Nani anamhujumu Rais Samia?

Nani anamhujumu Rais Samia?

Mama uwezo na upeo wake mdogo ndio unamuhujumu..kuna wakati anaongea kama kuwatisha wanaume au kushindana nao wasimuone ye mwanamke..

Ilitakiwa afuate kanuni tu bila kuwatisha kina kassim kama wakati ule alipomsema hadharani kuwa kassim na wenzio mlisema mi rais wa mpito..

Matokeo yake hata mtashindwa kumshauri au kumuelekeza..maana mtahisi ataona mnafanya hivyo sababu yeye ni mwanamke..Mwisho wa siku mnamkubalia kila anachoagiza.

Maana likiharibika inabaki kuwa mwenyewe ndio alisema au alitaka hivyo.

Mama ana kiburi fulani na dharau fulani ya madaraka..we mchunguze.
Hicho huwa kiburi cha Wanawake wote hasa Wanapofanikiwa, huwa wanataka neno lao liwe Alpha na Omega.

Kuhusu huyo PM kuna tetesi zinasema Mama anataka kumpiga chini kabla au baada ya 2025, na mbadala wake awe yule Waziri ambaye mdogo wake naye ni Mbunge.

Uwezo wake wa kupambanua mambo unaweza usiwe mkubwa lakini si ana washauri, awape nafasi hao wamsaidie.
 
Ccm ijitahimini. Mmeharibu nchi,wanaotajirika ni wale tu wachache wanaopewa nafasi. Lakini wananchi walio wengi bado ni masikini sana.

Ukipita vijijini huko watu wanatia huruma. Zamani watu walikuwa wanategemea walau kilimo kiwalishe,lakini siku hizi ardhi imeharibiwa kwa tabia za nchi kilimo chochote siku hizi lazima kitumie mbolea. Ni wachache wenye uwezo wa mbolea. Kilimo siku hizi lazima uwe na pesa pia.

Miaka kumi tu hapo mbele nchi hii kwa mwenendo huu itakuwa na watu masikini kuzidi. Huku nyie ccm mkifanya mambo yoyote ya Umma yakienda vibaya mnawasingizia wapinzani. Na bahati mbaya hata bungeni hawamo. Sasa hizo Sera za wapinzani zinatoka wapi?.
Huenda tatizo ni uwezo hafifu wa akili zetu wote.
 
Back
Top Bottom