Nani anamuelewa Pastor Tony Kapola?

Nani anamuelewa Pastor Tony Kapola?

Tusiwalaum sana watawala waliochoma biblia na quran.
Ni kati ya vitabu hatarishi kwa ustawi wa mwanadam..*

He Who Controls the Narrative Controls the People​

Hasa Biblia mana iko vague sana, mpenda mema ana pa kupita na mpenda mabaya ana njia ya lami pia.
Nyakati zitafuta hivi vitabu na kuipa nafs fikra huru ijitafute kwa mustakabari wake na mazingira yake.
Hata huku kuyumba kwa roman catholic ni mwanzo wa mwisho wake na falsafa za kufikirika kuruhusu imani za kimazingira kurudi juu.
...ujinga ni kuamini huku akili umezifungia ndan
...kizaz cha miujiza hakiko salama.
 
Mkuu siku hizi kinachoongelewa zaidi katika Mahubiri ni logic tu. Sikiliza alivyokuwa anahubiri JOSHUA ndio wengi wanahubiri hivyo hawa wahibiri wa kisasa. Hata wewe ukiweza kuosoma.vizuri na kuielewa utapendwa katika mahubiri yako. Wachungaji wakongwe wengi walikosa hiyo kitu ila vijana wengi wamesoma wanajua kuflow na premises.
Umeongea Point
 
Mbona juzi Nabii Angel alipokuwa Tanzania alimwita my son. Halafu Tony akawa anampigia magoti arudi bongo.
Yah mwanae ndie na huduma ya tony kwa sasa iko chini ya nabii urbet angel ndo maana ameanza kujiita Osborn
 
Wewe umeona mavazi tu ausio??? kwa bongo hakuna pastor anafundisha neno kwa uwezo mkuwa kumshinda huyu jamaa ni kijana ila laiti angekuwa na kanisa dar ningekuwa nasali kwake...!! ni mtumishi pekee kwenye maisha yangu namuona anaongelea neno masaa 4 plus bila kutaja sadaka ni zaidi ya mwalimu wa neno. Watu wanamsifia mwakasege sana nadhani huyu atamfata ni genius aje dar aokoe vijana na kizazi hiki kwa mafundisho pia kwa ustawi wa maisha yake.
Unawajua ma pastors wenyewe au unaropoka ili umuelewa pastor inabidi uwe na maneno machache rohoni ila kama uko vizuri rohoni hauwezi kumuelewa huyu.
 
Anaitwa Antony Kapola
Ana Masters ya Cyber security

Mkewe ana PhD.

Ana kanisa lake Morogoro ndiyo. Ila ana semina karibia Mikoa mingi. Kote huko ulipopataja. Halazimiki kubaki hapo Morogoro

Kanisa lake lipo chini ya Ministry ya Eubert Angel, huyo nabii anaiyemuita baba.

Unaweza kumtafsiri Eubert kama tapeli, ila taifa lake linamuona wa maana. Anasaidia kupooza makali ya vikwazo vya kiuchumi.
Kwa kufanya money laundering si ndiyo?
 
Tony yuko vizuri ila niliamua kumpuuza baada ya kuona anapenda KISWANGLISH. Mahubiri yake ni kwa wenye hela na wasomi. Nimemweka kundi moja na kina Masanja. Pia kujiunga na tapeli wa Zimbabwe inapoteza imani kabisa. Haiwezekani uwe unapiga madili yaliyokaa kimafia halafu hapohapo uwe mchungaji.
Amechagua niche yake huna na Kinge huwezi kukwepa
 
Back
Top Bottom