Haya madai yangekuwa na mashiko kama watu wa vijijini ambao ndio wengi zaidi wangekuwa wana barabara za lami, maji ya bomba, shule zenye walimu na hospitali zenye madaktari
Watu wa vijijini hizo huduma walizopelekewa sasa tu hawajaweza kuzi fund vizuri, tumetegemea sana misaada na mikopo.
Sasa unataka wapelekewe huduma zaidi kwa kodi gani wanayolipa?
Mtu mwenye average GDP per capita ya USD 1200 analipa kodi kiasi gani mpaka aweze ku fund huduma za jamii anazopewa?
Watu wamepelekewa umeme wa bei chee na wameshindwa kujiunga kwenye grid.
Na waliojiunga wanalalamika umeme uko bei ya juu, hata baada ya bei ya umeme Tanzania kuwa heavily subsidized na miongoni mwa bei nafuu Africa.
Katika nchi 10 zenye bei ya juu kabisa ya umeme Africa, Tanzania haimo. That is the top 25%.
Lakini watu bado wanalalamika umeme bei ni ghali. Licha ya wafanyabiashara wakubwa wachache kuchukua mzigo mzito kulipia wengi umeme.
Watu wanasema umeme ni ghali, si kwa sababu bei ni kubwa sana kiuhalisia kwa viwango vya kimataifa, hata Africa tu, bali kwa sababu kipato cha watu kiko chini, uchumi mdogo.
Sasa, badala ya ku fix tatizo la msingi la ku fix uchumi uzalishaji uwe effective zaidi, mna focus kwenye kudhibiti matumizi ya viongozi.
Nakubali matumizi ya viongozi ni tatizo. Lakini hilo si tatizo la msingi. Si tatizo la kiini kabisa. Kuna nchi zina viongozi wana natumizi ya kufuru, lqkini wanaweza kuhimiki matumizi hayo, kwa sababu uchumi unazalisha.
Ukidhibiti matumizi ya viongozi bila ya kuwa na mkakati mzuri wa kuongeza uzalishaji, hata hizo fedha itakazookoa kwenye kudhibigi matumizi ya viongozi hutaweza kuzizungusha vizuri upate uchumi mzuri.
Tatizo letu si fedha, tatizo ketu ni ideas na usimamizi wa hizo ideas zipate matunda nazuri.
Hiki ndilo tatizo la msingi, hili hiki tatizo ndilo linalosabqbisha hata matumizi ya viongizi yawe mabaya. Ukiweza kulitatua tatizo hiki, utatatua mambo mawili kwa wakati mmoja.
Utaongwza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza matumizi mabaya.
Hela kama haina project ya maana ya uzalishaji itapotwa tu, sasa unataka kudhibiti matumizi mabaya bila mkakati wa matumizi mazuri?
According to Yahoo Finance, the world’s electricity market is currently valued at over $1
africa.businessinsider.com