Nani anamdanganya Rais Samia kuwa kati ya Watanzania mil 65, ni milioni 2 tu wanaolipa kodi?

Nani anamdanganya Rais Samia kuwa kati ya Watanzania mil 65, ni milioni 2 tu wanaolipa kodi?

Kwahiyo kodi tunazotoa zaenda wapi
Swali la msingi sana. Tunakatwa kodi kwenye kila huduma tunayofanya, tunalipa kodi za maeneo tunayoishi( Majengo), Tunalipa kodi kwenye usafiri, tunalipa kodi kwenye mishahara yetu (PAYE) tunalipa kodi kadha wa kadhaa...... jumlisha idadi ya watanzania na leo tunaambiwa eti only 2mill Tanzanians ndio wanaolila kodi lol
Hapo sijataja kodi wanazokutana nazo wafanyabiashara + makampuni nchini.
 
Si ndio, hili jambo kamishina alishaliongea likaleta mjadala ila still naona bado halieleweki.

Hizi kodi za manunuzi kila mtu analipa, kila mtu si anafanya manunuzi? Mkurugenzi wa benki akinunua mkate si analipa kodi? Akiweka mafuta si analipa kodi? Ila akipokea mshahara anakatwa kodi ya mshahara. Sasa kodi inayoongelewa ni hii kodi ya mshahara.

Kwa ufupi anasema ajira ziongezeke, ujasiriamali uongezeke na ule usio rasmi urasimishwe.
Sio kila mtu anaweza kuelewa hivi.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Nani anaekubali alipwe kwenye m pesa au Benki Ili akatwe? Hapo ni kama mtoa pesa Yuko mbali ,harafu kama hela ni nyingi hawamkubali ukazitoa chap Kwa mara Moja Benki ndio maana watu wanafanya miamala Kwa Fedha mbichi.
Msikie huyu watu hawatumiwi pesa , unajifanya unaishi nje ya nchi

USSR
 
Raisi anaongelea direct tax, Indirect tax kila mtu analipa.
Bodaboda, mama ntilie, mawinga, fundi gereji, seremala, wakulima, wavuvi na wamachinga waanze kulipa direct tax.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
1. Je, ni Watanzania wangapi wanalipia LUKU ya umeme kuna kodi mle na kila siku tunalipa?

2. Tunaambiwa watumiaji wa simu tuko zaidi milioni 29 na kila siku unanunua vocha, tunalipia miamala?

3. Wangapi wanatumia magari yote yanalipiwa kodi na mafuta ukinunua unalipa kodi?

4. Tunalipa kodi tukilioia visimbuzi kila uchawi hiyo sio kodi?

5. Tunaonunua bidhaa kwa lipa namba, tunasafirisha bidhaa kutoka eneo moja hadi lingine bado tunalipa kodi

6. Mishahara yote nchini inakatwa kodi PAE.

NI UKWELI KUWA VAT na PAE tunalipa kila siku na kila mara

USSR

Pia soma:Rais Samia: Tunachokusanya hakiendani na idadi ya watu na shughuli za uchumi zilizopo. Pesa inaenda kwenye mifuko ya watu

Mama amekosea angetakiwa kusema kodi ya mapato. Kodi ya mauzo walipaji ni wengi sana kuanzia kwenye mafuta, madukani, vifaa vya ujenzi, simu, nauli.....
 
1. Je, ni Watanzania wangapi wanalipia LUKU ya umeme kuna kodi mle na kila siku tunalipa?

2. Tunaambiwa watumiaji wa simu tuko zaidi milioni 29 na kila siku unanunua vocha, tunalipia miamala?

3. Wangapi wanatumia magari yote yanalipiwa kodi na mafuta ukinunua unalipa kodi?

4. Tunalipa kodi tukilioia visimbuzi kila uchawi hiyo sio kodi?

5. Tunaonunua bidhaa kwa lipa namba, tunasafirisha bidhaa kutoka eneo moja hadi lingine bado tunalipa kodi

6. Mishahara yote nchini inakatwa kodi PAE.

NI UKWELI KUWA VAT na PAE tunalipa kila siku na kila mara

USSR

Pia soma:Rais Samia: Tunachokusanya hakiendani na idadi ya watu na shughuli za uchumi zilizopo. Pesa inaenda kwenye mifuko ya watu

Wakisha shiba hudhani kila mtu Huwa kesha shiba
 
Kwa hapo anaehesabika ni mlipakodi ni producer sio wewe maana yeye ndio anauza Kwa whole sellers.
Mkuu, hii kodi huwa inahamia kwenye bei mpaka mtumiaji wa mwisho anailipia akinunua bidhaa hata asipopewa risiti.

