Nani anamdanganya Rais Samia kuwa kati ya Watanzania mil 65, ni milioni 2 tu wanaolipa kodi?

Sasa 50% ya watanzania wote ni below 18 na 60% ni below 25 watalipa vipi Kodi ?
 
Inavyoonekana indirect tax zinaonekana sio kodi. Kiuhalisia watanzania wote tunalipa kodi ila viwango ni tofauti. Huenda walipaji wa pesa nyingi za kodi ni hao 2M ila wote ni walipaji wakubwa tukienda on progressive tax base.
 
Kweli mwanamke anapenda kudanganywa 😂! Pamoja na tozo zote hizo bado anaona watu hawalipi kodi! Kwenye tozo za miamala ni bidhaa gani inanunuliwa mle? Kama sio direct tax ni nini?
 
Jibu swali dogo .je wanaolipa indirect ile pesa haijumulishwi na wale wa direct,zote haziendi kwenye serikali hii hii

USSR
 
Indirect na direct zote ni kodi tu hakuna jipya hapo mimi nilinunua umeme naona VAT pale naumia kusikia silipi kodi

USSR
Nadhani walipaswa kuonyesha idadi ya wanaolipa direct tax na indirect tax kututia moyo sie wanunua LUKU na vocha. All in all, ukiona mwanasiasa anakupa takwimu ya idadi ya walipa Kodi na anakubali kwamba ni wachache ujue mambo ni mambo ni mabaya anatafuta justification ya vitu flani flani kutokwenda vyema.
 
Kama nchi imemshinda aachie
 
Punguza jazba.

Kuna direct taxes na indirect taxes. Indirect taxes mpaka mtoto mdogo analipia maana ni consumer based (mtu anapotumia kitu au bidhaa.)

Direct taxes ni predictable na inalipwa moja kwa moja. Hiyo wapiga kelele wengi hawalipi
Ila wachache sana au amezungumzia wafanyabiashara tu maana hata wafanyakazi through PAYE ni direct tax pia. Kuna miaka kadhaa iliyopita ilikuwa inakadiriwa walipa Kodi wapo kama 3 million na usheee
 
Kachokoza mabeberu pesa imekata anahaha.
 

Mwanzo tuliambiwa walikuwa milioni 3.
 
Hata kama ni ya moja kwa moja bado hiyo namba sio sahihi. Wafanyakazi walioajiriwa sekta binafsi na serikalini wanalipa Kodi ya moja kwa moja kuoitia PAYE. Unataka tuseme wafanyakazi walioajiriwa nchi hii wapo chini ya milion 2?
 
Mtangulizi wake alifanyaje kukusanya kodi?
 
Kama nchi imemshinda aachie
Yeye kuachia nchi tu ni wishful thinking.

Wewe unatakiwa kumfanya aachie nchi.

Wakenya wanafanya motion ya kumu impeach Deputy President, wanataka kumuingiza rais Ruto kwenye impeachment hiyo.

Hawasemi tu "kama nchi imemshinda aachie".

Hakuna mtu anayeachia nchi kwa style hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…