye viwanda kukulipia wewe umeme wako.

Na unaweza kukuta hizo kodi nyingine zote unazolipa kwenye manunuzi na PAYE hazifikii gharama za huduma za jamii kama barabara, kuunga umeme nchi nzima etc.

Na watu wengi hawana shughuli rasmi kama ajira au biashara na hivyo hawamo sana kwenye mfumo wa kodi, wanashikwa kwenye kodi za mauzo tu.
 
Value Added Tax (VAT) si kila mtanzania analipa , kuna mtu anaweza kukwepa kwsbb kila bidhaa utakayonunua kuna VAT
 
Indirect taxes ni hizo Kodi za mauzo zamani ziliitwa sales tax

Direct tax ni kama PAYE, Income tax na zifananazo

Kodi ya Majengo ikilipwa Halmashauri au TRA ni direct tax

Ikilipwa kupitia Luku ni Indirect tax

Ahsante sana 😄😄
 
shida yako umevimbiwa makande
 
Indirect na direct zote ni kodi tu hakuna jipya hapo mimi nilinunua umeme naona VAT pale naumia kusikia silipi kodi

USSR
Hizi indirect tax zinakuwa kubwa sababu direct tax zinalipwa na wachache mno. Watu M2 ni wachache mno, lazima bei za vitu ziwe juu kupitia indirect tax.
 
Anaongelea registered taxpayers.
Watanzania wengi ambao hawampendi Samia hata akiongea point ni vigumu kukubali.

Na yeye anaharibu zaidi kwa sababu mara nyingi hata akiwa na point nzuri anaiwakilisha vibaya.

Ukweli ni kwamba tax base ya Tanzania, effectively, ni ndogo sana. This is a fact, independent of all politics.
 
Punguza jazba.

Kuna direct taxes na indirect taxes. Indirect taxes mpaka mtoto mdogo analipia maana ni consumer based (mtu anapotumia kitu au bidhaa.)

Direct taxes ni predictable na inalipwa moja kwa moja. Hiyo wapiga kelele wengi hawalipi
Hao wapiga kelele wasiolipa Kodi ni pamoja na yeye
 
Raisi anaongelea direct tax, Indirect tax kila mtu analipa.
Hata kama ni direct tax, bado milioni 2 ni ndogo sana. Na isitoshe, unaposema direct tax maana yake nini? Mama akienda kununua mafuta ya taa kule kijijini Chiungutwa analipa kodi au sio direct tax?
 
Hata kama ni direct tax, bado milioni 2 ni ndogo sana. Na isitoshe, unaposema direct tax maana yake nini? Mama akienda kununua mafuta ya taa kule kijijini Chiungutwa analipa kodi au sio direct tax?
Mama akinunua Mafuta analipa indirect tax
 
Rais hafuatilii anasubiri achakatiwe kila kitu hata kam baadhi ya data zinapikwa yeye anazipokea na kusema.
 
Umesema vizuri kabisa kwamba watanzania wengi hawalipi Kodi ila ulichosahau ni kwamba viongozi wetu ndio wanaongoza kwa kutokulipa Kodi mfano mzuri ni wabunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…