Nani anamtumia Mwana FA juu ya ugonjwa wa Corona?

Nani anamtumia Mwana FA juu ya ugonjwa wa Corona?

Tee Bag

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
7,220
Reaction score
5,622
NANI ANAMTUMIA MWANA FA?

Na Thadei Ole Mushi

Mwana FA yupo Karantini au yupo nyumbani?

Wagonjwa wanaojulikana positive si wanawekwa Karantini chini ya uangalizi?

Mbona hajavaa Mask? Wanaomletea Chai, Chakula nk si atawaambukiza wote?

Je ni Nani anahusika kuvitangaza hivi visa? Ni wagonjwa wenyewe au Waziri? Naona Mwana FA na Meneja wa Diamond kashajitangaza wenyewe hata hivyo idadi ya walioambukizwa haikuongezeka au Hawa sio watanzania? Mbona Waziri haongezi idadi ya wagonjwa?

Anadai ametoka S.A juzi na video kaitoa Jana kwa maana hiyo juzi Ni jumanne ndio alirudi ila Jumapili alikuwa nchini kwa kuwa kwenye Uzinduzi wa albam ya Harmonize alikuwepo au tuseme aliondoka Jumapili na kurudi jumanne inawezekana ila angelituambi S.A alienda lini tungemwamini zaidi.

Kwa alichokipost baada ya hii video Ni kuwa malaria Ni hatari zaidi ya Corona kwa kuwa kapona. Kwa maneno haya tahadhari zote ambazo watu walikuwa wanazichukua wataacha kwa kuwa Ni ka ugonjwa kadogo na utapona tu kama yeye. Si tunajua huyu Ni celebrity hivyo vijana wengi watamuamini na kuacha kufuata kanuni za afya.

Nani anamtumia Mwana FA kupotosha jamii? Wizara ya Afya haioni upotoshaji huu wa wazi? Kwa Nini hawamkamati? Wanaomtumia kupotosha kwa nn wasimtumie kuwapa watu Elimu zaidi?

Serikali mbona haitoi tamko? Msanii mkubwa Kama huyu anasikilizwa na watu wengi je tufuate anayoyasema? Maswali Ni mengi kuliko majibu ila swali kuu linabakia Nani Anayemgumia na Kumtuma Mwana FA?

Tunavyozungumza hivi makamu wa pili wa Rais Burkinafaso ameshafariki kutokana na Corona. Mwana FA anatuambia hii ni vimafua tu?

Tuneona Ummy Mwalimu akimtakia kila la Kheri Mwana FA kuwa utavishinda tu hivi virusi mdogo wangu mbona Hao wengine sita wa awali hajawatakia salamu hii na Kheri hii? Nani anamtuma Mwana FA na Kwa malengo gani?

Ole Mushi
0712702602
FB_IMG_1584689298052.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikujibu ktk list ya wagonjwa walotangazwa jana wanaume wawili wenye miaka 40 ni Mwana Fa na sallam_sk...Tangazo la wizara alikutaja majina option ya kujitangaza wamepewa na wizara na haji manara yupo njian anarudi nae tutajua ni postv or negative...ni kweli ugonjwa upo ila autishi km hofu tunayojitia Tee Bag,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kuna mchezo unachezwa. Mtu anaumwa hajawekwa Karantini. Sijui kuna lengo gani lakini bila shaka sio zuri
Mkuu kuwa karantini sio lazima uwe hosp au kwenye kambi... Italy nchi nzima watu mil 60 wapo karantini ndio kusema wapo hosp au makambini? Nop, ni kutojichanganya na wengine ili kuepuka kusambaa kwa ugonjwa
 
Mwana FA yupo sahihi kutoa ile video kwani amewatoa hofu Mashabiki wake na raia wa kawaida wenye hofu kubwa juu ya Corona.(Ni maoni yangu binafsi)

Hata mke wa Waziri mkuu wa Canada alipoumwa Corona alitoa taarifa, wasanii wakubwa na wanamichezo pia wametoa taarifa hata Waziri mkuu wa Spain pia hivyo hakuna tatizo hapo.
 
Back
Top Bottom