Mfano mwepesi, Serikali ikiweka kodi kwenye mafuta, mwenye lori atapandisha bei ya usafirishaji wa unga wa kutengeneza mkate, mzalishaji wa mkate atakachofanya ni kupandisha bei ya mkate, muuzaji wa jumla atalipa ila atampandishia bei muuzaji wa rejareja naye atampandishia mnunuzi wa mwisho. Ile kodi ya mafuta amekuja kuilipa mnunuzi anayetaka kula mkate.
Whole sellers anaweza kukuuzia wewe na ukanunua ukijua umelipa.kodi.kumbe hapana.Bila risiti hakuna Kodi umelipa Mzee labda zile ambazo unaona directly kama Huduma za simu,Mafuta nk..
Wholesaler naye si alinunua akalipa hiyo kodi? Alichofanya ni kutaka mteja wake airudishe kwake.
Dai risiti ndio umelipa Kodi , otherwise Kuna producers wengi tuu kwenye informal sector hawalipi Kodi.
Ukidai risiti unamsababisha mwenye biashara alipe kodi halali ya mapato sababu mauzo yake yanakuwa wazi na pia unamfanya na yeye anapoagiza mzigo aombe risiti ili VAT isimuumize utakapomdai risiti hivyo supplier wake naye anajikuta hafichi mauzo and so on and so on. Risiti haihusiani na indirect tax za manunuzi, zile unalipa tu hata usipopewa risiti mkuu.

UKWELI NI KWAMBA RISITI ZINATAKIWA KUTOLEWA NI ILI MAUZO YAWE WAZI KUSIWE NA JANJA JANJA.
 
Ukweli ni kwamba tax base ya Tanzania, effectively, ni ndogo sana. This is a fact, independent of all politics.
Tax base ni pamoja na wanaolipa indirect tax?
Hata hivyo tatizo kubwa zaidi la Tanzania sio Tax base ndogo bali ni matumizi mabaya ya kodi na watawala.
Kukusanya kodi kubwa kwa walalahoi ni kuzidisha kiwango cha umasikini tu, muhimu zaidi ni kuzingatia matumizi ya kodi zenyewe.
 
Sio kila mtu anaweza kuelewa hivi.
Ni kweli, binadamu huwezi jua mambo yote, kuna mambo tutayaelewa kuna mengine kunakuwa na ugumu kidogo mpaka tueleweshane.
 
Hizi indirect tax zinakuwa kubwa sababu direct tax zinalipwa na wachache mno. Watu M2 ni wachache mno, lazima bei za vitu ziwe juu kupitia indirect tax.
Population kubwa ya Watanzania ni watu tegemezi wasiozalisha kabisa, wanaozalisha kidogo sana na masikini hoehae, utapataje kodi kwa kundi kubwa la watu wa aina hiyo??
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Bodaboda, mama ntilie, mawinga, fundi gereji, seremala, wakulima, wavuvi na wamachinga waanze kulipa direct tax.
Mawinga hawatataka kurasimishwa.
 
Population kubwa ya Watanzania ni watu tegemezi wasiozalisha kabisa, wanaozalisha kidogo sana na masikini hoehae, utapataje kodi kwa kundi kubwa la watu wa aina hiyo??
Duh, ni kweli mkuu, sijui labda tubane matumizi, tupunguze ufisadi au kuufuta, ajira rasmi ziongezwe, mikopo kwa vijana waliorasimishwa iongezwe huenda tukapunguza tatizo.
 
Tax base ni pamoja na wanaolipa indirect tax?
Hata hivyo tatizo kubwa zaidi la Tanzania sio Tax base ndogo bali ni matumizi mabaya ya kodi na watawala.
Kukusanya kodi kubwa kwa walalahoi ni kuzidisha kiwango cha umasikini tu, muhimu zaidi ni kuzingatia matumizi ya kodi zenyewe.
Hiyo indirect tax wanaolipa wengi wanatumia huduma zaidi ya wanavyolipa kodi, so on balance wanakuwa net takers.

Watawala wana matumizi mabaya ya kodi lakini sifikiri kwamba nchi ingekuwa na uchumi mzuri, watu wengi wanaolipa kodi inavyotakiwa kwenye mfumo rasmi, hilo tatizo la matumizi mabaya ya kodi lingekuwa kubwa hivyo.

Tatizo la matumizi mabaya ya kidi linaongeza ubaya wa tatizo la tax base ndogo, lakini tatizo la msingi ni tax base ndogo.
 
Wacha upoyoyo, kuna kodi na kuna tozo.

Anayoiongelea Rais mama Samia ni kodi, unayoiongele wewe ni tozo.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Wewe shule ndio ulienda kusomea ujinga, Tozo ni kodi.
 
Bodaboda, mama ntilie, mawinga, fundi gereji, seremala, wakulima, wavuvi na wamachinga waanze kulipa direct tax.
Wakilipa indirectly tax haifiki kwenye pato la taifa ,navyojua iwe direct au indirect zote husika kwenye mfumo

USSR
 
Mkuu, kodi anayoongelea raisi ni kodi ya moja kwa moja itokanayo na shughuli zinazozalisha mapato.

Umefanya kazi au biashara ukapata ujira au faida kisha ule ujira au faida ukakatwa kodi.
Mawinga na bodaboda walipe direct tax/kodi ya moja kwa moja.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom